03/04/2026
JAPO KWA UFUPI ELEWA HAYA MUHIMU๐
โผ๏ธMungu ni niniโ
Chanzo cha kila kitu kilichopo..kinachoonekana na kisichoonekana. Sio kiumbe chenye umbo la kibinadamu, bali ni nguvu hai yenye akili kamili (conscious energy) inayosababisha uhai na mpangilio wa ulimwengu.
Ni ile kanuni ya uwepo yenyewe..ndiyo inayofanya๐..nyota zizunguke kwa mpangilio..mimea ikue bila kufundishwa..maisha yaendelee bila kusimama
๐ Hahitaji kuabudiwa ili kuwepo, tayari yupo ndani ya kila kitu sio umbo fulani bali hali ya Uwepo, upo kwa sababu nipo & nipo kwasababu upo(ubunthu).
๐ Kumjua Mungu sio kumtafuta mbali, bali ni kuelewa uwepo wake ndani yako na katika sheria zinazotawala maisha.
โผ๏ธNeno la Mungu ni niniโ
Ni sheria za maumbile (universal laws)..kanuni zisizobadilika zinazoongoza maisha yote.
Hizi ndizo โsautiโ ya Mungu kwa sababu zinaonyesha jinsi ulimwengu unavyofanya kazi.
Ndizo dini nyingi huzielezea kwa lugha ya picha k**a๐
โMungu alisemaโฆโ
wakimaanisha kuwepo kwa kanuni fulani ya maisha, sio lazima sauti ya moja kwa moja k**a watu wanavyofikiria.
Orodha ya Sheria za Maumbile (Universal Laws)
1.Sheria ya Sababu na Matokeo (Law of Cause & Effect)
๐ Kila tendo lina matokeo, hakuna kinachopotea.
2.Sheria ya Mvutano / Unavuta (Law of Attraction)
๐ Unavuta kile unachokilingana nacho kiakili na kihisia.
3.Sheria ya Uwiano / Balance
๐ Kila kitu kinatafuta usawa, maisha yanarudisha hali zisizo sawa.
4.Sheria ya Mabadiliko / Change
๐ Hakuna kitu kinachobaki vilevile, kila kitu hubadilika.
5.Sheria ya Ndani na Nje (As Within, So Without)
๐ Maisha yako ya nje yanakisi hali yako ya ndani.
6.Sheria ya Mtetemo / Vibration
๐ Kila kitu kina mtetemo, mawazo na hisia zako zina athari kubwa.(pia๐Law of Polarity, Law of Rhythm na Law of Genderโฆ zote zinategemea mtetemo na uwiano wa uhai.)
Kwa ufupi:
7.Sheria ya Uwajibikaji / Responsibility
๐ Wewe ndiye chanzo cha maisha yako, hakuna mwingine.
8.Sheria ya Zawadi / Compensation
๐ Kila jambo nzuri au mbaya linaleta matokeo ya kulingana, malipo ya kazi yako.
9.Sheria ya Umoja / Oneness
๐ Kila kitu kipo ndani ya uhusiano mmoja wa uwepo, kila tendo linaathiri wote.
Hizi hazihitaji kuaminiwa bali zinafanya kazi tu.
๐Biblia, Qurโan (msahafu), na maandiko mengine ya kidini na kiimani huzungumzia sheria za maumbile...lakini mara nyingi kwa lugha ya mifano, hadithi, picha au ishara, sio kwa ufafanuzi wa kisayansi au moja kwa moja ufafanuzi wa kiroho kwa uwazi k**a nifanyavyo..hivyo misahafu yote ni UNIVERSAL LAWS BOOKS ,wewe unaovichukulia k**a vitabu vya dini ndio unaosaga meno usiojua wewe ni nani,kwanini upo hapa,ili iweje na nini hatima yako
๐ฃ๏ธsasa tuendelee na kujibu maswali ๐ฐ๐ฐ
โผ๏ธMbingu ni niniโ
Mbingu siyo sehemu ya mbali hiko angani k**a watu wengi wanavyofikiria. Mbingu ni hali ya ndani ya mtu...hali ya akili na roho kuwa katika amani, utulivu, na uelewa sahihi.
