Dr innocent shoo

Dr innocent shoo 🩺 Tabibu | Elimu ya Afya kwa Jamii
💬 DM kwa ushauri zaidi
👨‍⚕️ Afya na Ushauri – Dr Shoo.

25/04/2026
Haitakiwa kabisa
11/04/2026

Haitakiwa kabisa

Trachoma/ trakomani ugonjwa wa macho unaosababishwa na bakteria (Chlamydia trachomatis), unaoenea sana kwenye maeneo yen...
09/04/2026

Trachoma/ trakoma
ni ugonjwa wa macho unaosababishwa na bakteria (Chlamydia trachomatis), unaoenea sana kwenye maeneo yenye uhaba wa maji na usafi duni, na husambazwa kupitia mikono michafu, vitu vya pamoja k**a taulo, pamoja na nzi (flies) wanaohamisha maambukizi kutoka mtu mmoja kwenda mwingine.

Kwa kifuoi sana
🦠 Chanzo: Maambukizi ya bakteria
👁️ Huathiri: Macho (hasa ndani ya kope)
🚿 Sababu kuu: Usafi mdogo (uso kutooshwa mara kwa mara, maji haba)
🤝 Huenezwa kwa: Kugusana (mikono, taulo), nzi, na vitu vilivyochafuliwa

Dalili:
1.Macho kuwasha na kutoa uchafu
2.Macho kuwa mekundu
3.Kope kuuma au kuingia ndani (hii ni hatua ya hatari)
4.Kupungua kwa uwezo wa kuona (hata upofu k**a haitatibiwa)

Madhara:
Inaweza kusababisha upofu wa kudumu k**a haitatibiwa mapema

Kinga:
1.Kunawa uso mara kwa mara
2.Kutumia maji safi
3.Kuboresha usafi wa mazingira
4.Kuepuka kushirikiana taulo/vitu vya uso

Tiba:
Dawa za antibiotic (k**a Azithromycin)
Upasuaji kwa waliofikia hatua mbaya

Kukosekana kwa maji ndiyo changamoto kubwa kwenye ugonjwa huu.

Kichaa Cha mbwa Rabies 1. Ni nini?Ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi na huathiri ubongo. Ukishaanza kuonyesha da...
04/04/2026

Kichaa Cha mbwa Rabies
1. Ni nini?
Ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi na huathiri ubongo. Ukishaanza kuonyesha dalili, mara nyingi hauwezi kupata matibabu Tena (unaweza kusababisha kifo).

2. Unaenezwa vipi?
1.Kung’atwa na mbwa mwenye kichaa
2.Kung’atwa au kukwaruzwa na mnyama mwingine aliyeambukizwa (paka, popo n.k.)
3.Mate ya mnyama kugusa jeraha la wazi

3. Dalili zake kwa binadamu
Homa na maumivu ya kichwa
Maumivu au kuwashwa sehemu ya jeraha
Hofu ya maji (mtu hawezi kunywa maji vizuri)
Kuchanganyikiwa au tabia kubadilika
Degedege au kupooza

4. Ufanye nini uking’atwa?
Osha jeraha haraka kwa maji mengi na sabuni (dakika 10–15)
Nenda kituo cha afya mara moja kupata chanjo
Usisubiri dalili zianze

5. Kinga
Chanja mbwa na wanyama wa nyumbani
Epuka wanyama wasiojulikana
Pata chanjo mapema uking’atwa

Kwa kifupi: kichaa cha mbwa ni hatari sana, lakini kinaweza kuzuilika ukichukua hatua mapema.
Dr innocent shoo 👋

We are conducting a series of sessions on NTDs diseases, session after session.Elimu itakua kwa magonjwa ambayo apo Awal...
30/03/2026

We are conducting a series of sessions on NTDs diseases, session after session.
Elimu itakua kwa magonjwa ambayo apo Awali hayakupewa kipaumbele katika jamii lakini yapo na yanaendelea kuadhiri jamii zetu

We thank Almighty God for granting us life and the grace to receive specialized training on diseases that were previousl...
27/03/2026

We thank Almighty God for granting us life and the grace to receive specialized training on diseases that were previously not given priority, including Neglected Tropical Diseases (NTDs), malaria, disasters, and climate change.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kupata mafunzo maalum kuhusu magonjwa ambayo hapo awali hayakupewa uzito unaostahili, yakiwemo magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs), malaria, majanga, pamoja na mabadiliko ya tabianchi.
👋

Raccoon Raccoon ni mnyama mdogo wa porini anayejulikana kwa kuwa na alama nyeusi usoni k**a barakoa. Anafanana kidogo na...
21/03/2026

Raccoon

Raccoon ni mnyama mdogo wa porini anayejulikana kwa kuwa na alama nyeusi usoni k**a barakoa. Anafanana kidogo na mbweha lakini ni tofauti.

ASTHMA ( PUMU )ni ugonjwa wa muda mrefu wa njia za hewa/koo la hewa (mapafu) ambapo mirija ya hewa hubana, kuvimba, na k...
17/03/2026

ASTHMA ( PUMU )
ni ugonjwa wa muda mrefu wa njia za hewa/koo la hewa (mapafu) ambapo mirija ya hewa hubana, kuvimba, na kutoa ute mwingi—hali inayosababisha kupumua kwa shida. Kutokana na kiwango Cha hewa safi kinachoingia au kuvutwa ni kidogo zaidi ukilinganisha na mahitaji ya mwili kwa wakati huo.

SABABU AU VICHOCHESHI VYA UGONJWA WA PUMU.
Asthma husababishwa au kuchochewa na vitu k**a:
Vumbi na chavua (allergens)
Moshi (sigara, kuni, makaa)
Baridi kali
Mazoezi makali
Maambukizi ya njia ya hewa (k**a mafua)
Harufu kali (perfume, kemikali)

DALILI ZA UGONJWA WA PUMU.
Kupumua kwa shida (shortness of breath)
Kukohoa (hasa usiku au asubuhi)
Kubana kwa kifua
Kupiga mlio wakati wa kupumua (wheezing)

🩺 MATIBABU.
Asthma haina tiba ya kuondoa kabisa, lakini inadhibitika vizuri:
Kwa. Kutumia dawa zinatolewa kwenye vituo vya kutolea Huduma za afya Karibu yako

🚨 Dalili za hatari (Emergency)
Mgonjwa akipata:
Kushindwa kuzungumza vizuri kwa sababu ya pumzi
Kupumua kwa shida sana
Midomo au kucha kuwa bluu

➡️ Hii ni hali ya dharura—mpeleke hospitali haraka.
💡 Ushauri
Tumia dawa k**a ulivyoelekezwa
Epuka vumbi na moshi
Fuatilia hali yako mara kwa mara.

Keep following my page for more info.

"Endelea kusonga mbele; kila unachohitaji kitakujia kwa wakati sahihi kabisa kwenye njia yako."
17/03/2026

"Endelea kusonga mbele; kila unachohitaji kitakujia kwa wakati sahihi kabisa kwenye njia yako."

Address

Arusha
Arusha

Telephone

+255756976855

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr innocent shoo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Dr innocent shoo:

Share