Veriafya

Veriafya Tunazungumza afya!

17/08/2026

Unywaji wa maji haufanani, hutofautiana kati ya mtu na mtu kutokana na halijoto ya mazingira yake na shughuli anazofanya ikiwa humtoa jasho sana au la, sikiliza Bingwa Bobezi wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Oswin Mwemezi akifafanua uhitaji sahihi wa maji kulingana na uhalisia wa mtu husika.

Video: Sekoutourerrh

17/08/2026

Share nasi kwenye uwanja wa komenti, wewe unaogopa nini zaidi kati ya Simba, Soda, Juisi na Keki?

17/08/2026

Haishauriwi kuwapa watoto vinywaji vitamu vya viwandani kwani vina kemikali iitwayo ‘High fructose corn syrup’ ambayo hutumika k**a mbadala wa Sukari inayoweza kuwaletea Uraibu na Magonjwa Sugu ukubwani ikiwemo Saratani.

Dkt. Luka Mkeni Lui, Bingwa wa Magonjwa ya Watoto alisisitiza haya kupitia TBC Online Agosti 8, 2026.

Punyeto haisababishi ugumba, lakini inaweza kusababisha mwanaume kushindwa kushiriki tendo la ndoa
17/08/2026

Punyeto haisababishi ugumba, lakini inaweza kusababisha mwanaume kushindwa kushiriki tendo la ndoa

Mahojiano haya tumefanya na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake ...

Uvimbe kwenye kizazi unaweza kusababisha Ugumba au hata kuharibika kwa Ujauzito endapo utatungwa
17/08/2026

Uvimbe kwenye kizazi unaweza kusababisha Ugumba au hata kuharibika kwa Ujauzito endapo utatungwa

Mahojiano haya tumefanya na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake ...

Kutojisafisha vizuri au kutumia taulo zisizo salama wakati wa hedhi kunaweza kusababisha bakteria kuzaliana kwa urahisi ...
17/08/2026

Kutojisafisha vizuri au kutumia taulo zisizo salama wakati wa hedhi kunaweza kusababisha bakteria kuzaliana kwa urahisi kwenye njia ya uzazi. Kwa kuwa shingo ya kizazi huwazi wakati wa hedhi, bakteria hawa wanaweza kupanda juu hadi kwenye mfuko na mirija ya uzazi na kusababisha maambukizi ya via vya uzazi (PID) ambayo yakikaa muda mrefu bila kutibiwa husababisha uvimbe na makovu kwenye mirija ya uzazi, jambo linaloweza kuiziba na kupelekea ugumba.

Ili kujikinga na hatari hii, inashauriwa kubadilisha taulo za k**e (pedi) mara kwa mara kila baada ya masaa 4 hadi 6, kujisafisha vizuri kwa maji safi na salama pamoja na kunawa mikono vizuri kabla na baada ya kubadilisha.

17/08/2026

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Daniel Michael anaeleza dalili kuu zinazoweza kumfanya mtaalamu wa afya kuhisi au kubaini kuwa mwanamke ana uvimbe kwenye kizazi, ambazo ni pamoja na tumbo kuongezeka ukubwa au uvimbe kutoka nje ya eneo la nyonga, maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi au hata siku za kawaida, kushindwa kupata ujauzito, kutoka damu nyingi na kwa muda mrefu wakati wa hedhi, pamoja na kupata maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa au ndogo kutokana na uvimbe huo kukandamiza viungo hivyo.

Video kamili ya ufafanuzi huu inapatikana kwenye Chaneli yetu ya YouTube yenye Jina la Veriafya

17/08/2026

Akizungumza na Veriafya, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Godfrey Chale wa Dkt. Chale Polyclinic iliyopo Mbezi kwa Msuguri anabainisha kuwa tatizo la Ugumba linaweza kusababishwa na jinsia zote yaani mwanamke na mwanaume hivyo inapotokea kuna changamoto ya kupata watoto ni vyema wahusika wote wakapata uchunguzi na matibabu kwa kadri itakayo onekana inafaa.

Ufafanuzi kamili wa mazungumzo haya upo hapa https://youtu.be/A5Qa6RUHWNw?si=pXtj5L89Vn7wTOB-

16/08/2026

Mtu anapokula wanga kwa wingi na hajishughulishi mwilini huwa unageuzwa kuwa mafuta ambayo taratibu kwa muda mrefu yataendelea kujaa kwenye Ini, Mishipa ya Damu na viungo vingine na kupelekea Presha, Figo kufeli na hata Saratani, hivyo ni muhimu kula wanga kulingana na kushughulika kwetu.

Dkt. Luka Mkeni Lui, Bingwa wa Magonjwa ya Watoto alishauri haya kupitia TBC Online Agosti 8, 2026.

Hata baada ya kutolewa kwa uvimbe kwenye kizazi, mwanamke bado anaweza kupata uvimbe mwingine
16/08/2026

Hata baada ya kutolewa kwa uvimbe kwenye kizazi, mwanamke bado anaweza kupata uvimbe mwingine

Mahojiano haya tumefanya na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake ...

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Veriafya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share