21/01/2025
CHANGAMOTO YA UGONJWA WA FIGO:
Figo ni kiungo ambacho hufanya kazi muhimu kwa kuweka miili yetu safi na yenye afya kutokana na uwezo wake wa kutoa uchafu na sumu.
Ingawa kazi ya misingi ni kutoa uchafu mwilini pia hufanya kazi muhimu ua kusawazisha Presha ya damu,kuweka ujazo sawa wa maji maji na viini vingine sawa ktk mwili yaan balanced fluid & electrolytes.
Kwa miaka ya hivi karibuni kumejitokeza wagonjwa wengi wa Kisukari na Shinikizo la damu ambayo imeleta idadi kubwa ya wagonjwa wanaougua ugonjwa sugu wa figo.Hii inatufanya tuwe na msukumo mkubwa zaidi wa kuelewa magonjwa sugu ya Figo,Kinga yake,na matibabu ya mapema.
Figo yaweza kusababisha matatizo makinwa au hata mauti endapo ikishindwa kufanya kazi yake.Kazi zake mbili muhimu ni kutoa uchafu unaoathiri mwili na wenye sumu na kuweka usawa wa maji maji,madini na kemikali.
Baadhi ya dalili ugonjwa wa Figo ni pamoja na;
- Kuvimba uso,miguu na tumbo
- Kukosea hamu ya chakula, kichefuchefu na kutapika
- Shinikizo la damu kuwa juu (Hypertension)
- Anemi (ukosefu wa damu) na kuwa dhaifu
- Changamoto kwenye mkojo
Utambuzi wa changamoto ya Figo:
Ni vyema k**a una shida ya figo kulingana na dalili tajwa hapo juu na nyingine nyingi kufanyiwa uchunguzi kwa ajili ya utambuzi wa haraka na mapema kwani iwapo ikitambulika mapema inaweza kutibika kwa urahisi zaidi na kadiri unavyokua ndivyo na gharama ya matibabu yake huwa juu.
Walio kwenye hatari ya ugonjwa huu ni pamoja na;
- Magonjwa wa kisukari
- Presha (shinikizo la damu)
- Historia ya familia
- Mvutaji tumbaku(sigara),mtu mnene sana
- Mtu aliyetumia dawa za muda mrefu za kutuliza maumivu
Kwa msaada wa ushauri na matibabu wasiliana nami kwa namba 0781 052 052