Hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Songea

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Songea Ukurasa rasimi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Songea

WANAFUNZI WA SKILL PATH WAGEUZA WODI YA HOSPITALI YA SONGEA KUWA SEHEMU YA FURAHASi kila dawa huja kwenye chupa wakati m...
28/08/2026

WANAFUNZI WA SKILL PATH WAGEUZA WODI YA HOSPITALI YA SONGEA KUWA SEHEMU YA FURAHA

Si kila dawa huja kwenye chupa wakati mwingine, huja kupitia moyo wa mtoto.

Wanafunzi wa Skill Path English Medium Primary School ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamefanya ziara ya kijamii katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Songea, wakitoa zawadi na faraja kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.

Afisa Muuguzi Msaidizi aliyekuwa Msimamizi wa zamu, Sairice Mbena, alisema ziara hiyo imewapa wagonjwa faraja, matumaini na moyo wa kuendelea kupambana na changamoto za kiafya.

“Tunashukuru sana uongozi wa Skill Path kwa kufikiri kuwatembelea wagonjwa wetu,” alisema Mbena.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Skill Path English Medium Primary School, Rashidi Ayasi, alisema lengo la ziara hiyo ni kuwafundisha watoto upendo kwa vitendo, kuwajali wengine na kushiriki katika shughuli za kijamii.

Ziara hiyo inaonesha kuwa elimu bora si darasani pekee; inajenga pia kizazi kinachojua kuhurumia, kusaidia na kugusa maisha ya wengine.

UPENDO KWA VITENDO: WANAFUNZI WA SKILL PATH WAGAWA FURAHA KWA WAGONJWA HOMSOAfisa Muuguzi msaidizi ambaye alikuwa msimam...
28/08/2026

UPENDO KWA VITENDO: WANAFUNZI WA SKILL PATH WAGAWA FURAHA KWA WAGONJWA HOMSO

Afisa Muuguzi msaidizi ambaye alikuwa msimamizi wa zamu, Sairice Mbena ameushukuru uongozi wa Skill Path English Medium Primary School kwa hatua ya kuwaleta wanafunzi kutoa faraja kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.

Akizungumza baada ya kutoa zawadi hizo leo 27/8/2026 amesema wanafunzi hao wamekuwa faraja kubwa kwa wagonjwa na kuwatia moyo kitendo ambacho kimewajengea imani kubwa kubwa wagonjwa na matumaini katika kuimarika kwa afya zao.

“Tunashukuru sana uongozi wa SKILL PATH kwa kufikiri kuwatembelea wagonjwa wetu. Amesema Mbena.

Kwa upande wake Mwl.Mkuu wa Skill Path English Medium Primary School Rashidi Nyenje Ayasi amesema lengo ni kuwajengea watoto upendo wajue kuwa kuna watu wahitaji wajue kuwasaidia.

Vilevile kuwajengea wanafunzi utamaduni wa kumjali mwenzake na kushiriki katika shughuli za kijamii.

WATUMISHI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SONGEA WATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA IRINGA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYAWat...
28/08/2026

WATUMISHI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SONGEA WATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA IRINGA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA

Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa kwa ajili ya kumarisha huduma za afya na kunadilishana ujuzi wa utoaji wa huduma

Ziara hiyo imeongozwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea Dkt. Magafu Majura. Ambaye amepita katika jengo la Magonjwa ya Dharura (EMERGENCY DEPARTMENT) na kuona watumishi wa eneo hilo namna wanavyotoa huduma kwa wagonjwa.

Vile vile, Dkt. Majura alipita katika Ofisi ya Ustawi wa Jamii na kujua namna Ofisi hiyo inavyofanya kazi katika kuwahudumia wagonjwa wasiojiweza.

Wakati wa kikao cha majumuisho baada ya kufanya ziara hiyo wamesema katika maeneo mengine waliyopita wameona huduma nzuri zikitolewa kwa wagonjwa. Hii ni sehemu ya wao kujifunza na kubadilishana uzoefu na wanaenda kuyafanyia kazi yote waliyopata baada ya ziara yao ya mafunzo.

