22/06/2026
FAIDA 5 ZA KUNYONYESHA KWA MAMA MWENYE HEPATITIS B (Hakuna uvimbe kwenye chuchu)
1. Mtoto anapata kinga asilia (antibodies) kutoka kwa maziwa ya mama
🌚Maziwa ya mama yana immunoglobulins na vipengele vya kinga vinavyomsaidia mtoto kupambana na maambukizi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na virusi vya Hepatitis B.
🌚Hii ni kinga ya ziada baada ya mtoto kupata chanjo na HBIG ndani ya saa 12 za kuzaliwa.
2. Lishe bora na kamili kwa ukuaji wa mtoto
🌚Maziwa ya mama yana virutubisho vyote vinavyohitajika kwa mtoto: protini, mafuta mazuri, vitamini, na madini kwa uwiano sahihi.
🌚Hii inasaidia ukuaji wa ubongo, mfumo wa kinga, na mwili mzima wa mtoto.
3. Kupunguza hatari ya mtoto kupata ugonjwa wa manjano (jaundice) kali
🌚Kunyonyesha mara kwa mara husaidia mtoto kutoa kinyesi na mkojo, ambayo inasaidia kuondoa bilirubini nyingi mwilini.
🌚Hii inapunguza hatari ya jaundice ya kiafya (pathological jaundice) ambayo inaweza kuharibu ubongo.
4. Kuimarisha uhusiano wa kimama na mtoto (bonding)
🌚Kunyonyesha kunampa mtoto hisia ya usalama, upendo, na ukaribu wa mwili.
🌚Hii ni muhimu kwa maendeleo ya kisaikolojia na kihisia ya mtoto, na pia inampunguzia mama mafadhaiko.
5 Faida kwa afya ya mama mwenyewe
🌚Kunyonyesha husaidia kupunguza hatari ya saratani ya matiti na ovari kwa mama.
🌚Pia husaidia kurudisha uzito wa kabla ya ujauzito na kupunguza damu baada ya kujifungua kwa sababu inasaidia mshipa wa uzazi (uterus) kujirefusha.
✅MUHTASARI KWA MGONJWA (Unavyoweza kusema):
"Mama, kwa kuwa huna uvimbe kwenye chuchu na mtoto amepata chanjo yake ya kwanza, unaweza kunyonyesha salama. Faida za maziwa ya mama ni kubwa kuliko hatari – mtoto anapata kinga, lishe, uhusiano mzuri, na wewe pia unajikinga na magonjwa. Hakikisha unanyonyesha kwa usafi na unafuatilia chuchu zako kila siku."
TAHADHARI MOJA MUHIMU:
💎K**a chuchu zinapasuka au kuvuja damu – acha kunyonyesha kwa muda na ushauriane daktari, kwa sababu damu inaweza kuambukiza mtoto.
💎Hakikisha mtoto anapata dozi zote za chanjo ya Hepatitis B (kipimo cha 1: saa 12, kipimo cha 2: mwezi 1, kipimo cha 3: mwezi 6).
MUNGU AWABARIKI SANA❤️🙏Madam Becline +255 748672885 ゚viralシ