23/06/2026
๐จTutaongea yote kuhusu Yanga, lakini nadhani hatupaswi kushangaa sana kwasababu hii timu tunayoona sasahivi imeshuka imekuwa on top kwa miaka minne mfurulizo, imepiga watu Tano, sita za kutosha tu.
Tena ikiwa inatawala kweli kweli, hapo imefika Fainali ya CAF Confederation, na robo Fainali ya Champions league ikiwa ni miaka zaidi ya 20 hawajawahi kufika.
Dominance ya aina hii ulitegemea lazima ipo siku watapitia kipindi kigumu, kwasababu hakuna timu haipitii kipindi cha mpito. Hawa viongozi walioifikisha kule wanaweza tena wakawafikisha juu, hakuna haja ya kupanic.
Vipo vingi ambavyo vimewafanya wafike hapa na ni uzembe wa viongozi, mfano yale mabadiriko ya makocha walofanya last season mpaka season hii ๐ค, mambo ya failures za usajili n.k.
Ni muda wa kuandaa Project mpya, hii imeshafika mwisho. Hakuna haja ya Zimamoto.