Dkt. Majura ametoa shukrani kwa Uongozi na watumishi wote kwa ushirikiano mzuri ambao wameupata katika ziara hiyo.

ya Rufaa ya Mkoa Iringa

UONGOZI WA SONGEA RRH WAFANYA ZIARA YA KIKAZI HOSPITALI YA KANDA MBEYA KWA AJILI YA KUBADILISHANA UZOEFUUongozi wa Hospi...
28/08/2026

UONGOZI WA SONGEA RRH WAFANYA ZIARA YA KIKAZI HOSPITALI YA KANDA MBEYA KWA AJILI YA KUBADILISHANA UZOEFU

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea umefanya ziara ya kikazi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuimarisha utoaji wa huduma za afya.

Ziara hiyo imeongozwa na Mganga Mfawidhi Dkt. Magafu Majura ambaye ameambatana na wakuu wa idara mbalimbali za hospitali hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mganga Mfawidhi amesema ziara hiyo ni fursa muhimu kwa hospitali hizo kujifunza kutoka kwa kila mmoja, huku akieleza kuwa uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali kupitia miundombinu, vifaa tiba na wataalamu katika Hospitali hapo unaweza kuwa chachu ya kujifunza na kuimarisha huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songea.

“Tumekuja hapa Mbeya kujifunza kutoka kwa wenzetu. Kuna mambo mengi mazuri wanayofanya hapa ambayo tukienda kuyatekeleza Songea yatasaidia sana kuboresha huduma na kupunguza rufaa zisizo za lazima”alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Dkt. Godlove Mbwanji amesisitiza umuhimu wa ubunifu katika utoaji wa huduma, kujenga mahusiano mazuri baina ya viongozi na watumishi, pamoja na kuweka mikakati ya kuwapa motisha watumishi k**a sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wao katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Uongozi wa Hospitali ya Kanda Mbeya umepongeza ziara hiyo na kuahidi ushirikiano wa pamoja ili kuhakikisha huduma za afya zinaimarika zaidi katika Mikoa yote miwili.

TAWI LA YANGA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SONGEA LASHEREHEKEA SIKU YA YANGA KWA MATENDO YA HURUMATawi la Young Africans H...
09/08/2026

TAWI LA YANGA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SONGEA LASHEREHEKEA SIKU YA YANGA KWA MATENDO YA HURUMA

Tawi la Young Africans Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea limeadhimisha Siku ya Yanga kwa kuwatembelea na kuwapa zawadi za matendo ya huruma wagonjwa waliolazwa. Wametoa mahitaji ya msingi, ikiwa ni sehemu ya kurejesha tabasamu na kuwafariji wagonjwa wakati wa matibabu.

Akizungumza baada ya kutoa zawadi hizo, leo 9 Agosti, 2026 mwakilishi wa tawi hilo la hospitalini Bw. Onesmo Matindiko amesema wameamua kuifanya Siku ya Yanga kuwa tofauti kwa kutoa faraja kwa wagonjwa “Badala ya kushangilia tu uwanjani, leo tumekuja kushangilia ndani ya wodi. K**a timu yetu inapigania ushindi, sisi tunapigania uhai na upole kwa jamii,” amesema Matindiko.

Uongozi wa hospitali umeishukuru Yanga Tawi la Hospitali kwa ukarimu huo na kusema umetoa faraja kubwa kwa wagonjwa. Wamesema matendo ya namna hiyo yanatia nguvu wagonjwa na kuwakumbusha kuwa jamii ipo pamoja nao katika kipindi kigumu cha ugonjwa.

