27/06/2026
MAJANI YA MGOMBA: SIRI KUBWA YA TIBA ASILIA 🌿
Majani ya mgomba yametumika kwa muda mrefu kwa sababu yana virutubisho na kemikali asilia nyingi. Hapa nimekakupangia vizuri ili usome na utumie kwa urahisi:
FAIDA 18 ZA MAJANI YA MGOMBA
👉Afya ya Ndani ya Mwili
1. Kifua & Kikohozi: Chai ya majani ya mgomba husaidia kupunguza matatizo ya kifua na kikohozi kisichoisha.
2. Cholesterol: Kunywa chai husaidia kudhibiti kiwango cha mafuta mabaya yaliyozidi mwilini.
3. Sukari ya Damu: Inatumika jadi kusaidia kusawazisha sukari kwa watu wenye changamoto ya kisukari.
4. Uzito: Inasaidia kupunguza uzito na kuboresha jinsi mwili unavyotumia sukari.
5. Tumbo: Ni msaada mzuri kwa kuhara, gesi tumboni, na maumivu ya ndani ya tumbo.
6. Tezi Dume: Inaaminika kusaidia matatizo yanayohusiana na tezi dume.
7.Nguvu za Kiume: Inatajwa kusaidia wanaume wenye changamoto za nguvu za kiume.
👉Afya ya Ngozi & Uso
8. Mzio & Muwasho: Majani yakioshwa, yakasagwa, hupakwa kwenye ngozi yenye mzio.
9. Scrub ya Asili: Ukisaga na kuchanganya na maji kidogo, husafisha uso na kuondoa uchafu uliojificha.
10. Chunusi & Ngozi: Ina Vitamin C nyingi, hivyo hupunguza chunusi na kuboresha ngozi. Pia hupunguza dalili za kuzeeka mapema.
11. Majeraha: Yakisagwa hupakwa kwenye majeraha madogo kupunguza maumivu na kuzuia bakteria.
12. Kuuma na Mdudu: Yakisagwa na kupakwa sehemu iliyoumwa hupunguza maumivu na muwasho.
Afya ya Nywele & Mdomo
13.Nywele: Maji ya majani yaliyochemshwa yakipakwa kichwani husaidia kuimarisha, kurefusha na kuzuia nywele kukatika.
14. Meno & Ufizi: Kutafuna majani mabichi husaidia maumivu ya jino, vidonda vya ufizi na harufu mbaya mdomoni.
: Juisi ya ndizi yenyewe inasaidia bawasiri, afya ya figo na kupunguza mafuta moyoni. Pia, mizizi ya mgomba ikichemshwa inasaidia wanawake wenye changamoto za hedhi au majimaji sehemu za siri.
NAMNA MBILI ZA KUTENGENEZA CHAI YA MGOMBA
👉Njia ya Kwanza - Kuchemsha Maji Kwanza
1. Chemsha glasi 4 za maji kwa dakika 15-20 mpaka zitokote.
2. Weka majani 10-15 ya mgomba kwenye maji ya moto.
3. Funika, acha kwa dakika 10-15. Koroga, chuja. Chai iko tayari.
👉Njia ya Pili - Kuchemsha Pamoja*
1. Weka majani ya mgomba moja kwa moja kwenye maji.
2. Chemsha kwa dakika 15-20. Ondoa moto, acha dakika 10-15, kisha chuja.
3. : Tumia majani yaliyokaushwa na kusagwa - kijiko 1 cha chakula kwenye glasi ya maji ya moto.
👉 Ushauri wa Tabibu: Ongeza asali mbichi badala ya sukari kuongeza ufanisi.
MAPISHI MAALUM YA NJE
👉Kwa Nywele Zinazokatika
Chemsha majani, acha yapoe. Paka kichwani, sugua taratibu kwa dakika 15. Acha kwa dakika 30 kisha osha kwa maji safi bila sabuni. Rudia mara 3 kwa wiki.
👉Kwa Kupunguza Uzito
Fanya kunywa chai ya majani ya mgomba mara kwa mara k**a sehemu ya mtindo bora wa maisha.
Chanzo: Tabibu Faham Mwetemo
WhatsApp: +255 684 765 575