29/05/2026
SOMO LA 2: Sababu za Kisayansi Zinazofanya Lower Esophageal Sphincter (LES) Kudhoofika na Kusababisha Acid Reflux
⚠️Katika mwili wa binadamu, Lower Esophageal Sphincter (LES) ni mrija wa misuli unaofanya kazi k**a “valve ya usalama” kati ya umio (esophagus) na tumbo (stomach).
Kazi yake kuu ni:
➡️Kufunguka kuruhusu chakula kushuka tumboni
➡️Kufunga mara tu baada ya chakula kupita
⚠️Tatizo la acid reflux huanza pale LES inaposhindwa kufunga vizuri au inapofunguka bila mpangilio.
▶️Kitaalamu: Kwa nini LES inadhoofika?
1. Kuongezeka kwa Homoni ya Progesterone
Progesterone husababisha misuli ya mwili kulegea (smooth muscle relaxation).
👉 Hii ndiyo sababu:
➡️Wanawake wajawazito hupata acid reflux zaidi
➡️Watu wenye hormonal imbalance pia huathirika
2. Kuongezeka kwa Pressure ya Ndani ya Tumbo (Intra-abdominal Pressure)
Shinikizo kubwa tumboni husukuma asidi juu.
Hali zinazochangia:
➡️Unene kupita kiasi (obesity)
➡️Kula chakula kingi kwa mlo mmoja
➡️Mimba ya miezi ya mwisho
👉 Kitaalamu: pressure gradient inasababisha “retrograde movement” ya gastric contents.
3. Lishe yenye Mafuta Mengi (High-fat diet)
Chakula cha mafuta:
➡️Hupunguza kasi ya tumbo kumeng’enya chakula (delayed gastric emptying)
➡️Huongeza shinikizo tumboni
➡️Hulegeza LES kwa muda mrefu
4. Vinywaji Vinavyochochea Relaxation ya LES
➡️Caffeine (kahawa, energy drinks)
➡️Soda (carbonated drinks)
➡️Pombe
Hivi hufanya LES ipoteze “tone” yake ya kawaida.
5. Stress na Mfumo wa Fahamu (Autonomic Nervous System)
Stress huathiri vagus nerve, ambayo inadhibiti mmeng’enyo wa chakula.
Matokeo yake:
➡️Tumbo huzalisha acid nyingi
➡️LES hupata mishtuko ya kufunguka na kufunga bila mpangilio
6. Kuvimba kwa Tumbo (Gastritis / H. pylori infection)
Maambukizi ya bakteria Helicobacter pylori huweza:
➡️Kuongeza acid secretion
➡️Kuharibu lining ya tumbo
➡️Kuchangia reflux ya muda mrefu
7. Kula Haraka na Kutokutafuna Vizuri
Kitaalamu:
➡️Huchangia aerophagia (kumeza hewa nyingi)
➡️Huongeza gas pressure tumboni
➡️Husababisha reflux ya mara kwa mara
Hitimisho
LES inapodhoofika, mfumo wa mmeng’enyo wa chakula unapoteza “direction control”, na hivyo asidi hurudi juu na kuanza kuharibu umio hatua kwa hatua.
Hii ndiyo msingi wa GERD sugu (chronic acid reflux).
Post