๐ Unaweza kujiuliza..Baada ya kufa, mbingu ipo au hakuna?
Ndiyo, ipo,lakini sio k**a mji wenye nyumba au bustani za kawaida. Ni hali halisi ya kiroho ambapo roho inaishi katika mwanga, amani, na utulivu mkubwa zaidi.
๐ Hivyo ukweli ni huu..
Mbingu unayoianza kuijenga hapa duniani kupitia maisha yako,na baada ya kifo unaendelea nayo kulingana na ulivyoishi na ulivyojijenga ndani yako.
โผ๏ธWewe ni naniโ
Wewe ni roho yenye fahamu, unayotumia mwili huu k**a chombo cha kuishi hapa duniani. Mwili ni wa muda, lakini wewe halisi ni ule unaojitambua ndani yako..ule unaosema โmimiโ.
๐ Swali linaweza kuja: Kwa nini najiona k**a mwili?
Ni kwa sababu maisha yote unatumia mwili kuona, kusikia na kuhisi, hivyo unajikuta unajitambulisha nao.
Lakini ukweli ni kwamba.
Mwili hubadilika, hukua na hata kuisha..lakini ile fahamu yako inaendelea kuwepo.
๐ Hiyo ndiyo wewe halisi.
โผ๏ธWewe unakufaโ
Hapana, hufi. Kinachokufa ni mwili tu.
๐ Swali.. Baada ya kufa naenda wapi?
Unaendelea kuwepo kwenye hali ya kiroho inayolingana na jinsi ulivyoishi na ulivyojijenga ndani yako.
K**a uliishi kwa hofu, chuki na giza, utaendelea kwenye hali hizo.
K**a uliishi kwa uelewa, amani na mwanga..utaendelea kwenye hali hizo.
๐ Kifo hakubadilishi wewe ni nani, kinaendeleza hali uliyoijenga.
โผ๏ธUpo hapa kwa ajili yaโ
Upo hapa kujifunza na kukua kiufahamu kupitia uzoefu.
๐ Swali.. Kwa nini maisha yana changamoto na maumivu?
Kwa sababu maisha yanakufundisha kupitia matokeo.
Mfano.. ukifanya jambo lisilo sahihi, unapata maumivu,hiyo sio adhabu, ni fundisho.
๐ Ni k**a kugusa moto, unaungua ili ujifunze.
Hivyo..
Changamoto = mafunzo
Maumivu = ishara ya kurekebisha
Furaha = matokeo ya kuelewa
โผ๏ธKabla ya hapa ulikuwa wapiโฆโ
Ulikuwa k**a roho, bila mwili huu wa sasa.
๐ Swali..Kwa nini sikumbuki?
Kwa sababu kumbukumbu zako za sasa zinategemea ubongo wa mwili huu.
Ulipoingia kwenye mwili huu, ulianza mfumo mpya wa kumbukumbu.
๐ Lakini uwepo wako haukuanzia hapa..umeingia tu kwenye hatua mpya ya maisha.
โผ๏ธNani alitaka uje Dunianiโฆโ
Katika kiwango cha juu cha ufahamu, roho yako ambaye ndio wewe halisi(roho) ilikubali kuja kupata uzoefu wa maisha ya kimwili.
๐ Swali..Ina maana nilichagua maisha haya yote?
Sio kuchagua kila tukio moja moja, bali kuchagua safari ya kujifunza ambapo changamoto ni sehemu yake.
๐ Hakuna ukuaji bila majaribu.
Ndiyo maana maisha yana vipindi tofauti..vyote vina kusudi la kukuza ufahamu wako.
โผ๏ธShetani ni kitu ganiโฆโ
Shetani sio kiumbe halisi kinachotembea na kukushambulia.
