22/02/2022
New health herbal clinic
Search New Health Wiki
Submit
Kupimwa kisukari
Katika sura hii:
Sura: Kisukari
Kisukari ni ugonjwa gani?
Kisukari aina ya 2 husababishwa na nini?
Kwa nini watu wengi wana kisukari?
Kupimwa kisukari
Kuendelea kuwa mwenye afya hata ukiwa na kisukari
Kudhibiti sukari kwenye damu kwa kutumia dawa
Zuia na kudhibiti matatizo ya kisukari
Kisukari k**a fursa ya pili
Juhudi za jamii dhidi ya kisukari
Dharura za kisukari
Madawa
Kiwango cha sukari kwenye damu kinaweza kupimwa kwa kipimo cha damu au mkojo. Kipimo cha damu huwa na uhakika zaidi.
Nani anapaswa kupimwa?
Mtu anaweza kupimwa kwa ajili ya kisukari k**a:
Ana dalili za kisukari.
Kuna mtu kwenye familia yake ambaye ana kisukari.
Ana kiuno kikubwa au kiribatumbo na zaidi ya umri wa miaka 40.
Ana historia ya shinikizo la juu la damu.
Alijifungua mtoto mkubwa sana (zaidi ya kilo 4).
Ana umri mdogo na ana dalili zinazoweza kuwa za Kusukari Aina ya 1.
Vipimo vya damu
Aina zote za kisukari zinaweza kugundulika kwa kupima viwango vya sukari kwenye damu. Mfanyakazi wa afya anaweza kukupima vipimo tofauti kwa ajili ya kisukari au anaweza kurudia kipimo. Vipimo vinaweza pia kutumika kukidhibiti kisukari kwa kukusaidia kuangalia matokeo kulingana na mabadiliko ambayo unafanya katika ulaji wako, kujishughulisha, au dawa.
Vipimo vya damu hupima iwapo kiwango cha sukari kwenye damu ni sawa, au k**a kiko juu kiasi, au k**a kuna ugonjwa wa kisukari. K**a sukari kwenye damu iko juu lakini siyo kufikia kiwango cha kuashiria kisukari, mtu anaweza kuzuia kupata kisukari kwa kula vyakula vyenye afya, na kufanya mazoezi zaidi.
Kuna vipimo 2 vya kawaida vya kisukari, FBS na A1C.
Kipimo cha sukari kwenye damu kabla mtu hajala chochote -FBS au FPG). FBS au FPG ndiyo kipimo kikuu. Kipimo hiki hufanyika asubuhi kabla mtu hajala chochote. Baadhi ya kliniki hupima sukari kwenye damu kwa kutumia kifaa cha glukomita, kwa kupima tone la damu kutoka kwenye ncha ya kidole. Au kliniki inaweza kuchukua damu kwenye bomba la