Afya ya uzazi

Call Website Contact the business

Afya ya uzazi Uliza. Elewa. Linda afya yako. WhatsApp 0716749491/call 0613895091

🩺 Jukwaa la Afya ya Uzazi

Elimu rahisi na sahihi kuhusu afya ya uzazi kwa wanawake na wanaume.

🩸 Hedhi | PCOS | Homoni | Uzazi | Ujauzito | Afya ya Mwanaume

💬 Jifunze.

Tumewasaidia wanaume wengi na changamoto ya Afya ya uzazi  karibu sana
17/10/2026

Tumewasaidia wanaume wengi na changamoto ya Afya ya uzazi karibu sana

UZITO MKUBWA NA AFYA YA UZAZI KWA MWANAUME: UNGANO MBAYA UNAOGHARIMU WENGIWanaume wengi hufikiri uzito mkubwa unaathiri ...
16/10/2026

UZITO MKUBWA NA AFYA YA UZAZI KWA MWANAUME: UNGANO MBAYA UNAOGHARIMU WENGI

Wanaume wengi hufikiri uzito mkubwa unaathiri presha na moyo tu. Kumbe unaenda moja kwa moja kwenye uzazi.

Hivi ndivyo inavyofanya kazi:

1. MAFUTA HUUA TESTOSTERONE

Mafuta mengi hasa tumboni hubadilisha homoni ya kiume (Testosterone) kuwa homoni ya k**e (Estrogen).

Matokeo:
- Hamu ya tendo hupungua
- Mbegu zinakuwa dhaifu na chache
- Nguvu za ujumla zinashuka

Ukiwa na kitambi kikubwa, kiwanda chako cha uzazi kiko kwenye joto kali - na joto huua mbegu.

2. MZUNGUKO WA DAMU UNAZIBA

Uzito mkubwa = Cholesterol + Presha.

Mishipa ya damu inapoziba, damu inashindwa kufika vizuri sehemu ya uzazi. Hii ndio sababu kubwa ya wanaume wanene kupata changamoto ya nguvu na mbegu dhaifu.

3. INFLAMMATION YA KIMYA KIMYA

Mafuta mengi mwilini hutoa sumu inayoitwa inflammation. Hii sumu inashambulia moja kwa moja:

- Ubora wa mbegu
- DNA ya mbegu
- Uwezo wa mbegu kuogelea

Ndiyo maana mwanamume mnene anaweza kuwa na mbegu nyingi lakini nyingi ni dhaifu au zimekufa.

HABARI NJEMA

Utafiti unasema ukipunguza hata kilo 5-10 tu:

✅ Testosterone inapanda hadi 30%
✅ Ubora wa mbegu unaongezeka
✅ Mzunguko wa damu unaboreka

Sio lazima uwe na six-pack. Punguza tu mafuta ya tumbo.

JIONI: KWA WANAWAKE

Jioni nitazungumzia kwa nini uzito mkubwa kwa mwanamke unaharibu ovulation, homoni na nafasi ya kushika mimba.

Kaa karibu.

Unahitaji kujua k**a uzito wako upo kwenye kiwango salama kwa afya ya uzazi? Tuma neno "UZITO" WhatsApp tukupimie BMI na tukupe mwongozo.

KWA NINI UNAWEZA KUFANYA SIKU YA HATARI USIPATE MIMBA?1. SIKU YA HATARI SIO SIKU 1, NI DIRISHAWatu wengi huhesabu tarehe...
16/10/2026

KWA NINI UNAWEZA KUFANYA SIKU YA HATARI USIPATE MIMBA?

1. SIKU YA HATARI SIO SIKU 1, NI DIRISHA

Watu wengi huhesabu tarehe 14 tu. Kumbe yai likitoka kwenye mwanamke, linaishi masaa 12-24 tu.

Mbegu za kiume ndizo zinaishi siku 3 hadi 5 ndani.

