11/12/2025
π Newcastle Disease β Venye Unaweza Kudili Nayo Kwa Kuku
Wasee, Newcastle ikikuingia kwa kuku, si mchezo.
Hakuna dawa ya kuimaliza direct juu ni virus, but unaweza control damage na upunguze vifo.
Hii ndiyo ukweli ya ground:
1. Wasaidie wale kuku wameanza ku-roll downhill
Hakuna dawa ya kuua virus, so unasaidia tu mwili ipigane.
Wape multivitamins (ile ya kuongeza nguvu)
Keep them warm β baridi huwa inamaliza faster
Hakikisha maji safi iko 24/7
Epua stress β no noise, no endless kuingia kwa banda
K**a uko na immune boosters, weka kwa maji
Basically unawa-boost wapate nguvu ya kushikilia.
2. Watenge haraka
Ukiona kuku:
Wanapumua vibaya
Wanageuza shingo k**a wana-mix deejay
Wanadunga chini tu
Wanaanguka k**a wamelewa
Wanaharisha kijani mbaya
Weka hao kwa corner yao.
Wasirushie wengine madharau ya ND.
3. Wachanjwe wale bado wako fiti
Ukiwa na Lasota ama F-strain, chanjo bado inasaidia kwa outbreak.
Chanja wale bado wanatembea, wanakula, wanachechemea kidogo but wako strong.
Hata k**a ugonjwa uko ndani, booster hupunguza vifo sana.
4. Banda usafi ni lazima
Newcastle inasambaa faster kuliko story ya plot π
Safisha:
Vyombo
Floor
Mikono
Viatu
Kuta
Tumia disinfectant ile hatucheki nayo.
5. Banda ipate hewa
Usiweke kuku mpaka wanapumuliana k**a matatu ya peak hour.
Ventilation ni muhimu sana.
6. Wale wamekufa β wachukue serious
Usiwaweke hapo nje k**a drama.
Choma ama uzike mbali na banda.