SIMBA RUVUMA YACHANGIA DAMU UNITI 40 HOMSO KATIKA HITIMISHO LA WIKI YA SIMBA KIMKOAKitengo cha Damu Salama Hospitali ya ...
05/08/2026

SIMBA RUVUMA YACHANGIA DAMU UNITI 40 HOMSO KATIKA HITIMISHO LA WIKI YA SIMBA KIMKOA

Kitengo cha Damu Salama Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea kimeushukuru uongozi wa Chama cha Simba Sports klabu Mkoa wa Ruvuma kwa mchango wa damu uniti 40 katika hitimisho la wiki ya Simba Kimkoa. Akizungumza Afisa Mhamasishaji kwenye swala la uchangiaji damu Bw. Saidi Lauma amesema mchango huo ni mkubwa na utatoa msaada wa haraka kwa wagonjwa wengi wanaohitaji damu hospitalini, hususani kina mama wajawazito, watoto na wale waliopata ajali.

Bw. Lauma amewapongeza Simba kwa kuonesha muamko mkubwa wa hamasa miongoni mwa wanachama na mashabiki. Wamesema uwepo wa Simba umevunja ukimya na woga wa watu wengi ambao walikuwa wakidhani kutoa damu ni zoezi la watu wachache tu.

Vile vile, wataalamu wa Damu Salama wametumia fursa hiyo kutoa elimu kwa wanachama wa Simba kuwa mtu anaweza kuchangia damu kila baada ya miezi 3 kwa wanaume na miezi 4 kwa wanawake. Wamesisitiza kuwa si lazima kusubiri hadi maadhimisho ya Simba Day ndipo zoezi lifanyike.

Mwenyekiti wa Chama cha Simba Sports klabu Mkoa wa Ruvuma Garindua Mgaya amesema wanajivunia kuwa sehemu ya wale wanaopigania uhai wa wananchi na sio ushindi uwanjani tu. Simba imekuwa nguzo ya matumaini kwa jamii kupitia mchango wao wa kuchangia damu.

Katibu wa Simba Sports klabu Mkoa wa Ruvuma Boniface Ndomba amesema lengo kubwa la kuchangia damu ni kutaka kusaidia wanchi wenye uhitaji wa damu ili kuokoa maisha yao. Ambapo kila mfano wa damu unaotolewa na mwanachama ni ushindi wa kuinusuru familia moja kutoka kwenye majonzi.

Msemaji wa Simba Sports klabu Mkoa wa Ruvuma Alois Mavugo, amesema ni mapenzi yao kwa wananchi ndiyo sababu kuu iliyowafanya wameamua kutoa damu ili iweze kuwasaidia. K**a Simba wamezoea kupambania alama uwanjani, sasa wameamua kupambania uhai kwa kutoa damu, kwa kuwa uhai wa mwananchi mmoja ni ushindi mkubwa zaidi kwao.

VIONGOZI WA TANNA TAWI LA SONGEA RRH WAPEWA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO JUU YA UTUNZAJI WA FEDHAViongozi wa Chama cha Wau...
04/08/2026

VIONGOZI WA TANNA TAWI LA SONGEA RRH WAPEWA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO JUU YA UTUNZAJI WA FEDHA

Viongozi wa Chama cha Wauguzi na Wakunga Tanzania TANNA Tawi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea RRH wamepatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo kuhusu utunzaji wa fedha na kanuni za uhasibu.

Mafunzo hayo yametolewa na Mtunza Hazina wa Chama cha TANNA Tanzania Emelia Mwakanyanga amesisitiza umuhimu wa viongozi wa ngazi ya tawi kufuata miongozo ya kitaifa ili kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za chama.

Katika mafunzo hayo viongozi wamefundishwa namna ya kuandaa taarifa za mapato na matumizi, uhifadhi wa nyaraka za kifedha, na jinsi ya kupanga bajeti ya shughuli za tawi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TANNA Tawi la Songea RRH Emmanuel Ndumbaro amesema ujuzi waliopata utawasaidia kusimamia mapato na matumizi kwa uwazi zaidi, na kuhakikisha rasilimali za TANNA Tawi la Songea RRH zinatumika kwa manufaa ya wanachama wote.

