DR. TONNY

DR. TONNY Eternal health care:Ni wataalamu wa Tiba lishe

"UGONJWA WA MASUNDOSUNDO / VIGWARU (GE***AL WARTS) .-0622499570 Dr Tonny  "GE***AL WARTS - ( MASUNDO SUNDO )  NI NINI?Ni...
01/08/2025

"UGONJWA WA MASUNDOSUNDO / VIGWARU (GE***AL WARTS) .

-0622499570 Dr Tonny
"GE***AL WARTS - ( MASUNDO SUNDO ) NI NINI?

Ni vinyama Laini vidogovidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando Laini unaozunguka maeneo ya sehemu za siri, vinyama hivyo vinaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo (urethra), maeneo yanayozunguka haja kubwa na sehemu mbalimbali za mwili.

~Ugonjwa huu unaenezwa kwa njia ya kujamiiana (S*XUAL TRANSMITTED INFECTION) STI)

"CHANZO CHA TATIZO HILI"

~Ugonjwa wa Masundosundo husababishwa na virus waitwao HUMAN PAPILLOMA VIRUS ( HPV) hata hivyo Kuna Aina tofauti za virus wa HPV hivyo sio wote wanaosababisha tatizo hili kwani Kuna ambao wanaosababisha Masundosundo katika sehemu tofauti k**a vile mkono, mgongoni, mguuni nk.

Pia HPV huweza kasababisha saratani ya shingo ya kizazi (CARCINOMA OF THE CERVIX) kwa wanawake, na pia huweza kusababisha saratani ya sehemu ya haja kubwa (A**L CANCER) kwa jinsia zote mbili.

~Ugonjwa huu wa Masundosundo umejitokeza kwa kiasi kikubwa baada ya kuwepo kwa janga la UKIMWI hivyo watu wenye wapenzi wengi, wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo na haja kubwa, wajawazito, watumiaji wakubwa wa sigara na pombe, watu wenye upungufu wa kinga mwilini wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huu

DALILI ZA MASUNDOSUNDO"

"~mgonjwa wa tatizo hili hutokewa na vinyama Laini vidogovidogo vinavyoota kwenye katika maeneo tofauti (MFANO HALISI TIZAMA KATIKA PICHA) ingawa wakati mwingine huwa ni vidogo kiasi cha kutoweza kuonekana kwa njia ya kawaida.

~mgonjwa kupata ganzi maeneo yaliyozungukwa na Masundosundo
~kutokwa na uchafu mzito sehem za siri na kuwashwa kupita maelezo
~kutokwa damu ukeni mara baada ya kufanya tendo la ndoa.

NOTED :mwanaume huwa anachelewa kupata dalili na huwa na uwezekano mkubwa wa kuambikiza wenza wao

"MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA UGONJWA HUU"

~matibabu ya tatizo hili hupatikana kirahisi iwapo tatizo halijachelewa kupatiwa tiba, matibabu hutolewa kwa kufuata utaratibu wa Majibu yaliyopatikana katika vipimo mbalimbali, matibabu hayo huweza kuwa ya kuviondoa vinyama kwa kufanya operations au kutumia dawa, hata hivyo njia ya operation sio nzuri sana kwasababu huweza kutengeneza madhara zaidi na uwezekano mkubwa wa kupata kansa hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa ambazo zitatibu na kuondoa tatizo hilo na mgonjwa kupona kabisa ila cha kuzingatia ni kwamba ugonjwa huu ni wa kuambikiza hivyo inashauriwa wenza wote kupata matibabu hata k**a atajihisi hana dalili yoyote ni vyema akafanya vipimo ili kujihadhari kabla ugonjwa haujaleta madhara zaidi.

~Waswahili wanasema bora kinga kuliko matibabu hivyo ni vyema ukajiepusha na ugonjwa huu kwa kuepuka yafuatayo:

-EPUKA KUWA NA WAPENZI WENGI
-EPUKA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
-ACHA ORAL S*X UKISHINDWA BASI KUWA NA MPENZI MMOJA TU AMBAYE NDIO UNAWEZA KUMNYONYA SEHEMU ZAKE ZA SIRI.

ZINGATIA MAPENZI UJUZI LAKINI AFYA YAKO NI MALI ZAIDI WADADA/WAKAKA WENGI MMEKUA MKITAKA KUWARIDHISHA KILA MNAOKUTANA NAO KIMWILI KWA KUWANYONYA SEHEMU ZA SIRI KITU AMBACHO KINAKUWEKA KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU NA KANSA YA KOO.
-EPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA, SIGARA NA POMBE KUPITA KIASI

NOTED : NDUGU RAFIKI ugonjwa huu una madhara makubwa unaweza kusababisha kansa ya kizazi, kansa ya uume, kansa sehemu ya haja kubwa Nk hivyo hakikisha unapata matibabu ya uhakika iwapo una tatizo hili au ikiwa hauna jitahid kujiepusha na vihatarishi vya ugonjwa huu.

KWA MSAADA ZAIDI
WASILIANA NASI KUPITIA SIMU NAMBA 0622499570 DR TONNY

Huduma Ya Vipimo Vya Mwili MzimaJe,Unajiuliza Wapi,Utapata Huduma Ya Upimaji Wa Mwili Mzima kwa haraka Na gharama Rahisi...
31/07/2025

Huduma Ya Vipimo Vya Mwili Mzima

Je,Unajiuliza Wapi,Utapata Huduma Ya Upimaji Wa Mwili Mzima kwa haraka Na gharama Rahisi Zaidi
Kumbuka Afya Yako Ndio Msingi Wa Mambo Yote....

Tumekuandalia OFA Maalumu Ya Upimaji Wa Mwili Mzima Kuelekea mwisho wa mwezi

utalipia TSH 30,000/= tu k**a nawe Utakuwa Miongoni Mwa Watu 20 Wa Mwanzo

Gharama Halisi za Vipimo ni 150,000/= Lakini k**a Utakuwa Miongoni Mwa Watu Hawa Ishirini Utalipia 30,000/= tu na utaokoa Zaidi Ya Tsh 120,000/= Nzima

Natumaini k**a ni Miongoni Mwa Watu wanaopenda Afya Zao Basi Huwezi Kukosa OFA hii

KIPIMO KINAONYESHA;

1.Tatizo husika
2.Chanzo Cha tatizo
3.Viashiria Vya tatizo lingine
Kipimo kinahusika zaidi na magonjwa sugu ambayo hayaambukizi

Tunafanya Vipimo vya Mwili mzima Katika Mifumo ifuatavyo;

1.Mfumo wa Ubongo
2.Mfumo wa Upumuaji
3.Mfumo wa Tumbo
4.Mfumo wa Ngozi
5.Mfumo wa Mifupa na Misuli
6.Mfumo wa Uzazi Kwa wanawake na wanaume
7.Mfumo wa Macho

Pia Tunatoa huduma ya MATIBABU Kwa Magonjwa sugu k**a Ifuatavyo
_Vidonda Vya Tumbo, Presha, Kisukari,
Moyo, Figo, INI, Cholesterol, Bawasili,
_Tezi dume, fangasi , Uzazi Kwa wanawake na wanaume, Figo, Macho, Allergy, Mifupa, Ngozi
Tunatibu Uvimbe Aina zote bila upasuaje, stroke (Kupooza),Miguu, Magoti, Ganzi,Uzito mkubwa na UneneUvimbe kwenye vyia vya Uzazi, Ukuaji mbovu Kwa watoto n.k

Ili OFA Hii Isikupite basi fanya hivi Piga Simu/Tuma Sms au WhatsApp inbox kwenda namba
0622499570

Tunapatikana Tanzania nzima yaani Tanzania bara na visiwani gusa link apo👇https://chat.whatsapp.com/EhX4JPO3Q2T1BKKuMqc6bl

AINA ZA UCHAFU UNAOTOKA UKENI,RANGI NA DALILI ZAKE,Kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na kuwashwa au kutokewa na vipel...
24/07/2025

AINA ZA UCHAFU UNAOTOKA UKENI,RANGI NA DALILI ZAKE,

Kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na kuwashwa au kutokewa na vipele, hii huashiria kwamba kuna tatizo ukeni, na katika makala hii tumechambua aina mbali mbali za uchafu ukeni kwa kuangalia rangi zake na dalili za magonjwa.

1. UCHAFU WENYE RANGI YA KAHAWIA AU DAMU

Huu uchafu huonyesha dalili ya kuwa mzunguko wako wa hedhi umevurugika na wakati mwingine ni dalili ya magonjwa k**a kansa ya kizazi,
mwanamke anayepata tatizo hili hutoa damu nyingi pamoja na kuumwa sana nyonga, hivo ukiona dalili k**a hizi nenda kafanye vipimo hospital na kuanza tiba mapema

2. UCHAFU WENYE RANGI YA NJANO /KIJANI WENYE HARUFU MBAYA

Endapo uchafu huo utatoka k**a povu na wenye rangi ya kijani au njano na ukiambatana na harufu mbaya huwa ni dalili ya ugonjwa wa trichomonas,PID(pelvic inflammatory disease), maambukizi ya parasite yanatokana na ngono zembe,
dalili Yake nyingine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo,maumivu wakati wa tendo la ndoa,kutokwa na damu ukeni wakati wa tendo la ndoa n.k.

3. UCHAFU MWEUPE MZITO K**A JIBINI

Mara nyingi hii huwa ni dalili ya maambukizi ya fangasi(YEAST INFECTION) na dalili nyingine huwa ni kuvimba sehemu ya nje ya siri, kuwashwa na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.
Ngozi ya eneo la nje kubadilika rangi na kuwa nyekundu,kuhisi hali ya kuungua wakati wa kutembea,
uchafu mzito kutoka ukeni na wa rangi mithili ya maziwa mgando,uchafu huu huweza kuambatana na harufu mbaya kutoka ukeni

4. UCHAFU MWEUPE/KIJIVU WENYE HARUFU YA SAMAKI

Uchafu wa Aina hii ni dalili ya maambukizi ya bacteria vaginosis, mara nyingi mwenye tatizo hili husikia muwasho na maumivu sehem ya nje ya uke.
KUMBUKA: Jua kutofautisha kati ya ute ute ambao ni kawaida kumtoka mwanamke akiwa kwenye siku za hatari na aina za uchafu unaotoka ukeni ambao nimetoa maelezo yake.
Ute ute wa siku za hatari unakuwa wa kuvutika k**a vile ule wa kwenye yai la kuku,na hauna harufu yoyote mbaya.
NAMBA ZETU NI 0622499570 Dr Tonny

ZIJUE SABABU 7 ZINAZOPELEKEA MWANAUME KUSHINDWA KUTUNGISHA MIMBAZijue Sababu 7 Zinazopelekea Mwanaume Kushindwa Kutungis...
24/07/2025

ZIJUE SABABU 7 ZINAZOPELEKEA MWANAUME KUSHINDWA KUTUNGISHA MIMBA

Zijue Sababu 7 Zinazopelekea Mwanaume Kushindwa Kutungisha Mimba.

