01/05/2026
DALILI ZA HATUA YA MWISHO YA KUFELI KWA FIGO End-Stage Renal Disease
Hii ni hatua ambayo figo zinakuwa zimepoteza uwezo wake karibu kabisa (zaidi ya 85–90%). Katika hali hii, sumu na maji huzidi kujikusanya mwilini na kuleta dalili nzito zifuatazo:
DALILI KUU ZA HATUA YA MWISHO
1. Kupungua sana au kukoma kabisa kwa mkojo
Figo hushindwa kabisa kuchuja damu na kutoa maji.
2. Uvimbe mkubwa mwilini uso, miguu, tumbo
Maji yanajikusanya mwilini kwa kiwango kikubwa.
3. Uchovu uliokithiri na udhaifu mkubwa
Mwili hukosa nguvu kabisa kutokana na sumu na upungufu wa damu.
4. Upungufu mkubwa wa damu Anemia
Husababisha ngozi kuwa nyeupe, kizunguzungu na moyo kwenda mbio.
5. Kichefuchefu na kutapika mara kwa mara
Sumu nyingi mwilini huathiri mfumo wa mmeng’enyo.
6. Kupoteza kabisa hamu ya kula
Hali hupelekea kupungua uzito haraka.
7. Kupumua kwa shida Shortness of breath
Maji yanaweza kujaa kwenye mapafu au mwili kushindwa kudhibiti asidi.
8. Ngozi kuwasha sana itching
Sumu zikijikusanya husababisha muwasho mkali wa ngozi.
9. Misuli kukak**aa au kupata degedege muscle cramps
Kutokana na kuvurugika kwa madini mwilini k**a calcium na potassium.
10. Kuchanganyikiwa, usingizi mwingi au kupoteza fahamu
Sumu zinapoathiri ubongo uremia
11. Shinikizo la damu kuwa juu sana na lisilodhibitika
Figo zinaposhindwa, presha huwa ngumu kudhibiti.
12. Maumivu ya kifua au moyo kwenda mbio
Hutokana na maji kuzunguka moyo au madini kubadilika mwilini.
HALI HII NI HATARI SANA:
Mgonjwa katika hatua hii huhitaji matibabu maalum k**a dialysis kusafishwa damu kwa mashine au upandikizaji wa figo ili kuokoa maisha.
USHAURI MUHIMU:
Usisubiri kufikia hatua hii. Pima mapema, dhibiti kisukari na presha, na linda afya ya figo zako kabla hazijafika mwisho.