Jestycuny Health Builder

Jestycuny Health Builder Pona kisukari bila masharti ya kuzuiliwa kula vyakula. Pia epukana na matibabu ya maisha ya kisukari.

USHAURI KUHUSU ULAJI WA CHAKULA KWA  WAGONJWA WA KISUKARI ... Matibabu ya ugonjwa wa kisukari yanagharimu fedha nyingi. ...
17/06/2022

USHAURI KUHUSU ULAJI WA CHAKULA KWA WAGONJWA WA KISUKARI ...
Matibabu ya ugonjwa wa kisukari yanagharimu fedha nyingi. Kwa hiyo ni muhimu kuzuia na kudhibiti athari za kisukari mapema.
Ili kudhibiti ugonjwa wa kisukari mgonjwa anapaswa kupatiwa matibabu sahihi, kufuatilia na kupima afya mara kwa mara pamoja na kuzingatia mtindo bora wa maisha na taratibu zinazofaa za ulaji wa chakula.

Zifuatazo ni kanuni za ulaji unaofaa zinazopaswa kuzingatiwa na mgonjwa wa kisukari:

1.Kula mlo kamili (angalau mara 3 kwa siku) kwa kuzingatia muda mahususi aliojipangia kwani hashauriwi kukaa na njaa kwa muda mrefu.

2.Dhibiti kiasi cha nishati – lishe (wanga) katika chakula ili kisizidi mahitaji ya mwili. Kiasi kitegemee mahitaji ya mtu binafsi.

3.Ongeza ulaji wa vyakula vyenye makapi – mlo kwa wingi. Kiasi kikubwa cha nishati-lishe kitokane na vyakula vya asili ya nafaka isiyokobolewa, mizizi na ndizi za kupika.

Sukari inayotoka katika vyakula hivi hufyonzwa kwa taratibu na hivyo kupunguza kasi ya ongezeko la sukari katika damu.

4.Punguza kiasi cha vyakula vinavyozalisha nishati lishe kwa wingi hususani vyakula vyenye mafuta kwa wingi.

5.Panga utaratibu wa kula chakula na matumizi ya dawa. Iwapo unatumia insulin au dawa za kushusha kiwango cha sukari katika damu unapaswa kujipangia muda wa kula chakula na kumeza dawa ili kuzuia kupungua kwa sukari katika damu. Epuka kukaa kwa muda mrefu bila kula chakula.

6.Kula mbogamboga kwa wingi katika kila mlo.

7.Kula tunda katika kila mlo.

8.Epuka kunywa pombe.

9.Epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi k**a soda, keki, biskuti, p**i na asali.

Kanuni nyingine za kuzingatia ni:

1.Punguza uzito iwapo una uzito uliozidi - au dhibiti uzito wa mwili ili usifikie uzito uliozidi. Ni muhimu kuwa na uwiano sahihi wa uzito wa mwili kulingana na urefu wako.

2.Zingatia usafi na usalama wa chakula

Kwa tiba na ushauri kuhusu kisukari Wasiliana nami kupitia namba 0629981577
WhatsApp 0629981577...

*𝗟𝗘𝗢 𝗧𝗨𝗧𝗔𝗭𝗨𝗡𝗚𝗨𝗠𝗭𝗜𝗔 𝗔𝗜𝗡𝗔 𝗬𝗔 2 𝗬𝗔 𝗨𝗚𝗢𝗡𝗝𝗪𝗔 𝗪𝗔 𝗞𝗜𝗦𝗨𝗞𝗔𝗥𝗜*Aina ya 2 hutokea wakati kongosho linapopunguza uzalishaji wa insuli...
13/06/2022

*𝗟𝗘𝗢 𝗧𝗨𝗧𝗔𝗭𝗨𝗡𝗚𝗨𝗠𝗭𝗜𝗔 𝗔𝗜𝗡𝗔 𝗬𝗔 2 𝗬𝗔 𝗨𝗚𝗢𝗡𝗝𝗪𝗔 𝗪𝗔 𝗞𝗜𝗦𝗨𝗞𝗔𝗥𝗜*

Aina ya 2 hutokea wakati kongosho linapopunguza uzalishaji wa insulini au wakati insulini haiathiri seli namna ifaavyo.

Baada ya kuzitambulisha kwa ufupi aina hizi mbili za ugonjwa wa kisukari, tunaendelea na makala hii kwa kuzingatia aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari.

Ni yapi yanayohusiana na aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari?

Aina ya 2 ya kisukari ni ugonjwa ulioenea zaidi duniani.

Ni nani aliye katika hatari?
Kila mtu ana kiwango tofauti cha hatari ya kupata aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari.

Kiwango cha hatari kinahusishwa na mtindo wa 1: maisha
2: umri
au sababu za kimaumbile (jenetiki).

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazopelekea mtu kuwa kwenye hatari ya kupata aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari:

*kuwa na uzito wa kupita kiasi

*kutokujishughulisha kimwili mfano kutofanya mazoezi ya viungo

*kuwa na umri wa miaka 45 au zaidi

*kuwa na historia ya ugonjwa wa kisukari,, aina ya 2 katika familia
kuwa na asili ya Waafrika Weusi, Waafrika wa Karibiani, au Asia ya Kusini.

Ni muhimu kukumbuka kwamba unaweza kupata aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari bila kuwa na historia yoyote ya ugonjwa huo katika familia.

Na pia kuwa na historia ya ugonjwa huu katika familia haimaanishi kuwa utaupata. Jambo la msingi zaidi ni kuelewa sababu zinazoathiri kiwango chako cha hatari ya kuupata.

Nini hutokea unapokuwa na aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari?

Watu wenye aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari wanaweza kupata dalili kadhaa.

Zifuatazo ni baadhi ya dalili ambazo ni kawaida kutokea:

*kwenda haja ndogo mara nyingi sana, haswa wakati wa usiku.

*kuhisi kiu kuliko kawaida

*kuhisi uchovu sana

*kupungua uzito bila sababu

*mikato au vidonda kuchukua muda mrefu kupona

*uwezo hafifu wa kuona (kuona ukungu).

Baadhi ya watu hawatambui dalili zao kwa muda mrefu. Kwahiyo ni muhimu uelewe ni nini kinakuweka hatarini. Ikiwa haujatibiwa.

KWA USHAURI 0629981577
WhatsApp: 0629981577

Address

Mbeya

Opening Hours

Monday 08:00 - 19:00
Tuesday 08:00 - 19:00
Wednesday 08:00 - 19:00
Thursday 08:00 - 19:00
Friday 08:00 - 19:00
Saturday 08:00 - 19:00
Sunday 10:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jestycuny Health Builder posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Jestycuny Health Builder:

Share