05/08/2026
FAHAMU HAKI NA WAJIBU WAKO K**A MWANACHAMA WA TANNA 📜🤝
Uwanachama wa Tanzania National Nurses Association (TANNA) si tu fursa ya kukua kitaaluma, bali ni nguzo muhimu ya kuimarisha na kutetea taani ya uuguzi na ukunga nchini. Ili kujenga chama imara na chenye sauti, kila mwanachama anapaswa kutambua haki na wajibu wake.
Haki Zako K**a Mwanachama:
⚖️ Kuwakilishwa na kutetewa kisheria na kitaaluma.
🗳️ Kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa viongozi wa chama.
📚 Kupata fursa za mafunzo endelevu ya kitaaluma (CPD).
🤝 Kunufaika na mipango mbalimbali ya ustawi na maendeleo.
Wajib Wako Kwako na Kwa Chama:
💳 Kulipa ada ya uwanachama kwa wakati.
🛡️ Kulinda na kuendeleza maadili mema ya taaluma ya uuguzi.
🏛️ Kushiriki kikamilifu katika shughuli na mikutano ya tawi lako.
Pamoja tunajenga chama imara, chenye sauti, na kinachotetea maslahi ya wauguzi wote!
🔗 Tembelea tovuti yetu: www.tanna.or.tz
📱 Tufuatilie kwenye mitandao ya kijamii:
Hashtags: