01/01/2022
*MWAKA MPYA, CHANGAMOTO MPYA.*
______________
Wapendwa zangu,
Amani, rehema, na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe nanyi daima!
Mwaka umekwisha na mwingine kuingia, je ni kipi tukitarajie?
Kwanza tunapaswa kuzitoa shukurani zetu za dhati kwa Mwenyezi Mungu aliyetujaalia kuufikia mwaka huu mpya, kwani *mwaka mpya ni changamoto mpya.*
Inawezekana mwaka uliopita ulikuwa eidha kwako au dhidi yako. Kipi kifanyike?
Kwanza, tufanye mahesabu. Tuangalie ni yapi tuliyoyafanya mazuri? Je ni yapi tuliyakosea? Je ni nafasi zipi tulisipoteza? Pili tuweke malengo mapya yatakayoambatana na dhamira madhubuti.
Pengine mwaka uliopita ulijaa vikwazo, matatizo, machungu, na mabaya basi hayo yote tuyasamehe na tuipokee hii changamoto mpya. Tuupokee mwaka mpya kwa kuusamehe uliopita na tuuone kuwa ni dhahabu tuliyoiokota jalalani. Tujihisi tumezaliwa upya ili tuyarekebishe yaliyopita. Tuuone kuwa ni mwaka mpya wenye changamoto mpya.
Pengine ulikuwa ni mwaka wenye mafanikio, mwaka wenye furaha na faraja, mwaka uliotuinua na kuzifikia neema za Mungu. Basi kwa hakika matunda hayo sio yote, tunahitaji zaidi yatulichokipata. Tuuone mwaka mpya kuwa ni muendelezo wa ubora tuliokuwa nao.
Mwanzo mzuri ni ule uliosheheni shukurani na maombi. Shukurani nzuri ni maombi, na maombi ndio shukurani nzuri. Tuuanze mwaka mpya kwa yote mawili na isiwe kinyume chake. Ninakutakia heri ya mwaka.
*Mwaka mpya, changamoto mpya.*
Wako rafiki,
Doctor Ibun Idris
Shafaa Rouhaniyyah
Simu: +265998293509
Telegram: https://t.me/doctoribunidris
Facebook: https://www.facebook.com/abdulhamid.othman.315
Instagram: https://www.instagram.com/invites/contact/?i=1e3km0mlbty6x&utm_content=ghsd216
You can view and join right away.