Zijue Sababu 7 Zinazopelekea Mwanaume Kushindwa Kutungisha Mimba.

K**a ilivyo kawaida kwenye jamii zetu watu wengi wamekuwa wakidhani kuwa mwanamke pekee ndiye mwenye wajibu wa kuhakikisha anapata mimba na ikitokea akakaa muda mrefu kwenye ndoa bila hilo kutokea, basi jamii inamtupia lawama wakiamini tatizo ni lake na siyo mumewe. Lakini kiukweli tatizo linaweza kuwa kwa mwanaume au mwanamke au wote wawili (mwanamke na mwanaume).

Tatizo la mwanaume kushindwa kutungisha mimba hujulikana k**a ugumba. Tatizo hili pia hujlikana kwa kitalaamu k**a infertility. Ugumba kwa wanaume hutokana na tatizo katika mbegu za kiume, manii kuwa kidogo, manii kushindwa kutembea, manii kuwa na umbo lisilo la kawaida au kuziba kwa mirija ya mbegu za kiume.

Fahamu Kiwango Sahihi Cha Mbegu Za Kiume Kutungisha Mimba.

Leo katika makala yetu tuta zungumzia sababu zinazochangia mwanaume kushindwa kutungisha mimba.

Sababu Za Mwanaume Kushindwa Kutungisha Mimba:

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazoweza kuchangia mwanaume kushindwa kutungisha mimba ambazo ni pamoja na;

1) Uvutaji Wa Sigara Na Matumizi Ya Pombe Kupita Kiasi.

Baadhi ya mitindo ya kimaisha (lifestyle) kwa wanaume k**a vile uvutaji wa sigara, bangi, matumizi ya madawa ya kulevya, matumizi ya pombe kupita kiasi yanaweza kuchangia ugumba kwa mwanaume kwani husababisha hitilafu katika uzalishwaji wa mbegu za kiume. Lakini pia kukaa masaa mengi au kila mara sehemu zenye joto sana hasa joto la kutengenezwa (saunas and hot tubs) kunaweza kuchangia ugumba kwa mwanaume na hivyo kushindwa kutungisha mimba.

2) Mazingira.

Baadhi ya mazingira anayoishi mwanaume yanaweza kumpelekea kupoteza uwezo wa kutungisha mimba. Japokuwa ni kwa asilimia chache lakini k**a mwanaume anajihusisha na umwagiliaji wa dawa za kuulia wadudu mashambani zijulikanazo kwa kitaalamu k**a Dichlorodiphenyltrichloroethane (DDT) kwa kipindi kirefu kunaweza kuchangia mwanaume kupoteza uwezo wa kutungisha mimba.

Lakini pia k**a mwanaume anafanya kazi kwenye ofisi au kiwanda ambako mionzi (radiations) ni vitu anavyotakiwa akutane navyo kila siku basi hali hii inaweza kumuandalia ugumba polepole na hatimaye akaishiwa kabisa uwezo wa kutungisha mimba.

3) Madhara Ya Saratani Ya Matibabu Yake.

Madhara yatokanayo na ugonjwa wa saratani pamoja na matibabu yake hasa matibabu yanayohusisha mionzi (radiotherapy or chemotherapy) vinaweza kuwa ndiyo sababu ya ugumba kwa mwanaume. Matibabu hayo ya saratani yanaweza kuharibu uzalishaji wa mbegu za kiume zenye afya na hivyo kumpelekea mwanaume kupoteza uwezo wa kutungisha mimba.

4) Magonjwa Ya Zinaa (Sexually Transmitted Infections).

Magonjwa ya zinaa k**a vile kaswende, kisonono, pangusa yanaweza kupelekea mwanaume kupoteza uwezo wa kutungisha kwani magonjwa haya huchangia kuziba kwa mirija ya mbegu za kiume.

5) Magonjwa Ya Muda Mrefu (Chronic Diseases).

Magonjwa ya muda mrefu k**a vile kisukari, shinikizo la juu la damu yanaweza kupelekea uzalishwaji wa mbegu za kiume za kiume usio wa kawaida. Pia hata uwepo wa uvimbe kwenye korodani kunaweza kuathiri uzalishwaji wa mbegu za kiume na hatimaye kumpelekea mwanaume kupoteza uwezo wa kutungisha mimba

6) Matatizo Katika Kusafiri Kwa Mbegu Za Kiume.

Kuna nyakati wanaume anaweza kuwa anatoa mbegu za kiume lakini mbegu hizo zikawa aidha hazifiki sehemu husika kwenye viungo vya uzazi wa mwanamke au zinafika sehemu hizo kwa kuchelewa na hivyo kupelekea mbegu za kiume nyingi kufia njiani.

Tatizo hili la mbegu za kiume kutokufika haraka sehemu husika kwenye viungo vya uzazi wa mwanamke linaweza kusababishwa na tatizo la mwanaume kuwahi kufika kileleni anaposhiriki tendo la ndoa (yaani ndani ya sekunde, dakika 1 au 2 tayari ameshafika kileleni). Mwanaume mwenye changamoto ya kuwahi kufika kileleni anaweza kushindwa kutungisha mimba.

Tatizo la mwanaume kuwahi kufika kileleni linaweza kusabishwa na upigaji wa kunyeto kupita kiasi, kuangalia video za ngono kupita kiasi, kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa n.k.

7) Mvurugiko Wa Homoni.

K**a ilivyo kwa mwanamke, mwanaume pia anaweza kupata tatizo la mvurugiko wa homoni ya uzazi ijulikanayo k**a testosterone na hivyo kushindwa kuungisha mimba. Dalili za mvuugiko wa homoni kwa mwanaume ni pamoja na; mwanaume kuota mat**i (gynecomastia), mwanaume kushindwa kusimamisha uume (erectile dysfunction), kuwa na hasira kupita kiasi bila sababu, msongo wa mawazo.

Kumbuka:

Mwanaume kushindwa kumpa mimba mwanamke pia kunaweza kukasababishwa na matatizo ya kuzaliwa nayo k**a vile korodani kushindwa kushuka kwenda kwenye mapumbu (sc***um) kabla ya kuzaliwa, hali ijulikanayo kwa kitaalamu k**a Undescended te**es (cryptorchidism).

Tatizo lingine linaloweza kusabisha mwanaume kushindwa kutungisha mimba ni la kimaumbile ambapo kwenye mrija wa kutolea mbegu, pamoja na mkojo uitwao urethra huota sehemu ya chini ya uume, hivyo kusababisha mbegu kutoweza kufika sehemu ya ndani ya uke, tatizo hili kitaalamu huitwa Hypospadias.

Tiba Ya Mwanaume Kushindwa Kutungisha Mimba:

Tatizo la mwanaume kushindwa kutungisha mimba linaweza kutibika au kushindikana kutibika kutokana na sababu iliyopelekea tatizo hilo. Tiba inaweza kuwa kubadilisha mfumo wa kuishi kutokana na maelekezo ya daktari, dawa za kutumia na lishe au upasuaji (kutegemeana na upatikanaji wa vifaa tiba na wataalamu).

HITIMISHO:

Kwa msaada wa ushauri, na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi kwa wanaume na wanawake wasiliana nasi kwa simu namba
PIGA/SMS
WHATSAPP
🇹🇿0622499570 Dr Tonny

*FAHAMU TATIZO LA MAPAFU KUJAA MAJI* ✍🏻Mapafu Kujaa Maji; Ni pale ambapo kunakuwa na mkusanyiko wa maji kati ya kuta mbi...
24/07/2025

*FAHAMU TATIZO LA MAPAFU KUJAA MAJI*
✍🏻Mapafu Kujaa Maji; Ni pale ambapo kunakuwa na mkusanyiko wa maji kati ya kuta mbili zinazozunguka mapafu. Kujaa huku kwa maji husababisha mgonjwa kupata shida ya kupumua vizuri.
✍🏻Sababu za mapafu kujaa maji zinaweza kuelezewa kutokana na aina ya maji yaliyojaa:
👉🏻Kwa mfano kuna kitu kinatajwa kuwa ni Transudate; hapa maji hutoka kutoka kwenye mishipa ya damu na kuingia kwenye mapafu hasa kwa watu ambao wana magonjwa yafuatayo:
✅Moyo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi (congestive cardiac failure),
✅ini kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi (liver failure) na,
✅figo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi (renal failure)
👉🏻Exudate; hapa maji hujaa kutokana na kuta zinazozunguka mapafu kuwa na maji kitaalamu (pleura) husababisha mapafu kuvimba.
✍🏻Mtu anaweza mapafu yake kujaa kutokana na magonjwa ya mapafu mfano:
✅Kansa ya mapafu au ya t**i,
✅ugonjwa unaoitwa Lymphoma,
✅Kifua kikuu (TB),
✅vichomi,
✅figo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi au
✅kuwa na majipu ndani ya tumbo.
DALILI YA UGONJWA
✍🏻Mtu ambaye amepatwa na tatizo la mapafu kujaa maji huwa na dalili za;
👉🏻kusindwa kuhema vizuri,
👉🏻kusikia maumivu ya kifua
👉🏻hukumbwa na Kifua Kikuu
👉🏻jasho jingi kutoka kipindi cha usiku,
👉🏻Kukohoa damu, na
👉🏻Kupungua uzito kwa kasi ya kutisha.
👉🏻Kuwa na vichomi,
👉🏻Kupatwa na homa,
👉🏻Kukohoa makohozi yenye rangirangi, inaweza kuwa damudamu au manjano.
MATIBABU
✍🏻Kwa sababu ya kusababisha matatizo ya kupumua huduma zetu huangalia kwanza kudhibiti yafuatayo;
👉🏻kuokoa,
Kuangalia mfumo wa hewa na kadhalika.
👉🏻Kutibu magonjwa yanayosababisha maji kwenye mapafu.
✍🏻Kila mtu aonapo dalili nilizozitaja anatakiwa kufanya vipimo ili kujua chanzo cha tatizo na kuanza matibabu mapema

Calls/whatsapp 0622499570 Dr Tonny

ZIJUE SABABU ZINAZOMFANYA MWANAUME KUTOKUWA NA HISIA AU HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA.Je, Nini Kinasababisha Kuwa Na His...
24/07/2025

ZIJUE SABABU ZINAZOMFANYA MWANAUME KUTOKUWA NA HISIA AU HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA.

Je, Nini Kinasababisha Kuwa Na Hisia Za Chini Sana Za Mapenzi?

Hisia za chini za mapenzi humaanisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Hii ni hali ya kupoteza kabisa hamu ya kushiriki tendo la ndoa kila inapofikia muda wa kufanya tendo la ndoa na mke au mpenzi wako, na viwango vya kupungua kwa hisia za mapenzi hutofautiana katika maisha yako yote.

NUKUU: Hata hivyo, kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa kipindi kirefu kunaweza kusababisha mtafaruku kwa wanandoa ndani ya nyumba. Inaweza kuwa ishara ya matatizo ya kiafya.

Hapa nitapenda kuelezea visababishi vichache vya kukosa hisia za mapenzi au hamu ya kufanya tendo la ndoa.

1. Kupungua Kwa Homoni Ya Testosterone

Homoni ya testosterone ni ya muhimu sana kwa mwanaume, nayo hutengenezwa kwenye korodani. Homoni hii inahusika na kujenga misuli pamoja na mifupa, na katika kuamsha uzarishaji wa mbegu za mwanaume au manii. Viwango vya homoni ya testosterone pia humfanya mwanaume kuwa na hisia au hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Viwango vya kawaida vya homoni ya testosterone vinatofautiana. Hata hivyo, wanaume wenye umri mkubwa wanatakiwa kuwa na kiwango kidogo cha homoni ya testosterone. Pale viwango vya homoni ya testosterone vinapopungua, hamu ya kufanya tendo la ndoa pia hupungua.

Kupungua kwa homoni ya testosterone ni sehemu ya kawaida katika umri wa mtu. Hata hivyo, kushuka kwa homoni ya testosterone kunaweza kupelekea kupungua kwa hisia za tendo la ndoa.

Fika ofisini kwetu Dar masaki ikiwa k**a una sumbuliwa na tatizo hili. Utapata Tiba ili kuongeza viwango vyako vya homoni ya testosterone.

2. Matumizi Ya Madawa Bila Ushauri Wa Daktari

Utumiaji wa madawa fulani ya vidonge kunaweza kupunguza viwango vya homoni ya testosterone ambayo kwa upande mwingine, inaweza kupelekea kupungua kwa hisia au hamu ya tendo la ndoa.

Kwa mfano, madawa ya magonjwa ya moyo k**a vile shinikizo la damu(blood pressure) yanaweza kuzuia mwanaume ashindwe kudindisha au kukojoa au kufika kileleni.

Utumiaji sigara, pombe, ma*****na, madawa ya kulevya k**a vile opiates yanaonyesha pia kuwa chanzo cha kusababisha kupungua kwa uwezo wa kuzarisha homoni za testosterone. Hali hii inaweza kupelekea mwanaume kutokuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa. Sumu zitokanazo na uvutaji sigara huharibu uwezo wa uzarishaji wa mbegu au manii na hivyo mwendo wake kuwa tofauti kabisa na manii zenye afya.

NUKUU: K**a ukiwa na athari za kushuka kwa homoni ya testosterone kutokana na matumizi ya vidonge, basi fika hospitali haraka ukaweze kupata vipimo na ushauri.
3. Huzuni Au Mawazo

Huzuni hubadiri sehemu zote za maisha ya mtu. Watu wenye huzuni hukosa hamu ya kufanya mambo yao ikiwemo tendo la ndoa. Kukosa hamu au hisia ya mapenzi pia ni athari ya madawa yatumikayo kwa ajili kuondoa hali hiyo nayo ni,

• Serotonin-Norepinephrine Reuptake Inhibitors, k**a vile duloxetine(Cymbalta)

• Serotonin-Norepinephrine Reuptake Inhibitors, k**a vile Fluoxetine(Prozac) na Sertraline(Zoloft)

4. Magonjwa Ya Muda Mrefu

Unapojisikia vibaya kutokna na athari za ugonjwa wa muda mrefu, k**a vile maumivu makali ya muda mrefu, hamu ya kufanya tendo la ndoa hutoweka katika akili yako. Magonjwa fulani k**a vile, salatani, yanaweza kupunguza pia uzarishaji wa viwango vya mbegu au manii. Magonjwa sugu mengine ambayo yanaweza kusababisha ukakosa hamu ya tendo la ndoa ni pamoja na haya;

• Kisukari aina ya 2

• Uzito au kitambi

• Shinikizo la juu la damu

• Mafuta mengi mwilini

• Mapafu, moyo, figo na ini kushindwa kufanya kazi
NUKUU: K**a unasumbuliwa na magonjwa sugu, basi nakushauri ufike hospitali muda ili uweze kupata ushauri. Unaweza pia kumuona mshauri wa ndoa k**a vile au daktari wa magonjwa ya uzazi.

5. Umri Kuwa Mkubwa

Viwango vya homoni ya testosterone, ambavyo huambatana na kukosa hamu au hisia ya tendo la ndoa, huwa viko juu sana pale mwanaume anapokuwa bado katika hali yake ya ujana. Katika miaka ya uzee, mwanaume anaweza kuwa anachukua muda mrefu kufika kileleni pale anaposhiriki tendo la ndoa na mwenza wake, na hivyo hata hisia zenyewe au nyege, nazo huchelewa kuzipata. Umme wake unaweza ukasimama lakini usiwe mgumu sana, na huchukua mud asana kuja kusimamisha uume wake.

NUKUU: Hata hivyo tunazo dawa ambazo zina uwezo mkubwa wa kuondoa tatizo hili.
6. Msongo Wa Mawazo

Ikiwa umetatizwa na hali au vipindi vyenye kutatanisha, basi hamu ya tendo la ndoa hupungua. Hii ni kwasababu msongo wa mawazo unaweza kuvuruga viwango vyako vya homoni. Mishipa yako ya ateri inaweza kusinyaa wakati wa msongo wa mawazo. Kusinyaa huku kwa mishipa huzuia damu kuweza kutiririka na hivyo kusababisha uume kushindwa kusimama.

NUKUU: Hivyo basi, msongo wa mawazo unaathiri pande zote mbili; kwa mwanaume na mwanamke pia na kusababisha matatizo katika mambo ya ndoa. Msongo wa mawazo ni vigumu sana kuepukana nao. Matatizo ya mahusiano, kupeana talaka, kufiwa na mwenza uliyekuwa ukimpenda sana, matatizo ya kiuchumi k**a vile kufirisiwa au mikopo, kufiwa na mtoto, ni baadhi ya matukio ya maisha ambayo yanaweza kuathiri hisia au hamu ya tendo la ndoa.

7. Kufanya Mazoezi Kupita Kiwango Au Kutokufanya Mazoezi Kabisa

Kutokufanya mazoezi au kufanya mazoezi kwa kupita kiwango kunaweza pia kumfanya mwanaume kukosa hisia au hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kutokufanya mazoezi kabisa kunaweza kumfanya mwanaume kuwa na matatizo ya kifya ambayo yanaweza kuathiri hisia za mapenzi na kukosa nyege kabisa.

NUKUU: Kufanya mazoezi kila mara kunaweza kupunguza hatari ya magonjwa sugu k**a vile uzito kuwa mkubwa, shinikizo la damu, kisukari, ambayo yote huambatana na kupungukiwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa.
8. Athari Za Kupungua Kwa Hisia Za Mapenzi Katika Mwili

Kupungua kwa hamu au hisia ya mapenzi kwa mwanaume kunaweza kumfanya asitulie. Kukosa hisia ya mapenzi kunaweza kupelekea mwanaume kuwa na athari kubwa katika mwili wake, hasa kupungukiwa nguvu za kiume, kushindwa kusimamisha uume kwa muda mrefu na hivyo kushindwa kumridhisha mwanamke. Kupungua kwa nguvu za kiume kunaweza kumsababisha mwanaume kuwa na wasiwasi wakati wa kufanya tendo la ndoa.
NUKUU: Hali hii inaweza kupelekea ugomvi kati yake na mke au mwenza wake, hali ambayo inaweza kusababisha kuwa na michepuko nje ya ndoa au kuwa na wapenzi wengi. Kushindwa kufika kileleni kutokana na kukosa nguvu za kiume kunaweza kusababisha kuhisi huzuni, kutokujiamini, na mwili kuharibika.

Mtazamo Unaotakiwa Kuufuata

Kutibu tatizo la kukosa hisia za mapenzi mara nyingi hutegemeana na visababishi vyake. K**a hali ya kukosa hisia inasababishwa na matatizo ya kiafya, utahitahi utumie tiba. Laikini k**a tatizo hilo limesababishwa na mambo ya kisaikolojia, basi utahiji kumtembelea mshauri wa mambo ya ndoa.
Unaweza pia kuchukua hatua ya kuongeza uwezo wa hisia za mapenzi wewe mwenyewe. Mambo yafuatayo yana uwezo mkubwa wa kuongeza hisia za mapenzi;
• Kuishi mtindo mzuri wa maisha
• Kupata muda mwingi wa kusinzia
• Kula vyakula vyenye virutubishi vingi
• Kutembelea maeneo mazuri k**a vile kutali, nk.

SURUHISHO NA TUMAINI LIPO.

Karibuni sana🙏🙏🙏

NITUMIE UJUMBE WHAT'SAAP 🟢

🔜 0622499570 Dr Tonny

SABABU ZA TATIZO LA MBEGU CHACHE ZA KIUME(LOW S***M COUNT)*✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿⚫Watu wengi hudhani k**a mwanamke hapati ujau...
24/07/2025

SABABU ZA TATIZO LA MBEGU CHACHE ZA KIUME(LOW S***M COUNT)*
✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿
⚫Watu wengi hudhani k**a mwanamke hapati ujauzito basi tatizo na lawama zote zitakuwa ni upande wa *mwanamke,* lakini hilo si lazima mara zote liwe hivyo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa tatizo la kutopata mtoto katika familia likawa linatokana na ugumba upande wa *mwanaume.*

⚫Mwanaume kuzalisha mbegu chache kuliko kawaida ni mojawapo ya sababu kubwa za ugumba kwa wanaume.

*MBEGU CHACHE NI KIASI GANI?*

⚫Shahawa kawaida ni mchanganyiko wa maji maji *(ute)* unaotengenezwa na tezi dume na mbegu za kiume *(manii).* Mtu anakua na tatizo la mbegu chache pale katika kila Millilita moja ya shahawa zake kunakua na mbegu *(manii)* chini ya *millioni 15.* Kwa kawaida mwanaume anazalisha zaidi ya manii *millioni 20* katika kila millilita moja ya shahawa anazomwaga.

⚫Kitaalamu tatizo hili linaitwa *OLIGOS***MIA (ol-ih-go-spur-me-uh),* na kutokuwa na mbegu za kiume kabisa kwenye shahawa inajulikana k**a *AZOOS***MIA*

*DALILI*
⚫Dalili kuu ya tatizo hili ni kushindwa kutungisha mimba/kupata mtoto.

