23/09/2026
β«π BLACK MAMBA - MFALME WA NYOKA AFRIKA.
Habari ya asubuhi
Leo nataka kuwaonya kuhusu nyoka hatari zaidi Afrika - *BLACK MAMBA!*
ANAJULIKANA VIPI?
- Mwili wake sio mweusi! Ni grey/kahawia, lakini *NDANI YA MDOMO NI WEUSI K**A MKAA* - ndio alama yake!
- Mrefu 2.5m - 4.5m - mrefu k**a baiskeli 2!
- Kasi 20km/h - anaweza kukimbia kushinda wewe!
- Kichwa k**a jeneza, macho makubwa
ANAISHI WAPI?
- Sio k**a Green Mamba wa mitini - huyu ni wa chini!
- Anapenda mawe , mashimo ya mchwa,na vichaka.
- Mchana na jioni ndio hutembea - asubuhi mapema na jioni 4-7pm
TABIA YAKE - Tofauti NA GREEN MAMBA:_
Green Mamba anakimbia, *Black Mamba ANAPIGANA!*
Akiona umemzingira:
1. Anainua kichwa juu (1 meter!)
2. Anafungua mdomo mweusi mkubwa
3. Anatoa sauti "HISS"
4. Anauma mara 10-12 haraka!
KWA NINI NI HATARI MARA 10?_
- Sumu 100mg kwa kuumwa moja - 15mg tu inaua mtu!
- *KIFO NDANI YA DAKIKA 20-45 K**A HAKUNA ANTIVENOM!* Haraka zaidi kuliko Green Mamba!
- Sumu inafunga moyo na kupumua
DALILI:
β° Dakika 5: Maumivu makali
β° Dakika 15: Kizunguzungu, kuona mara mbili
β° Dakika 30: Kutapika, kupooza mdomo
β° Dakika 45: Moyo kudunda haraka, kupumua kukatika, KIFO!
JINSI YA KUJILINDA :_
β
Ukienda shamba asubuhi - vaa buti ndefu, piga kelele kidogo aisikie aondoke
β
Usiweke mkono kwa shimo la mawe au mchwa bila kuangalia
β
Usikanyage mawe makubwa bila kuangalia nyuma yake
β
Ukiona ameinua kichwa na mdomo mweusi - RUDI NYUMA POLE POLE, USIKIMBIE GAFLA (atakuona unakimbia)
UKIUMWA:_
β USIFUNGE KAMBA
β USIKATE NA WEMBE
β
Mlaze chini, asitembee kabisa
β
KIMBIA HOSPITALI - HII NI EMERGENCY YA DAKIKA!
Wito wangu:_ Antivenom ya Black Mamba ni ghali sana - Ksh 10,000 kwa vial, unahitaji 10-20 vials! Serikali toa bure!
Niko hapa kwa ajili yenu - Bonny Elder Kilala Snake Bite Safety Advocate Vihiga