Hivyo k**a umefanya tendo siku 5 kabla yai halijatoka, au masaa 24 baada ya yai kufa, mimba haitatokea ingawa kalenda inasema ni "siku ya hatari". Hesabu ya watu wengi inakosea hapo.

2. HOMONI NA MSONGO HUBADILISHA OVULATION

Hata k**a mzunguko wako ni wa siku 28 kila mwezi, ovulation inaweza chelewa au kutotokea mwezi huo kwa sababu ya:

- Msongo wa mawazo
- Kukosa usingizi
- Mabadiliko ya uzito ghafla
- Ugonjwa au homoni kuvurugika

Hivyo siku uliyodhani ni ya hatari, kumbe yai halikutoka kabisa.

3. MWILI WA MWANAMKE HAUCHUKUI KILA MARA

Ili mimba itokee, mambo 4 lazima yakutane kwa wakati mmoja:
a) Yai liwe bora
b) Mbegu ziwe na nguvu
c) Mrija wa uzazi uwe wazi
d) Kizazi kiwe tayari kupokea

Mmoja ukikosekana, mimba haitatokea hata ukifanya siku ya hatari.

ELIMU MUHIMU

Kutopata mimba siku ya hatari sio njia ya uzazi wa mpango. Ni bahati.

K**a bado hutaki mtoto, usitegemee bahati. Tumia njia sahihi inayokubaliana na afya yako.

Hii ni elimu ya jumla. K**a unahitaji kujua dirisha lako la uzazi au njia sahihi kwako, tuma neno "ELIMU" WhatsApp tukuelekeze .

MWANAUME, JE, UNARIDHIKA NA AFYA YAKO YA KIUME?Wanaume wengi hukutana na changamoto zinazowaathiri katika maisha ya ndoa...
15/10/2026

MWANAUME, JE, UNARIDHIKA NA AFYA YAKO YA KIUME?

Wanaume wengi hukutana na changamoto zinazowaathiri katika maisha ya ndoa, lakini wengi huogopa kuzungumza kuhusu hali zao.

💡 Usikimbilie kutumia bidhaa bila kuelewa changamoto yako kwanza. Kila mtu ana hali yake, na hatua sahihi huanza kwa kupata taarifa na mwongozo unaofaa.

📩 Una changamoto au unahitaji kujua zaidi kuhusu BEDROOM PACK?

Nitumie ujumbe INBOX kwa faragha. Nitakusikiliza, nitakuelewa na kukupa mwongozo kulingana na hali yako.

Unakosa ute wakati wa faragha na mwenzi wako tumia hi itakusaidia sana
15/10/2026

Unakosa ute wakati wa faragha na mwenzi wako tumia hi itakusaidia sana

UHUSIANO WA MOJA KWA MOJA  ULIOPO KATI YA NGUVU ZA KIUME/ UUME KUSIMAMA KWA MUDA MREFU NA MZUNGUKO WAKO WA DAMUNguvu za ...
14/10/2026

UHUSIANO WA MOJA KWA MOJA ULIOPO KATI YA NGUVU ZA KIUME/ UUME KUSIMAMA KWA MUDA MREFU NA MZUNGUKO WAKO WA DAMU

Nguvu za kiume = Mzunguko wa damu.

Hivi ndivyo inavyofanya kazi kwa hatua

Hatua 1: Ishara kutoka ubongo
Ubongo ukitoa ishara, mishipa ya fahamu hutoa kemikali inaitwa Nitric Oxide.

Hatua 2: Mishipa ya damu kufunguka
Nitric Oxide inafanya misuli laini ya mishipa ya damu iliyoko kwenye uume itanuke. Mishipa ikitanuka, damu inaingia kwa wingi mara 6 hadi 8 zaidi ya kawaida.

Hatua 3: Damu kushikiliwa
Damu nyingi inapokuja, inakandamiza mishipa ya kurudisha damu. Hivyo damu inabaki hapo na kusababisha hali ya nguvu/UUME kusimama imara.

