Veronica Majura

Veronica Majura Maisha Bora na Afya Bora, Utapata ushauri nzuri kuhusu afya yako na urembo, pia ni fulsa kwako kuongeza kipato

11/04/2026
31/03/2026

Watu wengi huangalia aina ya chakula pekee lakini husahau kuwa namna unavyopika inaweza kubadilisha kabisa kiwango cha kalori kinachoingia mwilini..

Kukaanga mara nyingi huongeza kalori kwa haraka kwa sababu chakula huchukua sehemu ya mafuta yanayotumika kupikia.. Hata ukitumia mafuta mazuri k**a Olive Oil bado kalori huongezeka kwa urahisi k**a kiasi hakitadhibitiwa..

Ndiyo maana watu wengi hujikuta wanashangaa kwanini hawapunguzi uzito ilhali wanahisi wanakula chakula kilekile isipokuwa wamekikaanga zaidi..
Kuchemsha ni njia rahisi inayosaidia kupunguza matumizi ya mafuta kwa kiasi kikubwa..

Chakula kinabaki na kalori zake za kawaida bila kuongezewa kalori za ziada kutoka kwenye mafuta mengi.. Hii husaidia kudhibiti jumla ya kalori kwa siku bila kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye aina ya chakula unachokula..

Kupika kwa mvuke ni moja ya njia zinazosaidia kuhifadhi virutubisho vya chakula huku ikiepuka kuongeza mafuta yasiyo ya lazima.. Njia hii husaidia chakula kubaki na ubora wake wa asili na hufanya iwe rahisi kudhibiti kiasi cha kalori bila kupunguza kiwango cha virutubisho unachopata..

Kosa ambalo wengi hufanya ni kufikiria kwamba aina ya chakula pekee ndiyo inaamua matokeo ya diet.. Ukweli ni kwamba njia ya kupika inaweza kuongeza au kupunguza kalori bila wewe kugundua..

Unaweza kula chakula kilekile lakini matokeo yakawa tofauti kulingana na namna kilivyopikwa..
K**a lengo lako ni kupunguza uzito, jaribu kupunguza vyakula vya kukaanga mara kwa mara na tumia zaidi kuchemsha, kuoka au kupika kwa mvuke pale inapowezekana..

Hii husaidia kudhibiti kalori bila kufanya diet iwe ngumu kufuata kwa muda mrefu..

Kesho nitatoa elimu kuhusu makosa yanayofanya watu washindwe kudhibiti kiasi cha chakula hata wanapokula vyakula vinavyoonekana kuwa vya diet..


#0752380570

Kwa siku za karibuni nimekuwa nikipokea maswali mengi sana kuhusu hali ya uzito kupungua lakini tumbo kubaki vilevile, h...
26/03/2026

Kwa siku za karibuni nimekuwa nikipokea maswali mengi sana kuhusu hali ya uzito kupungua lakini tumbo kubaki vilevile, hivyo leo naelezea kwa upana ili uelewe kinachoendelea bila kuchanganyikiwa..

Ukweli ni kwamba mwili haupunguzi mafuta sehemu unayotaka wewe, unapunguza mafuta kwa mfumo wake wenyewe kulingana na genetics, homoni, na mtindo wa maisha. Ndiyo maana unaweza kuona uzito unashuka kwenye mizani lakini tumbo bado linaonekana kubaki..

Sehemu ya tumbo ni moja ya maeneo ambayo mwili hupenda kuhifadhi mafuta kwa urahisi zaidi, hasa pale kunapokuwa na changamoto za homoni k**a Cortisol zinazoweza kuongezeka kutokana na stress au usingizi usio mzuri. Mafuta ya tumbo mara nyingi hupungua polepole kuliko sehemu nyingine k**a mikono au uso, jambo linalowafanya watu wengi kufikiri hawapigi hatua wakati ukweli ni kwamba mwili bado unaendelea kubadilika taratibu..

Pia, watu wengi hupoteza uzito wa maji au hata misuli mwanzoni, hasa k**a diet haina protini ya kutosha au hakuna mazoezi ya nguvu. Hapo mizani inaonyesha mabadiliko, lakini mafuta ya tumbo yanakuwa bado hayajapungua kwa kiwango kikubwa. Ndiyo maana kuangalia namba pekee kwenye mizani bila kuangalia muonekano wa mwili kunaweza kukupa picha isiyo sahihi ya maendeleo yako..

Tatizo lingine ni matarajio ya kupunguza mafuta sehemu maalum tu. Ukweli ni kwamba hakuna zoezi au chakula kinachoweza kulazimisha mwili kupunguza mafuta sehemu moja pekee. Unapofanya mazoezi ya tumbo, unajenga misuli ya eneo hilo lakini mafuta juu yake hupungua kulingana na mwili wako unavyoamua kutumia akiba ya mafuta kwa ujumla..

