Munanta MED CO.LTD

Munanta MED CO.LTD afya na huduma zote zinazohusu AFYA
kuchora ramani na picha za majengo
Tafiti mbalimbali
ujenzi wa

Moja Kati ya Jambo kubwa na La Msingi katika Maisha ya Mwanadamu ni Afya Yake,Zipo Hali mbalimbali katika Mazingira yetu...
12/09/2021

Moja Kati ya Jambo kubwa na La Msingi katika Maisha ya Mwanadamu ni Afya Yake,Zipo Hali mbalimbali katika Mazingira yetu ambazo zinaweza kuwa Hali Hatarishi(Risk) kwa afya zetu
Katika Kuendelea kuimarisha Afya za Jamii Yetu Moja ya Kazi kubwa ni Kupunguza Risk Behavior na Kuongeza Protective Behavior kwa jamii K**a Ufanyaji wa Mazoezi,Kula Mlo unaofaa,Kupunguza matumizi ya Pombe,Kuacha Tumbaku na Mengine Mengi

Pichani ni CEO wetu Dr Juma Muna akiwa katika Moja ya majukumu ya Kila siku k**a yalivyo malengo ya Taasisi yetu

AFYA KWANZA,KWA PAMOJA TUNAWEZA 🇹🇿🙏

15/02/2021
About Blood donation,,,,16/08/2020,,,Oljoro Arusha-Tanzania!!!!!Donate blood Save life!!!BLOOD DONATION BONANZA!!!!!!!
24/08/2020

About Blood donation,,,,16/08/2020,,,Oljoro Arusha-Tanzania!!!!!

Donate blood Save life!!!

BLOOD DONATION BONANZA!!!!!!!

VITA DHIDI YA UGONJWA WA COVID-19 NI YETU SOTEHabari ndugu zangu,poleni na majukumu ya Kulijenga  Taifa letu la Tanzania...
13/05/2020

VITA DHIDI YA UGONJWA WA COVID-19 NI YETU SOTE

Habari ndugu zangu,poleni na majukumu ya Kulijenga Taifa letu la Tanzania,,,

Sote tunajua kuwa tuna changamoto kubwa inayotukabili la Ugonjwa wa(CORONA) COVID-19 ambao kiukweli unahitaji umakini na Kila mmoja wetu kutekeleza maelekezo na miongozo yote jinsi ya kujikinga toka Wizara ya Afya lakini pia shirika la Afya duniani,,,jambo hili linahitaji team work linahitaji Mimi nitimize wajibu wangu na ww utimize wajibu wako ili sote tuwe salama,,,,

Nilibahatika wiki iliyopita kufika maeneo ya mpakani mwa Nchi yetu na Kenya eneo la NAMANGA ,na juzi,Jana na Leo maeneo ya Vijiji vya Tarafa ya Engaranaibo takribani kilometer 107 kutoka Arusha mjini,kilometer k**a 10 kuingia Nchi ya Kenya,eneo hilo lina vijiji zaid ya 11 vinavyochukulia huduma makao makuu ya Tarafa ya Engaranaibor yaani kata ya Engaranaibor pamoja na baadhi ya raia wa kigeni pia wapo maeneo hayo,ni eneo ambalo kuna mwingiliano mkubwa wa wananchi ikiwepo mnada wa Engaranaibor uliofanyika Jana ,mbali na shughuli kubwa kuwa ni ufugaji na kilimo wengi wa wananchi ambao wanazungumza lugha ya kinyumbani peke(Kimasai) uelewa juu ya ugonjwa wa corona bado ni mdogo sana,,,binafsi kwa kuona uhatari uliopo maeneo ya mipakani ili kuilinda Nchi yetu kwa wananchi wa maeneo hayo ya mipakani kuwa salama tulifika k**a MUNANTA MED CO.LTD kutoa elimu juu ya ugonjwa huu wa corona kwa viongozi wa vijiji vya Tarafa ya Engaranaibor,Viongozi wa Kimila ,Waganga wa Jadi,Wakunga jumla zaidi ya 71 na baadae wananchi waliohudhuria mnada wa Engaranaibor ikiwa ni mkakati mmoja wapo kusaidia kufikisha ujumbe wa serikali chini ya Wizara ya Afya juu ya mbinu za kujikinga na janga hili la Ugonjwa wa Corona,Pia tuliwapatia Barakoa 100,Ndoo za Kunawia mikono,na Sabani za kunawia Lita 65,,,

Mbali na Elimu hiyo ambayo ilifikishwa kwa kutafsiriwa kimasai pia Wakazi hao walielekezwa jinsi ya kunawa mikono kwa maji tiririka kwa maji safi na sabuni kwa muda wa sekunde ishirini na Zaidi ,jinsi ya kuvaa Barakoa na Maelekezo mengine ya kitaalamu ambazo pia zitaenda kusaidia taaisis za kidini k**a makanisa na misikiti na maeneo mengine ya mikusanyiko

Zoezi hili litakuwa endelevu nitoe wito kwa sote kuungana hasa kuzijali na kuzipatia elimu jamii zilizo kwenye hatari kubwa hasa maeneo yenye mikusanyiko na sana vijijini ambapo social media hazipo,vyombo vya habari havipo na wengi kipato chao ni cha chini na wengi hawajui hata kiswahili na vyombo vyote vya habari sidhani k**a kuna kinachowafikia kikizungumza kilugha chao cha nyumbani,,tunatajaria kufika kijiji cha KIMWATI ambacho ndio kijiji cha mwisho kuingia Kenya ambapo wananchi wake wanapata huduma za kiafya kituo cha afya ambacho tulichoambiwa kipo maeneo mpakani kabisa