KWA NINI UKIKOSA MZUNGUKO MZURI WA DAMU, NGUVU INAKOSekANA/ UUME HUSIMAMA LEGELEGE?

1. K**a una mafuta kwenye mishipa, mishipa haitatanuki vizuri - damu kidogo inaingia.

2. K**a una presha au kisukari, kuta za mishipa zimeharibika - haziwezi kutoa Nitric Oxide ya kutosha.

3. K**a unavuta sigara, nikotini inabana mishipa moja kwa moja.

Matokeo Ishara inatoka ubongoni, lakini damu haifiki kwa wingi au haishikiliki.

Ndio maana madaktari wakimkuta mtu ana tatizo hili, jambo la wanachopima ni:
- Presha ya damu
- Sukari
- Cholesterol
- Homoni ya Testosterone

Hizi ndizo zinaamua k**a mzunguko wako wa famu uko sawa au haupo sawa ...........

Usikate tamaa, bado kuna hatua unazoweza kuchukua kuelekea kwenye lengo lako la kupata mtoto.Nimeamua kukushirikisha fee...
13/10/2026

Usikate tamaa, bado kuna hatua unazoweza kuchukua kuelekea kwenye lengo lako la kupata mtoto.

Nimeamua kukushirikisha feedback hizi za wateja wangu wa zamani ambao walinieleza changamoto zao na hatua walizochukua katika safari yao ya kutafuta mtoto.

Kila mtu ana hali yake, na changamoto za uzazi zinaweza kuwa na sababu tofauti. Ndiyo maana ningependa kwanza nikuelewe vizuri, historia ya changamoto yako na hatua ambazo umeshawahi kuchukua, ili tuone ni mwongozo gani unaoweza kukufaa.

Usipoteze matumaini. Nipo hapa kukusikiliza, kukupa elimu sahihi ya afya ya uzazi na kukuongoza kujua hatua zinazofaa kuchukua. Ikiwa kuna haja, tutazingatia pia ushauri na uchunguzi wa kitaalamu wa daktari.

Safari yako ni muhimu, na huhitaji kuipitia bila mwongozo.

🤰🏽 UNATAMANI KUPATA UJAUZITO? ANZA KWA KUIELEWA AFYA YAKO! ❤️Kupata ujauzito kunahusisha mambo mbalimbali, si kutumia vi...
09/10/2026

🤰🏽 UNATAMANI KUPATA UJAUZITO? ANZA KWA KUIELEWA AFYA YAKO! ❤️

Kupata ujauzito kunahusisha mambo mbalimbali, si kutumia virutubisho pekee.

Mambo muhimu ya kuzingatia:
✅ Kuelewa mzunguko wako wa hedhi.
✅ Kula lishe bora yenye virutubisho muhimu.
✅ Kufahamu siku zenye uwezekano mkubwa wa kupata ujauzito.
✅ Kufuatilia afya ya uzazi ya mwanamke na mwanaume.

💡 Kumbuka: Changamoto ya kupata ujauzito inaweza kuwa na sababu mbalimbali. Uchunguzi sahihi ni hatua muhimu ya kujua kinachoendelea.

❤️ Una swali kuhusu afya ya uzazi au maandalizi ya kupata ujauzito?

📩 Nitumie ujumbe inbox ukianza na neno UZAZI

We hii package kwa wanandoa hasa baba itakufaa nimewasaidia watu wengi sana na wamepata matokeo
07/10/2026

We hii package kwa wanandoa hasa baba itakufaa nimewasaidia watu wengi sana na wamepata matokeo

Usikae na tatizo lako huko. Njoo upate suluhu
05/10/2026

Usikae na tatizo lako huko. Njoo upate suluhu

Address

Kivule Matembele Ya Pili
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya ya uzazi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Afya ya uzazi:

Shortcuts

Share