Ocean Road Cancer Institute

Ocean Road Cancer Institute Treatment,
Palliative care,
Research,
Diagnostic,
Prevention

Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuwapeleka watoto wao wa k**e wenye umri wa miaka 9 hadi 14 kupata chanjo ya saratani...
10/08/2026

Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuwapeleka watoto wao wa k**e wenye umri wa miaka 9 hadi 14 kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa huo unaoongoza kwa vifo miongoni mwa saratani za uzazi kwa wanawake.

Rai hiyo imetolewa leo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Frank Rutachunzibwa, wakati akitoa mada ya uelimishaji kuhusu saratani kwa watumishi wa Wizara ya Fedha, Mtumba jijini Dodoma.

Dkt.Rutachunzibwa alisema chanjo hiyo hufanya kazi vizuri zaidi kwa watoto ambao bado hawajaanza kujamiiana kwani huwapa kinga dhidi ya maambukizi yanayoweza kusababisha saratani ya mlango wa kizazi baadaye katika maishani yao.

Alibainisha kuwa kila mwaka maelfu ya wanawake hupoteza maisha kutokana na saratani hiyo huku sababu kubwa ikiwa ni kuchelewa kugundua ugonjwa huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mali za Serikali, Choto Sendo aliishukuru Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kwa kutoa elimu ya magonjwa ya saratani na yasiyo ya kuambukiza kwa watumishi wa Wizara hiyo na kusema kuwa elimu waliyoipata pamoja na upimaji watakaofanyiwa utawasaidia kujua hali za afya zao.

Saratani ya mlango wa kizazi ni miongoni mwa saratani zinazoongoza kwa vifo vya wanawake nchini, huku changamoto kubwa ikiwa ni uelewa mdogo na kuchelewa kwa uchunguzi na matibabu. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, chanjo kwa watoto wa umri wa miaka 9 hadi 14 ni njia muhimu ya kinga dhidi ya ugonjwa huo sambamba na uchunguzi wa mara kwa mara kwa watu wazima.

09/08/2026

Waziri Kikwete: Usisubiri kuugua, pima afya yako mara kwa mara

09/08/2026

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wanufaika na zoezi la upimaji wa magonjwa ya Saratani na yasiyo ya kuambukiza kwani mara nyingi hukosa muda wa kwenda hospitali kupima afya hadi wanapougua

Wataalamu wa ORCI wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upimaji wa afya kwa Watumishi wa O...
09/08/2026

Wataalamu wa ORCI wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upimaji wa afya kwa Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mtumba jijini Dodoma.

Zaidi ya watumishi 225 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wamejitokeza kushiriki zoez...
09/08/2026

Zaidi ya watumishi 225 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wamejitokeza kushiriki zoezi la upimaji wa magonjwa ya Saratani na yasiyo ya kuambukiza lililofanyika Mtumba jijini Dodoma na kumalizika hivi karibuni.

Mbali na upimaji huo zoezi hilo pia lilihusisha utoaji wa elimu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza hususan Saratani pamoja na utoaji wa chanjo ya homa ya Ini kwa watumishi ambao hawakuwa wamepata chanjo hiyo.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha zoezi hilo Mkurugenzi wa Kinga na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) Dkt. Crispin Kahesa alisema zoezi hilo limekuwa na mafanikio makubwa na mwitikio mzuri kutoka kwa watumishi.

Alieleza kuwa vipimo vilivyotolewa vilihusisha uchunguzi wa viashiria vya Saratani mbalimbali ikiwemo Saratani ya utumbo mkubwa, ngozi, tezi dume, matiti na mlango wa kizazi pamoja na upimaji wa maambukizi ya VVU pia chanjo ya homa ya Ini ilitolewa kwa wale waliokuwa hawajapata huduma hiyo.

Dkt. Kahesa alibainisha kuwa mwanzoni baadhi ya watumishi hususan wanaume walikuwa na hofu ya kupima hasa kipimo cha Saratani ya tezi dume kutokana na imani potofu iliyopo katika jamii ya upimaji wa Saratani hiyo hata hivyo baada ya kupatiwa elimu sahihi wengi walijitokeza kupima.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mwalibora Mwamtuya aliishukuru ORCI kwa huduma hiyo huku akisema imewasaidia watumishi wengi kufahamu hali zao za afya.

Naye Afisa Tawala na Mratibu wa VVU/UKIMWI na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka ofisi hiyo, Kokolo Lusanda alisema watumishi wengi wamefaidika na zoezi hilo kwani mara nyingi hukosa muda wa kwenda hospitali kupima afya hadi wanapougua.

Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) inaendelea kusogeza huduma za uchunguzi wa Saratani karibu na wananchi ili kuongeza upimaji wa mapema hii ni kutokana na watu wengi kuchelewa kugundulika kuwa na ugonjwa huo hatua hii inalenga kuongeza uelewa na kuhamasisha utamaduni wa kupima afya mara kwa mara.

08/08/2026
07/08/2026

Madhara ya saratani ya matiti kwa wanaume ni makubwa kuliko kwa wanawake

07/08/2026

Unajua unaweza kupata saratani ya matiti ukiwa na umri gani? jibu litakushangaza!

07/08/2026

Je, Unajua Saratani ni nini? Ukweli muhimu unaoweza kuokoa maisha yako

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dkt. Diwani Msemo, ametembelea Hospitali ya Benjamin Mka...
06/08/2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dkt. Diwani Msemo, ametembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha Matibabu, Mafunzo na Tafiti za Saratani hatua inayolenga kuimarisha huduma za kibingwa nchini.

Katika ziara hiyo Dkt. Msemo alipata fursa ya kujionea hatua iliyofikiwa ya mradi huo na kufanya mazungumzo ya kimkakati na Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Prof. Abel Makubi yaliyolenga kuendeleza ushirikiano baina ya taasisi hizo katika kuboresha huduma za saratani.

Akizungumza mara baada ya kuangalia ujenzi huo Dkt. Msemo alieleza kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa kituo hicho na kusisitiza kuwa ORCI iko tayari kushirikiana kwa karibu na BMH ili kuhakikisha kituo hicho kinaanza kutoa huduma za kibingwa, mafunzo kwa wataalamu pamoja na tafiti za kisayansi mara tu kitakapokamilika.

Alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa katika sekta ya afya huku akieleza kuwa ujenzi wa kituo hicho ni hatua muhimu katika kupanua huduma za saratani na kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaotegemea ORCI.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Prof. Abel Makubi aliwataka wakandarasi wa mradi huo Kampuni ya Mohamed Builders pamoja na Mshauri Elekezi wa mradi, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhakikisha wanakamilisha ujenzi kwa wakati uliopangwa ili wananchi waanze kunufaika na huduma hizo muhimu.

Mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 71 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2026 ukiwa na thamani ya Shilingi bilioni 32.

Address

Ocean Road, Luthuli Street
Dar Es Salaam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ocean Road Cancer Institute posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Ocean Road Cancer Institute:

Shortcuts

Share