Lugarawa Health Training Institute

Lugarawa Health Training Institute Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Lugarawa Health Training Institute, Medical and health, P. O Box 380, Njombe.

DIrisha la Udahili awanu ya pili sasa limefunguliwa
05/08/2026

DIrisha la Udahili awanu ya pili sasa limefunguliwa

Leo katika Mahafali ya 26 ya Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lugarawa, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mheshimiwa Olivanus Thomas, ...
31/07/2026

Leo katika Mahafali ya 26 ya Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lugarawa, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mheshimiwa Olivanus Thomas, aliwahimiza wahitimu kuwa wabunifu, wachapakazi na wenye kujituma katika kutekeleza majukumu yao ya kitaaluma. Alieleza kuwa katika kipindi cha sasa wasomi ni wengi, hivyo mafanikio na utofauti wao vitategemea uwezo wa kubuni suluhisho, kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma zenye ufanisi na ubora.

Aidha, aliwasihi kuitumia elimu waliyoipata kuleta mabadiliko chanya katika jamii kwa kutoa huduma za afya zenye weledi, maadili na ubunifu, huku wakichangia maendeleo ya sekta ya afya na taifa kwa ujumla.

Katika hotuba yake, Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lugarawa (LUHETI), Ndugu Buteye Dotto Buteye, aliwakumbusha wahit...
31/07/2026

Katika hotuba yake, Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lugarawa (LUHETI), Ndugu Buteye Dotto Buteye, aliwakumbusha wahitimu kuwa kuhitimu masomo si mwisho wa safari ya kujifunza, bali ni mwanzo wa jukumu kubwa la kitaaluma na kijamii. Aliwahimiza kuitumia elimu waliyoipata k**a nyenzo ya kuokoa maisha ya watu na kutoa huduma bora za afya kwa kuzingatia maadili ya taaluma, upendo, huruma, utu na usawa kwa wagonjwa wote bila ubaguzi wa aina yoyote.

Aidha, aliwasisitiza kuendelea kujifunza na kujiendeleza kitaaluma ili waendane na mabadiliko ya teknolojia na maendeleo katika sekta ya afya, huku wakidumisha uaminifu, uwajibikaji na weledi katika maeneo yao ya kazi.

Leo, tarehe 31 Julai 2026, Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lugarawa (LUHETI) imefanya kwa mafanikio Mahafali ya 26, ambapo wa...
31/07/2026

Leo, tarehe 31 Julai 2026, Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lugarawa (LUHETI) imefanya kwa mafanikio Mahafali ya 26, ambapo wahitimu kutoka kozi mbalimbali wametunukiwa vyeti na diploma baada ya kukamilisha masomo yao.

Wahitimu walitoka katika fani za:
🔹 Maabara ya Tiba
🔹 Maabara ya Sayansi na Teknolojia
🔹 Uuguzi na Ukunga
🔹 Utabibu
🔹 Ufundi Sanifu wa Dawa

Mgeni Rasmi katika sherehe hizi alikuwa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ndugu Antony Mtaka. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Ndugu Olivanus Thomas, Mhashamu Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe, Askofu Eusebius Kyando, pamoja na wageni wengine mbalimbali waalikwa walioongeza heshima katika tukio hili muhimu.

Tunawapongeza wahitimu wote kwa hatua hii muhimu ya mafanikio na tunawatakia kila la heri wanapoendelea kulitumikia taifa kwa weledi, uadilifu na moyo wa huduma kwa jamii.

Hongereni Wahitimu wa Mahafali ya 26!

Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lugarawa inakupongeza kwa uongozi wako mahiri na mchango wako mkubwa katika kuendeleza sekta ...
28/07/2026

Taasisi ya Mafunzo ya Afya Lugarawa inakupongeza kwa uongozi wako mahiri na mchango wako mkubwa katika kuendeleza sekta ya afya mkoani Njombe. Tunakutakia mafanikio na afya njema unapoendelea kulitumikia taifa.

23/07/2026
heri ya siku ya Sabasaba🎉
07/07/2026

heri ya siku ya Sabasaba🎉

Address

P. O Box 380
Njombe
389

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Lugarawa Health Training Institute posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share