Zinaweza kuwepo dalili nyingine kulingana na chanzo cha tatizo hili mfano
⏩mirija ya manii kuziba,
⏩matatizo kwenye korodani na matatizo kwenye mfumo wa hormone.
⏩Dalili nyingine ni k**a
Matatizo kwenye uwezo wa kufanya tendo la ndoa *mfano* kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa,
⏩uume kushindwa kusima au kuwa mlegevu unaposimama.
⏩Maumivu na uvimbe kwenye korodani
⏩Kupungua au kutokuwa na ndevu na nywele za sehemu nyingine za mwili ,hii ni dalili ya uhaba au upungufu wa hormone ya *testosterone.*

*VISABABISHI VYA TATIZO HILI*
⚫Kutengenezwa kwa mbegu inahusisha *korodani* na tezi iliyopo kwenye ubongo inayojulikana k**a *hypothalmus* ambayo hii inahusika na kuzalisha hormone zinazochochea uzalishwaji wa mbegu za kiume. Matatizo katika viungo hivi huweza kupelekea tatizo hili.

⚫ Pia kuna weza kuwepo na matatizo katika maumbo ya mbegu za kiume nayo kupelekea tatizo hili.

*Visabibishi vya tatizo hili ni k**a ifatavyo:*
✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿
*SABABU ZA KIAFYA*

⏩1. *Kuvimba kwa mishipa ya damu ya korodani- Varicocele* ,hali hii inaathiri kiwango cha joto kwenye korodani hivyo kuathiri utengenezwaji wa mbegu za kiume.

⏩2. *Maambukizi,* Baadhi ya maambukizi yanaweza kuathiri utengenezwaji wa mbegu za kiume na jinsi mbegu hizi zinavyotelewa nje.Magonjwa ya zinaa,magonjwa ya korordani yanaweza kupelekea kuziba kwa mirija ya manii na kuharibu seli zinazohusika na kutengeneza manii kwenye korodani.

⏩3. *Matatizo katika* kutoa mbegu nje mfano tatizo la misuli ya shingo ya kibofu kutobana vizuri hivyo kupelekea shahawa kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kutolewa nje.

⏩4. *Kinga ya mwili* kuziharibu mbegu.Kuna tatizo la kinga ya mwili kuzisoma mbegu za kiume k**a wadudu wanaoleta magonjwa hivyo kuziharibu *(s***m ant bodies)*

⏩5. *Saratani,* kuna baadhi ya saratani k**a saratani ya tezi ya *pituitari,* saratani ya korodani zinaathiri pia utengenezwaji wa mbegu za kiume

*6.USAWA WA HOMONI USIO SAWA (Hormone Imbalance):*
⏩Tatizo la homoni kutokuwa sawa si jambo linalowapata wanawake peke yao, ni jambo linalojitokeza pia kwa wanaume ingawa wengi wao huwa hawana muda wa kufikiri kuwa nalo. Homoni zina umhimu mkubwa katika kazi ya uzalishaji wa mbegu na katika afya ya uzazi wa mwanaume kwa ujumla.

⏩Moja ya homoni kuu inayohusika na uzazi kwa mwanaume ni homoni ya *testosterone.* Kutokana na maisha yetu ya kisasa na baadhi ya matatizo yaliyoelezwa hapo juu upande wa uwingi wa mbegu, wanaume wengi wanajikuta katika hali hii ya kuwa na tatizo la homoni zao kutokuwa katika usawa unaohitajika kwa afya bora ya uzazi.
Vipo vitu vinavyoweza kuharibu homoni ya testerone na huanza kwa kuigiza au kijifanya vyenyewe ni estrogens *(xenohormones).*

⏩ *Estrogen* ikizidi katika mwili wa mwanaume hupelekea uhanithi *(uume kushindwa kusimama),* kukosa hamu ya tendo la ndoa, kupungua kwa mbegu na kupungua kwa maji maji ya mbegu kwa ujumla.

*Visababishi hasa vya kuharibika kwa testeroni ni pamoja na*
⏩• Vyakula vyenye soya
⏩• Madawa yanayotumika katika mazao mashambani
⏩• Homoni zinazoongezwa katika bidhaa za maziwa na nyama
⏩• Vifaa au vyombo vya plastiki aina ya HDPE.

*7.Mishipa ya manii kuziba*

*8.Madawa,* Baadhi ya madawa mfano dawa za kutibu saratani,dawa za fangasi,na baadhi ya ant biotic zikitumika kwa muda mrefu zinaweza kusababisha tatizo hili.

*9.Mfadhaiko (Stress)* – Mfadhaiko au stress inaweza kuleta majanga makubwa katika homoni na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.
Stress inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.

⚫Vile vile kuna presha kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwamba kwanini huzai. Hivi vyote ukiviweka kichwani na kuviwaza kila mara ni rahisi kwako kupatwa na tatizo la kupungua kwa mbegu na uzazi kwa ujumla.
Kuwa na amani, mwamini Mungu kwamba siku yako ipo, *just relax* kila kitu kina muda wake.
👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿
*KWA TIBA NA USHAURI WA BURE WASILIAN NAMI KUPITIA SIMU NAMBA 0622499570 Dr Tonny

"MADHARA YA HORMONAL IMBALANCE KWA MWANAMKE- •Kwa Kawaida Homoni hii Inapoongezeka kwenye damu (oestrogen) katika mwili ...
24/07/2025

"MADHARA YA HORMONAL IMBALANCE KWA MWANAMKE-

•Kwa Kawaida Homoni hii Inapoongezeka kwenye damu (oestrogen) katika mwili wa mwanamke husababisha changamoto nyingi ktk mwili hasa ktk Via vya uzazi wa mwanamke na mwishowe kupelekea UGUMBA iwapo hatapata tiba mapema na ya uhakika.