๐ Ni hali ya akili yako na nafsi yako kuwa na...Ujinga.Hofu.Tamaa isiyo na mipaka.Chuki
๐ Swali..Sasa Kwa nini inaonekana k**a kuna nguvu inanivuta kufanya mabaya?
Ni kwa sababu hujaitawala akili yako..hivyo mazoea, tamaa na hisia vinakuwa k**a vinakuongoza.
๐ Ukweli...Vita halisi siyo nje bali ,ni ndani yako, kati ya uelewa (mwanga) na ujinga (giza).Akili yako(mwili) uilishe nafsi yako(mwili wako wa ndani) upendo,haki na hali ya amani ili Roho(wewe) iwe huru
โผ๏ธJehanam ni niniโ
Jehanam ni hali ya mateso ya ndani.
๐ Swali...Baada ya kifo jehanam ipo?
Ndiyo, lakini sio lazima iwe moto wa nje k**a Dini zisemavyo.
Ni hali ya roho kuendelea kuteseka kutokana na hali ya giza iliyoijengwa na mwili(mwili wa nje)+ nafsi(mwili wa ndani wa katikati kabla yako wewe Roho)
Mfano wake unaanza hata hapa duniani....Kukosa amani..Kuishi na hofu..Majuto yasiyoisha
๐ Hiyo tayari ni jehanam ya ndani.
โผ๏ธPeponi ni wapiโฆโ
Peponi ni hali ya amani, furaha, na utulivu wa ndani.
๐ Swali.. Baada ya kifo kuna pepo halisi?
Ndiyo ipo..lakini siyo k**a mfundishwavyo katika dini ukidhani ni eneo lenye bustani ya kawaida ya kimwili,mito ya asali na maziwa, mabikira 72 n.k๐.
Bali ....Ni hali ya kiroho ambapo roho inaishi katika mwanga, utulivu, na furaha ya kweli.
Tofauti ni hii๐
Hapa duniani unaanza kuijenga kwa maisha yako
Baada ya kifo unaendelea nayo
๐ Hivyo hauendi kuanza upya..unaendelea na hali uliyoijenga.
โผ๏ธDunia ni niniโ
Dunia ni darasa la kujifunzia.
๐ Swali.. Kwa nini maisha hayako sawa kwa kila mtu?
Kwa sababu kila mtu yupo kwenye hatua tofauti ya ufahamu na mafunzo.
๐ Lakini ukweli ni huu...Kila mtu anajifunza, hakuna aliyekuja hapa kukaa bure.
Changamoto = mtihani
Watu = walimu
Maisha = somo
โผ๏ธDini hufunza kwa mafumboโ
Big Yes!..Dini nyingi hutumia picha na hadithi kufikisha ujumbe wa kiroho.
๐ Swali..Kwa nini wasiseme moja kwa moja?
Kwa sababu zamani watu walielewa zaidi kwa mifano na hadithi kuliko maelezo ya moja kwa moja.
๐ Tatizo linakuja pale mtu anapochukua hadithi k**a uhalisia bila kuelewa maana yake ya ndani.
Mfano๐
Moto, pepo, malaika..mara nyingi ni alama za hali za kiroho, sio vitu vya kimwili k**a vinavyoonekana akilini mwako
โผ๏ธMWISHO
๐ฃ๏ธJambo la muhimu zaidi
Usiishie kwa kuamini tu..tafuta kuelewa.
๐ Jiulize maswali
๐ Chunguza maisha yako
๐ Elewa sheria za maumbile
Kwa sababu..
๐ Uelewa unakupa uhuru
๐ Ujinga unakuweka kwenye mzunguko wa mateso
Kupitia Ukiroho Elimu, unaanza kuona maisha kwa jicho la ndani..na hapo ndipo unaanza kuishi kwa ufahamu, sio kwa mazoea.
una swali weka chini ktk comment, nikirudi nitakujibu ๐
โ๏ธNaligia Mninoi
-mwanafunzi mahiri katika sayansi ya ukiroho(spiritual science ) na Nguvu za kimungu(divine power) Shekhe Africa Gentleman Siri ya Nyota na Tiba Piva Viva