07/04/2026
TATIZO LA KUZIDI KWA KIWAGO CHA ACID TUMBONI (ACID REFLUX-GERD)
𝐊𝐀𝐑𝐈𝐁𝐔
Gastroesophageal reflux disease (GERD).
-Ni hali inayotokana na kuzid kwa kiwango cha Acid tumboni (Hydrochloric Acid) ambapo hupelekea kupanda kwa acid kutoka tumboni kuelekea katika koo la Chakula (Oesophagus) na kupelekea kudhurika kwa mfumo wa chakula upande wa juu ambao unahusisha koo la chakula na mdomo pia.
Watu wengi sana wanasumbuliwa na tatzo hili bila wao kujua wanasumbuliwa na tatzo hili na hufikia hatua wengine kudhani wamerogwa kutokana na dalili ya tatzo hili. Tutaangalia dalili ambazo mtu anaweza kugundua kuwa anasumbuliwa na tatzo hili.
DALILI ZA MTU ANAYESUMBULIWA NA KUZID KWA ACID TUMBONI (GERD-Acid Reflux
-Zipo dalili nyingi ambazo huashiria mtu kusumbuliwa na tatizo la kuzidi kwa Acid tumboni,dalili hizo ni zifuatazo:⤵️⤵️
1.🖇️ Kuwaka moto kifuani(Kiungulia) hasa wakati wa usiku au unapolala,hali hii hutokea pia mara baada ya kula.
2.🖇️ Mapigo ya moyo kwenda mbio/kushtuka kwa moyo baadhi ya nyakati.Hali hii hupelekea baadhi ya watu kuhisi wana matatizo ya moyo.
3.🖇️ Kuhisi k**a kichwa kimevurugika na kuhusi kuchanganyikiwa.
4.🖇️ Kusahau mara kwa mara hata vitu vya kawaida kabisa/Kupungua kwa kumbukumbu.
5.🖇️ Kujisaidia choo kigumu k**a cha mbuzi.
6.🖇️ Kuwa na wasiwasi na khofu kubwa na hufikia hatua hata ukipigiwa simu hasa nyakati za usiku moyo huanza kwenda mbio na kujawa na wasiwasi mkubwa.
7.🖇️ Kukosa usingizi ama kushtuka mara kwa mara kutoka usingizini.
8.🖇️ Kupumua kwa tabu baadhi ya nyakati.
9.🖇️ Kupata maumivu ya kichwa ya mara kwa mara kwa baadhi ya watu wenye tatizo hili.
10.🖇️ Kupata kikokozi kisichoisha
11.🖇️ Kuvimba Tonsillitis/mafidofido mara kwa mara.
12.🖇️ Mdomo kuwa mchachu na huwez kupelekea kutoa harufu mbaya ya kinywa.
13.🖇️ Kuhisi k**a kuna kitu kimekwama kooni lakin kila unavyojaribu kukitoa hakitoki
14.🖇️ Kupata fangasi mdomoni(mdomo huanza kutoa ute mweupe ambao una harufu mbaya).
15.🖇️ Huweza kupelekea ukaanza kuota ndoto