MADHARA HAYO NI

✓ uvimbe kwenye kizazi ( FIBROIDS)

✓Uvimbe kwenye mayai(OVARIAN CYSTS)

✓mvurugiko wa hedhi

✓uvimbe kwenye tezi ya shingo,

✓mimba kutoka/ kuharibika

✓ uvimbe kwenye ukuta wa mji wa mimba

✓Mirija ya uzazi kuziba

✓Ugumba

Hormone imbalance inaweza kujitokeza kwa dalili tofautitofauti katika mwili wa mwanamke. Mojawapo ni

©mvurugiko wa hedhi kwa mwanamke ambayo inaweza kujionesha katika makundi matatu ya watu:

♦Kupishana kwa tarehe za hedhi (period) anozoingia mwanamke kila mwezi

♦Mwanamke kuingia hedhi zaidi ya mara moja katika mwezi moja.

♦kutopata hedhi/ period zaidi ya mwezi mmoja ama zaidi

Ili kusaidika na matatizo haya ya hormon imbalance na HEDHI ,

Watsup/ call / sms

+ 255622499570 Dr Tonny

🍅🍓  MATATIZO  YANAYO MFANYA MWANAMKE  ASIBEBE  MIMBA  🤦‍♀️🤷‍♀️  KWA  HARAKA ( Infertility )   🍎🍇🍉☑️ Elimu iliyo wasaidia...
21/07/2025

🍅🍓 MATATIZO YANAYO MFANYA MWANAMKE ASIBEBE MIMBA 🤦‍♀️🤷‍♀️ KWA HARAKA ( Infertility ) 🍎🍇🍉

☑️ Elimu iliyo wasaidia Wengi.

🎯 Kwa kawaida mwanamke anatakiwa apate ujauzito ndani ya mwaka mmoja baada tu ya kuolewa au kuanza mahusiano na yule ambaye tayari ana mtoto.

🍎 Kitendo cha kukaa muda mrefu bila ya kupata mtoto Hua linahitaji uchunguzi na tiba.

🍅 CHANZO CHA MATATIZO

🍅 Mwanamke kutopata ujauzito husababishwa na matatizo mengi kwa upande wake au mumewe.

🎯 Kwa upande wa mwanaume, vyanzo vinaweza kuwa kukosa nguvu kabisa au kupungukiwa nguvu za kiume tatizo liitwalo, ‘Erectile Dysfunction,’

🎯 Mwanaume anaweza kutoa manii mepesi sana kiasi kwamba baada tu ya kumaliza tendo mwanamke akisimama zinamwagika au zinatoka.

🎯 Dalili nyingine ni pale manii zinapopimwa hospitali na kuonekana zipo chache sana au hazina nguvu.

🍅 Kwa upande wa mwanamke, vyanzo vinaweza kuwa matatizo katika mfumo wa homoni au vichocheo mbalimbali vya uzalishaji na upevushaji mayai na mzunguko..
🍅 Mwanamke mwenye tatizo hili hupoteza siku zake za hedhi, mzunguko wa hedhi huvurugika na asijue ratiba yake ya mzunguko.

🍓 Pia hupoteza hamu na raha ya tendo, maumivu wakati wa tendo, hapati ute wa uzazi.
🎯Matatizo mengine ni kuziba kwa mirija ya uzazi, uwepo wa uvimbe katika mfuko wa uzazi, kupata damu ya hedhi kwa muda mfupi sana yaani moja au mbili au zaidi ya siku saba.

🍅 Pia kuumwa tumbo chini ya kitovu mara kwa mara, kutokwa sana na uchafu ukeni ambao wakati mwingine huambatana na harufu mbaya na muwasho pamoja na maumivu wakati wa haja ndogo.

🍅 Matatizo ya kutokwa na uchafu ukeni na muwasho havihusiani na ugonjwa wa yutiai ‘UTI’ k**a wengi walivyozoea.

🍓 Matatizo mengine yanayomfanya mwanamke asipate ujauzito anapohitaji ni kutokufahamu siku za kupata mimba. Ili kufahamu siku za kupata mimba lazima ufahamu kwanza mzunguko wako uko vipi,

🍓♦️ Vile vile mwanamke ajue siku zake za ‘Ovulation’ au siku za ute wa uzazi. Ute wa uzazi upo wa aina tatu, kuna mwepesi, mwepesi wa kuvutika na mzito.

🌹Inawezekana Ukawa Una Changamoto yoyote Ya Uzazi au Ya Kiafya Kwa Ujumla,
📲 K**a Ndio Napenda Nikukaribishe Eternal International Clinic
💥Tunatoa Huduma hata kwa waliowahi kupima wakaja na cheti cha daktari
🩸 Dawa Zetu ni Tiba Lishe na
🩸 Tuna zaidi ya Vituo Mia moja Duniani kote,

💥 RATIBA YA KAZI NA ORODHA YA VITUO VYETU NCHINI TANZANIA 💥

🙏🙏

🌹KARIBUNI SANA

Tupigie au sms Kwa Namba

☎️🇹🇿0622499570

🩸Au Wasiliana na Doctor kwa Njia ya Whatsapp ♻️0622499570

Address

Zanzibar City

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when DR. TONNY posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share