Watu wengi pia hukata tamaa mapema sana kwa sababu tumbo mara nyingi ni sehemu ya mwisho kuonyesha mabadiliko makubwa. K**a unaendelea kuwa kwenye mpangilio mzuri wa diet, kufanya mazoezi, kulala vizuri na kuwa consistent, tumbo nalo hupungua kadri muda unavyoenda. Tatizo ni kwamba wengi wanataka tumbo lipungue haraka kuliko mwili ulivyo tayari kubadilika..

Ukweli ambao wengi hawapendi kuusikia ni kwamba kupunguza mafuta ya tumbo kunahitaji kitu maalum njoo inbox chap
#0752380570

Kwa muda sasa nimekuwa nikipokea maswali mengi kuhusu nini hasa husababisha watu kupungua uzito kwa mafanikio, hivyo leo...
26/03/2026

Kwa muda sasa nimekuwa nikipokea maswali mengi kuhusu nini hasa husababisha watu kupungua uzito kwa mafanikio, hivyo leo nimeamua kuweka wazi ukweli ambao wengi hawauzingatii..

Kupungua uzito si bahati, wala si siri maalum ni matokeo ya tabia unazozirudia kila siku bila kukosa. Watu wengi wanatafuta mbinu za haraka au vitu maalum vya kula, lakini wanapuuza mambo madogo wanayofanya kila siku ambayo ndiyo huamua matokeo yao..

Kupungua uzito mara nyingi ni matokeo ya kula kwa kiasi kinacholingana na malengo yako. Hapa haimaanishi kula chakula maalum tu, bali kudhibiti kiasi cha chakula bila kuzidisha kalori bila kujua. Watu wengi wanakosea kwa kula vyakula vinavyoonekana kuwa vizuri kiafya lakini wakizidisha kiasi..

Ukweli ni kwamba hata chakula kizuri kinaweza kuzuia matokeo k**a hakitapimwa kwa kiasi sahihi..

Pia, kupungua uzito hutokana na kuwa na mpangilio unaoeleweka wa milo yako. Kuruka milo bila mpango au kula muda wowote bila utaratibu mara nyingi husababisha kula kupita kiasi baadaye. Nidhamu ya kula kwa utaratibu husaidia mwili kuwa na mfumo unaotabirika na kupunguza uwezekano wa kula bila mpango..

Tabia nyingine muhimu ni mwili kuushughulisha mara kwa mara. Hata k**a si mazoezi mazito kila siku, kuhakikisha mwili unatumia nguvu mara kwa mara husaidia kuongeza matumizi ya kalori..

Kukaa muda mrefu bila movement hupunguza kiwango cha nishati kinachotumika na kufanya iwe rahisi kalori kuzidi bila kujua..

Usingizi wa kutosha pia ni tabia ambayo watu wengi wanaipuuzia. Usingizi mdogo huathiri homoni zinazodhibiti njaa na kushiba, na kufanya mtu kula zaidi bila kupanga. Hii huathiri consistency ya diet hata k**a mwanzoni ulikuwa na mpango mzuri..

Ukweli ambao wengi hawataki kuukubali ni kwamba hakuna tabia moja inayoweza kufanya kazi peke yake. Matokeo yanatokana na mkusanyiko wa tabia ndogo ndogo zinazofanywa kwa muda mrefu bila kukata tamaa. Watu wengi hushindwa si kwa sababu hawajui cha kufanya, bali kwa sababu hawafanyi kwa muda wa kutosha kuona matokeo..

Kupungua uzito ni matokeo ya nidhamu ya kila siku, si motisha ya muda mfupi. Ukibadilisha tabia zako na kuzifanya ziwe sehemu ya maisha yako, matokeo yatakuja bila kulazimisha sana..

Watu wengi wanaanza diet na kuamini mbogamboga peke yake zitawafanya wapunguze uzito, lakini wanaharibu kila kitu kwenye...
24/03/2026

Watu wengi wanaanza diet na kuamini mbogamboga peke yake zitawafanya wapunguze uzito, lakini wanaharibu kila kitu kwenye namna ya kupika bila hata kujua. Tatizo si mbogamboga, tatizo ni jinsi zinavyopikwa. Unaweza kula mbogamboga kila siku lakini bado usione matokeo kwa sababu ya makosa madogo yanayojilimbikiza..🙌

Kosa kubwa la kwanza ni kutumia mafuta mengi kupika...Watu wanaweka mboga kwenye mafuta mengi wakidhani bado ni healthy, lakini wanasahau mafuta yana kalori nyingi sana... Hapa ndipo unajikuta umegeuza chakula kuwa bomu la kalori bila kujua. Diet yako inaonekana safi kwa macho, lakini kwa ndani umeiharibu..

