08/02/2024
*ACIDIC REFLUX au KUCHEUA TINDIKALI NI NINI?.*
*Kuna hali* inaweza kukutokea ambapo *utasikia kiungulia, uchungu mdomoni, kupata shida katika kumeza au kusikia k**a chakula kinakwama kwenye koo au pengine matatizo mengine.* Ni tatizo ambalo linaweza kukutokea muda wo wote lakini mara mara nyingi *litakusumbua zaidi baada ya kula na kuwa zito zaidi pale unapoingia kitandani kulala hadi pengine kusababisha ukakosa kupata usingizi mzuri.* Katika ukurasa huu tutalizungumzia tatizo hili ambalo *kitaalamu huitwa chronic acid reflux au gastroesophageal reflux disease.* Kwa lugha yetu tunaweza kuliita tatizo la kucheua tindikali.
*Kucheua Tindikali Maana Yake Nini?*
๐๐๐๐
*Kucheua tindikali (gastroesophageal reflux disease, au chronic acid reflux) ni hali ambapo mchanganyiko wa chakula wenye tindikali uliopo tumboni kila wakati hupanda juu kupitia umio (esophagus).* Hali hii hutokea kwa sababu vali iliyopo unapoishia umio, lower esophageal sphincter, haifungi vizuri chakula kinapokuwa kimeingia tumboni. *Tindikali, kwa hiyo, hupanda kupitia umio kuingia kooni na kisha mdomoni, na kukufanya usikie ladha ya uchungu.*
Kucheua tindikali na kupata kiungulia, kwa wakati fulani, ni kitu cha kawaida. *Lakini unapopatwa na tatizo hili zaidi ya mara mbili kwa wiki kwa kipindi cha wiki kadhaa mfululizo, na unatumia dawa za kiungulia na antacids na dalili zinakurudiarudia, unaweza kuwa na gastroesophageal reflux disease (GERD).*
*Kumbuka๐ค;* *Ukishakuwa na GERD unahitaji tiba ya mtaalamu, kwa sababu GERD huweza kuleta matatizo makubwa zaidi ya kiafya.*
*DALILI ZA ACIDIC REFLUX;*
*1. Dalili kuu za acid reflux ni kiungulia na kucheua tindikali.*
Watu wengine wana acid reflux bila kiungulia.
*2. Wengine anasikia maumivu kwenye kifua,*
*3. Sauti ya kukwaruza asubuhi au matatizo ya kumeza.*
*4. Unaweza kuhisi kuwa chakula kimekwama kwenye koo, au k**a unakosa pumzi au koo limekabwa.*
*5. Kuhisi uvimbe kwenye koo wakati hakuna uvimbe*
*6. Husababisha kikohozi kikavu au kutoa harufu mbaya kinywani.*
*7. Ukiona kiungulia na kucheua tindikali vinakusumbua kila baada ya muda mfupi -utando laini juu ya umio unaunguzwa kila wakati na tindikali kutoka tumboni.* Hatimaye utando huu huharibika. Tatizo hili likiwa sugu, tabia zako za ulaji na kulala vitabadilika.
Watu tofauti huathirika kwa namna tofauti na acid reflux. *Dalili ambazo huwatokea wengi ni๐๐:*
โ๏ธ. Kuhisi uvimbe kwenye koo
โ๏ธ. Kiungulia
โ๏ธ. Kucheua chakula
โ๏ธ. Hisia kwamba chakula kinakwama kooni
โ๏ธ. Kukohoa
โ๏ธ. Maumivu ya kifuani
โ๏ธ. Shida wakati wa kumeza
โ๏ธ. Kutapika
โ๏ธ. Kukauka koo na sauti kukwaruza.
*Watoto wadogo wanaweza kupata dalili hizo hizo, k**a๐๐:*
๐ฃ๏ธ. Vipindi vifupi vya kutapika vya mara kwa mara
๐ฃ๏ธ. Kulia kupita kiasi, kukataa kula (watoto na vichanga)
๐ฃ๏ธ. Matatizo mengine ya upumuaji
๐ฃ๏ธ. Ladha ya tindikali ya mara kwa mara, hasa ukiwa umelala
๐ฃ๏ธ. Koo linalokwaruza
๐ฃ๏ธ. Kusikia kukabwa ambako kunaweza kumwamsha mtoto
๐ฃ๏ธ. Harufu mbaya akipumua
๐ฃ๏ธ. Shida ya kulala baada ya kula, hasa kwa watoto.
*ACIDIC REFLUX HUSABABISHWA NA NINI??.*
*Acid reflux husababishwa na udhaifu au kulegea kwa vali ya chini ya umio (lower esophageal sphincter).*
Kwa kawaida vali hii hufunga kikamilifu mara baada ya chakula kuingia tumboni. *Lakini ikijilegeza wakati ambapo haitakiwi, mchanganyiko wa chakula wa tumboni hupanda kwenye umio, na kusababisha acid reflux.*
*Vipengele ambavyo vinavyosababisha hali hii kutokea ni pamoja na๐๐:*
*1. Msukumo mkubwa mno kwenye tumbo.* Baadhi ya wanawake wenye ujauzito hupata kiungulia karibu kila siku kwa sababu ya mwongezeko wa msukumo
*2. Aina fulani za chakula (k**a bidhaa za maziwa, chakula kilichojaa viungo au kilichokaangwa) na tabia za kula*
*3. Dawa zikiwa ni pamoja na dawa za asthma, high blood pressure na mzio, pia dawa za kuzuia maumivu, sedatives na anti-depressants.*
4. Hiatal hernia.
*5. Kutofanya mazoezi na mafuta mengi mwilini.*
*Unaweza Kufanyaw Nini Kuzuia Acid Reflux?*
*1. Uweke mwili wako kwenye uzito unaofaa(Punguza uzito)*
*2. Kula chakula kidogo, mara nyingi badala ya milo michache mikubwa*
*3. Jaribu kupunguza mafuta kwa kupunguza siagi, mafuta na bidhaa za maziwa*
*4. Kaa wima wakati wa kula na dumisha mkao au simama wima kwa dakika 45 hadi 60 baadaye*
*5. Acha kulala mara baada ya kula. Kaa angalau saa 3 baada ya kula ndipo ulale*
6. Acha kuvaa nguo zinazobana maeneo ya tumbo. Zinaweza kulibana tumbo na kukamua tindikali ya tumboni ipande kwenye umio
*7. Ulalapo nyanyua kichwa cha kitanda chako nchi 6 hadi 8, kwa kutumia vipande vya mbao. Mito mikubwa haifai.*
8. Acha uvutaji wa sigara
*9. Unaweza kushauriwa kutumia antacids. Fuata maelekezo ya wataalamu wa afya.*
*10. Acha kula chakula kinachosababisha acid reflux.*
*MATIBABU YA KUDUMU YA KIUNGULIA.*
Kuhusu matibabu tunatibu chanzo na kutokomeza kabsa tatizo la acidic reflux, *fika ofisini kwetu maana kila mkoa tuna ofisi zetu au wasiliana nasi kupitia namba za ofisi 0750155946