ELIMU NI UFUNGUO WA KILA JAMBO,NILINDE NIKULINDE,NIKINGE NIKUKINGE

MUNGU IBARIKI TANZANIA🇹🇿🙏

Dr Juma A.Muna
CEO &FOUNDER-MUNANTA MED.CO.LTD

Visit us

Www.Munantamed.com

HISTORIA FUPI YA VIRUS VYA CORONAUgonjwa wa COVID-19 ni mpya lakini virus vya corona si vipya,viligunduliwa kwa mara ya ...
19/04/2020

HISTORIA FUPI YA VIRUS VYA CORONA
Ugonjwa wa COVID-19 ni mpya lakini virus vya corona si vipya,viligunduliwa kwa mara ya kwanza na Dr.Almeida mnamo 1964 katika maabara hospital ya Mtakatifu Thomas huko mjini London.Mtaalamu huyo mwanamke alizaliwa mwezi june mnamo mwaka 1930 na alikulia Nchini Scotland.Aliacha kusoma shule ya kawaida akiwa Mdogo na kupata ajira katika maabara.
Maambukizi ya Virus vya COVID19 vimepelekea vikao vikubwa vya wanasayansi kusitishwa,Safari nazo kusitishwa lakini Dunia imeenda mbali zaidi hadi kujitenga kwa mtu mmoja baina ya mwengine(social distancing) na njia Lukuki nyingi nyingine k**a vile kunawa mikono mara kwa mara,Kuvaa Barakoa(mask) k**a njia Za kujikinga zidi ya Maambukizi.
Lakini Swali ni JE tulifikaje hapo!!???
Virus vya Corona(COVID19)au maambukizi yake yalianzia au kutambuliwa kwa mara ya kwanza kabisa Nchini China katika Jimbo na Wuhan,Humbei mnamo December 2019,na kwa sasa ni takriban Mabara sita Duniani yamepata visa vya CoViD19 na Zaidi Ya Nchi 100 zimeathirika na maambukizi.Hivyo basi Kwa kuwa Dunia imejikita katika kuhakikisha watu wanajifunza jinsi ya kutibu ama kujikinga zidi ya maambukizi,Upo umuhimu Mkubwa wa kujua historia ya Virus vya Corona ili kuliweka Janga hili kwenye mikakati kwa kila mmoja wetu.Ya jinsi tunavyoweza kujilinda na kubaki salama zidi ya Virus hivi Hatari.
VIRUS VYA CORONA NI NINI!!????
Virus vya Corona ni kutoka katika kundi kubwa la virus vijulikanavyo k**a Zoonotic viruses(zoonotic ikiwa na maana ni virus vinavyoweza kusambaa kutoka kwa wanyama hadi kwa mwanadamu).Ambapo Virus hivi vinasababisha ugonjwa kuanzia homa ya mafua ya kawaida yaan COMMON COLD,Hadi homa kali ya Mapafu.K**a ilivyotangulizwa kusema kuwa kuna Aina nyingi ya Virus vya Corona na virus hivyo vinapatikana kutoka kwenye makundi mbalimbali ya Wanyama ikiwemo Ngamia,Paka,Popo na Kadhalika.Ambapo miungoni mwa Virus vya corona bado yapo makundi ambayo visa vyake havijapata kutambulika vikiambukiza binadamu.Aina hii ya COVID19 kwa hivi punde ndo imepatikana kuruka kuambukiza Binadamu.Zipo aina nyingine Mbili za virus vya Corona vilivyowahi kutokea mnamo 2002 na Mwaka 2012,vilikuwa vinasababisha homa ya mapafu,Mnamo mwaka 2002 ilisadikika vilitokea kwa Paka, hivi vilijulikana k**a SARSCoV, pia 2012 vilijulikana kam MERS-CoV(middle East respiratory syndrome hivi vilisadikika kuwa vilitokea kwa Mnyama Ngamia.Ingawa virus aina ya COVID19 vinaonesha kushabihiana na Virus vya Corona vilivyotokea hapo awali,lakini Upo utofauti.(TUTAJIFUNZA zaidi utofauti baadae,Ebu tuangazie Dalili na Ishara za maambukizi ya COVID19,Ambapo dalili zake zinafanana sana na zile za mafua ya kawaida(COMMON COLD)
-kikohozi kikavu
-Homa
-kupumua harakaharaka
-shida katika kupumua
Lakini maambukizi makali sana husababisha homa ya mapafu 1.Pneumonia 2.Njia ya hewa kushindwa kufanya kazi.3 figo kushindwa kufanya kazi,pia KIFO.
NAMNA maambukizi yanavyotokea;
Maambukizi ya CoVID19 Hutoka kwa mtu mmoja mwenye maambukizi kwenda kwa mtu mwinginge kupitia Majimaji (droplets) yanayotoka kwenye mfumo wa hewa wa mwanadamu hususan wakati wa kukohoa,kupiga chafya N.k.Na Tafiti zinaonesha kuwa mtu kuanzia anapopata maambukizi hadi kuonesha ishara au dalili za ugonjwa ni Takriban siku 2 hadi 14 na kwa wastani wake ni siku 5.
Tuendelee KUJIKINGA na MAAMBUKIZI ili Tuvuke salama
IMEANDALIWA NA Dr.Mohamed Yusuph Bwamkuu( MD)
MED CO. LTD
Ref.
1.WHO,2.Novel corona virus covid19 situation dashboard 3.CDC 4 global health security

Address

Kimandolu Arusha
Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Munanta MED CO.LTD posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share