Kosa lingine ni kupika kupita kiasi hadi mbogamboga zinapoteza virutubisho vyake...Unakuta mboga zimeiva sana, zimebadilika rangi na kuwa laini kupita kiasi...Hapa hupati faida kamili ya virutubisho, na pia ladha inapotea, hivyo unajikuta unaongeza mafuta au chumvi nyingi kujaribu kurekebisha..

Wengine wanaongeza vitu vingi vya ziada bila kufikiria mchuzi mzito, n**i, au viungo vyenye mafuta mengi...Hapa tena unaharibu ile faida ya mbogamboga kwa kuongeza kalori zisizo za lazima.. Unajidanganya unakula diet food, lakini ukweli ni tofauti..

Pia kuna kosa la kula mbogamboga pekee bila balance. Watu wanajaza sahani mboga tupu wakidhani ndiyo njia ya haraka kupunguza uzito, lakini hawapati protini ya kutosha...Hii inasababisha kushiba kwa muda mfupi na baadaye wanakula zaidi. Hapo unarudi pale pale ulipoanza..

Ukweli ambao wengi wanakwepa ni huu, si kila kitu kinachoonekana healthy ni sahihi kwa kupunguza uzito. Mbogamboga zinaweza kusaidia sana, lakini zikitumika vibaya zinapoteza maana yake kabisa... Diet siyo tu kula mboga, ni namna unavyozipika, kiasi unachotumia, na jinsi unavyo-balance na vyakula vingine..

K**a unataka matokeo ya kweli, acha kujidanganya na healthy look ya chakula. Wasiliana nami nikusaidie kupungua Kwa afya

#0752380570

22/03/2026

Tupo kukusaidia
Nitafute Kwa namba
0752380570

Asilimia kubwa ya watu wanaopunguza uzito kwa diet kali za muda mfupi, hupandisha tena uzito ule ule, au hata zaidi ya m...
22/03/2026

Asilimia kubwa ya watu wanaopunguza uzito kwa diet kali za muda mfupi, hupandisha tena uzito ule ule, au hata zaidi ya mwanzo, mara tu wanapoanza kula kawaida..

Hii ni kwa sababu metabolism hushuka sana ili kulinda mwili usife njaa..

> Kasi ipi ni Salama sasa?🤔

Wataalamu wa afya na lishe duniani kote wanashauri kupunguza kati ya nusu kilo hadi kilo 1 kwa wiki. Hii inamaanisha kwa mwezi mmoja, kupunguza kilo 2 hadi 4 ndiyo njia salama, na inayohakikisha unachoma mafuta badala ya kupoteza misuli..

Lengo lako linapaswa kuwa kuishi vizuri bila kuendekeza mipangilio mibaya ya chakula, siyo tu namba kwenye mizani..

Kupunguza uzito ni mabadiliko ya mfumo wa maisha, siyo mbio za siku 30..

Ikiwa elimu hii imekusaidia au imekufungua macho, basi usisite kulike na kushare ili wengine pia wapate kufaidika

Pia tuko na program ya kupungua Kwa afya Miezi 3-6 unarudi kwenye mwilini wako.
0752380570

Mara nyingi, tunapambana na njaa, tunapunguza wanga, na tunatoa jasho gym, lakini kuna siri ndogo ambayo tunaisahau..JE,...
22/03/2026

Mara nyingi, tunapambana na njaa, tunapunguza wanga, na tunatoa jasho gym, lakini kuna siri ndogo ambayo tunaisahau..

JE, MAJI UNAKUNYWA YA KUTOSHA!

Hivi ndivyo kunywa maji kunavyokusaidia moja kwa moja..

Maji ni k**a mafuta ya injini ya metabolism yako. Kunywa glasi mbili za maji ya kunaweza kuongeza kasi ya mwili wako kuchoma kalori kwa muda fulani..

Mara nyingi, mwili wetu huchanganya njaa na kiu. Unapohisi hamu ya kula, kwanza kunywa maji. Yanakushibisha na kukusaidia kula kidogo..

Upungufu wa maji husababisha uchovu haraka. Unapofanya mazoezi, unahitaji nishati ya kutosha ili kuchoma mafuta mengi zaidi..

Maji husaidia figo zako kuondoa sumu na taka mwilini, jambo linalofanya mfumo wako kufanya kazi zaidi..

USHAURI..

Weka malengo ya kunywa kati ya lita 2.5 hadi 3 za maji kwa siku. Iweke chupa yako ya maji karibu, na unywe hata kabla ya kuhisi kiu!

Ikiwa elimu hii imekusaidia au imekufungua macho, basi usisite kunitafuta Kwa program ya kupungua vzr bila stress

Unaweza kuwa na mwili unaoutaka angalia unakula nini
13/03/2026

Unaweza kuwa na mwili unaoutaka angalia unakula nini

Address

Mwenge Mpakani Center
Rajshahi Division

Telephone

+255752380570

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Veronica Majura posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Veronica Majura:

Share