31/05/2026
β€οΈ PRESHA YA JUU (SHINIKIZO LA DAMU): SIMBA MWENDA POLE β€οΈ
Watu wengi wanaishi na presha ya juu bila kujua kwa sababu mara nyingi haina dalili za wazi. Ndiyo maana hapa nmeipa jina "simba mwenda pole."
π©Ί Presha ya juu ni nini?
Ni hali ambapo damu inasukumwa kwa nguvu kubwa ndani ya mishipa ya damu kuliko kawaida. Hali hii inaweza kuathiri moyo, ubongo, figo na macho ikiwa haitadhibitiwa.
β οΈ Baadhi ya watu wanaweza kupata:
β’ Maumivu ya kichwa mara kwa mara
β’ Kizunguzungu
β’ Mapigo ya moyo kwenda kasi
β’ Kuchoka haraka
β’ Kupumua kwa shida
Hata hivyo, watu wengi wenye presha ya juu hawana dalili zozote.
π Nani yuko kwenye hatari zaidi?
β
Wenye uzito mkubwa kupita kiasi
β
Wanaokula chumvi nyingi
β
Ubwanyenye (sedentary lifestyle)
β
Wavutaji wa sigara
β
Wanaotumia pombe kupita kiasi
β
Wenye historia ya presha katika familia
π‘ Jinsi ya kujikinga na kudhibiti presha:
βοΈ Punguza matumizi ya chumvi
βοΈ Kula matunda na mboga za kutosha
βοΈ Fanya mazoezi mara kwa mara
βοΈ Dhibiti uzito wa mwili
βοΈ Epuka uvutaji sigara
βοΈ Pima presha yako mara kwa mara
π¨ Usisubiri mpaka upate matatizo makubwa. Kupima presha ni rahisi na kunaweza kuokoa maisha yako.
Afya njema huanza na hatua ndogo unazochukua leo. Jali moyo wako, jali maisha yako.
π Kwa ushauri na elimu zaidi kuhusu afya:
0717262733
π± Unaweza kupiga simu au kutuma ujumbe wa WhatsApp.