Naye, Katibu wa TANNA Tawi la Songea RRH Mary Ndunguru ameahidi kwenda kufanyia kazi mafundisho waliyoyapata ili kuboresha utunzaji wa fedha ngazi. Amesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati na yatawasaidia viongozi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

SIMBA RUVUMA WACHANGIA DAMU UNITI 20 HOMSOWanachama wa tawi la Simba Sports Club Mkoa wa Ruvuma wamechangia damu uniti 2...
01/08/2026

SIMBA RUVUMA WACHANGIA DAMU UNITI 20 HOMSO

Wanachama wa tawi la Simba Sports Club Mkoa wa Ruvuma wamechangia damu uniti 20 na zawadi za matendo ya huruma kwa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea leo 1 Augasti, 2026 . Zoezi hilo lililolenga kusaidia wagonjwa wenye uhitaji wa damu hospitalini hapo.

Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mfawidhi, Muuguzi Mfawidhi Berkumans Migunda ametoa shukrani za dhati kwa wanachama hao kwa ukarimu wao.

“Tunawashukuru sana Simba Sports Club Ruvuma kwa moyo wa huruma na upendo. Damu hii itaokoa maisha ya watu wengi wa Mkoa wa Ruvuvuma na wagonjwa wengine. Tunaomba ushirikiano huu uendelee ili tuweze kuhudumia wananchi wetu vizuri zaidi,” alisema.

Kwa upande wake Katibu wa Simba Sports Club Mkoa wa Ruvuma Roger Said amesema uamuzi wa kutoa damu umelenga kuwasaidia wananchi wanaopata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea na kuongeza akiba ya damu kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura.

WATUMISHI WA HOMSO WAKUMBUSHWA MAADILI NA SHERIA ZA UTUMISHIWatumishi  wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea wamefanya ki...
31/07/2026

WATUMISHI WA HOMSO WAKUMBUSHWA MAADILI NA SHERIA ZA UTUMISHI

Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea wamefanya kikao kazi cha kukumbushana kanuni, sheria na maadili ya utumishi wa umma. Mganga Mfawidhi Dkt. Magafu Majura amesisitiza kuwa kila mtumishi anatakiwa kufuata miongozo ya kazi kwa uadilifu, nidhamu na ubunifu ili kutoa huduma bora kwa wananchi. “Tuwe mfano wa nidhamu na uzalendo kazini.

Hata hivyo kikao hicho kimetoa taarifa mbalimbali juu ya uendeshaji wa hospitali ikiwemo maboresho ya huduma, matumizi sahihi ya rasilimali na mipango ya kuimarisha miundombinu.”Ushirikiano na uwajibikaji ndio utakaotufikisha mbali katika kutoa huduma bora na endelevu.

ZAWADI ZA MATENDO YA HURUMA: POLISI RUVUMA WAJENGA DARAJA NA WANANCHI HOMSOWakati wengi huliona Jeshi la Polisi likiteke...
31/07/2026

ZAWADI ZA MATENDO YA HURUMA: POLISI RUVUMA WAJENGA DARAJA NA WANANCHI HOMSO

Wakati wengi huliona Jeshi la Polisi likitekeleza majukumu ya ulinzi na usalama, Julai 30, 2026 limeandika sura nyingine ya huduma kwa jamii baada ya kuwafariji wazazi waliojifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Songea (HOMSO) kwa kuwapatia mahitaji muhimu kwao na watoto wachanga.

Msaada huo ulitolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani, kwa kushirikiana na Kitengo cha Polisi Jamii, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya polisi na wananchi kupitia matendo ya huruma.

Bidhaa zilizokabidhiwa zilijumuisha mahitaji muhimu ya akina mama na watoto wachanga, yakilenga kupunguza changamoto zinazowakabili familia katika siku za mwanzo baada ya kujifungua.

Hatua hiyo inaendeleza falsafa ya polisi kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kijamii zinazogusa maisha ya wananchi, sambamba na jukumu lao la msingi la kulinda amani na usalama.

Address

P. O. BOX 5
Songea

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Songea posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share