Kitonka Medical Hospital

Kitonka Medical Hospital This page is about to show medical services provided from our hospital.

Page hii ni mahususi kwa ajili ya kuwafahamisha Watanzania juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na hospitali yetu.

We are Hiring!!
14/07/2026

We are Hiring!!

08/07/2026

🇹🇿 HERI YA SIKU YA SABASABA! 🇹🇿Leo tunasherehekea Siku ya Saba Saba, siku inayotukumbusha umuhimu wa biashara, uwekezaji...
07/07/2026

🇹🇿 HERI YA SIKU YA SABASABA! 🇹🇿

Leo tunasherehekea Siku ya Saba Saba, siku inayotukumbusha umuhimu wa biashara, uwekezaji na maendeleo ya taifa letu.

Afya njema ndiyo msingi wa mafanikio katika biashara na kazi za kila siku. Kitonka Medical Hospital tunaendelea kujitoa kutoa huduma bora za afya ili kuhakikisha jamii inabaki yenye afya, nguvu na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa Tanzania.

Afya yako ni mtaji wako. Usiache kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara.

17/06/2026

ZOEZI LA TOHARA LINAENDELEA

LIKIZO TIME OFA.
03/06/2026

LIKIZO TIME OFA.

01/06/2026

.
KITONKA MEDICAL YAWEKA KAMBI YA UCHUNGUZI WA BURE WA FIGO KWA WANANCHI
Katika kuendeleza sera yake ya kurudisha kwa jamii, Kitonka Medical Hospital tarehe 30 na 31 mwezi mei 2026 imeendesha kambi maalum ya uchunguzi wa bure wa magonjwa ya figo kwa wananchi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza uelewa wa afya na kuhamasisha jamii kufanya uchunguzi wa mapema.

Kambi hiyo iliyovutia wananchi kutoka maeneo mbalimbali, iliambatana pia na huduma za uchunguzi wa presha, kiwango cha sukari mwilini pamoja na wingi wa damu, huduma ambazo zimeendelea kuwa muhimu katika kubaini mapema magonjwa yasiyoambukiza yanayoathiri idadi kubwa ya watu nchini.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, uongozi wa Kitonka Medical ulieleza kuwa lengo la kambi hiyo ni kusaidia wananchi kupata huduma za msingi za afya bila gharama, huku ukitoa elimu kuhusu umuhimu wa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kutokana na kuchelewa kugundua maradhi.

Wananchi waliojitokeza walipongeza hatua hiyo wakieleza kuwa imewasaidia kufahamu hali zao za kiafya na kupata ushauri wa kitabibu kutoka kwa wataalamu waliokuwa kambini hapo.
Wataalamu wa afya walieleza kuwa magonjwa ya figo mara nyingi hayatoi dalili katika hatua za awali, hali inayowafanya watu wengi kugundulika wakiwa tayari katika hatua hatarishi.

Kutokana na hali hiyo, wananchi wametakiwa kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara, hasa kwa wenye historia ya presha, kisukari au matumizi ya muda mrefu ya dawa bila ushauri wa daktari.

Uchunguzi wa Figo Mara kwa Mara Huokoa Maisha

Eid Mubarak!May Eid al-Adha fill your life with happiness, success, and countless blessings. We appreciate your valued s...
27/05/2026

Eid Mubarak!
May Eid al-Adha fill your life with happiness, success, and countless blessings. We appreciate your valued support and look forward to serving you always.

19/05/2026
18/05/2026

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha upatikanaji wa damu salama nchini, Hospitali ya Kitonka Medical kwa kushirikiana na Taasisi ya Damu Salama ilifanya zoezi maalum la uchangiaji wa damu salama tarehe 16 Mei 2026.

Zoezi hilo lilianza kwa jogging fupi iliyowakutanisha wanachama wa vikundi mbalimbali vya jogging pamoja na wadau wa sekta ya afya, kabla ya washiriki kupata kifungua kinywa na baadaye kushiriki katika uchangiaji wa damu salama.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, uongozi wa Hospitali ya Kitonka Medical ulisisitiza umuhimu wa jamii kujitokeza kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa haraka wa huduma hiyo, hususan wagonjwa wenye changamoto mbalimbali za kiafya.

Aidha, hospitali hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali pamoja na taasisi nyingine za afya katika kampeni za uhamasishaji na uchangiaji wa damu salama, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya kuhakikisha huduma hiyo muhimu inapatikana kwa wakati kwa wahitaji.

Zoezi hilo lilihitimishwa kwa wito kwa wananchi kuendelea kuwa na utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara ili kusaidia kuimarisha akiba ya damu salama nchini.

11/05/2026

Katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani iliyofanyika jana Mei 10, Bakari Shingo alijumuika na taasisi mbalimbali pamoja na vikundi vya michezo katika zoezi maalum la uchangiaji damu lililoambatana na matembezi ya kijamii kutoka Mzambarauni hadi Pugu Kona.
Tukio hilo lililovutia mamia ya wananchi lilikuwa na lengo la kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu salama ili kuokoa maisha ya wahitaji katika hospitali mbalimbali nchini. Washiriki wa matembezi hayo walionyesha mshikamano mkubwa huku wakisisitiza umuhimu wa afya, upendo na kusaidiana katika jamii.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mheshimiwa Bakari Shingo aliwataka wananchi kuendelea kujitokeza katika shughuli za kijamii zenye manufaa kwa taifa, akieleza kuwa uchangiaji damu ni tendo la kibinadamu linaloweza kuokoa maisha ya wengi, hususan kina mama na watoto wanaohitaji huduma za dharura hospitalini.
Aidha, taasisi na vikundi vya michezo vilivyoshiriki vilieleza kuwa ushiriki wao ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali na wadau wa afya katika kuhakikisha upatikanaji wa damu salama unakuwa endelevu. Tukio hilo lilihitimishwa kwa wananchi wengi kujitokeza kuchangia damu pamoja na kutoa ujumbe wa upendo na mshikamano kwa jamii katika maadhimisho ya Siku ya Mama Duniani.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kitonka Medical Hospital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kitonka Medical Hospital:

Shortcuts

Share