Kona Ya Ushauri wa Afya

Kona Ya Ushauri wa Afya Utapata ushauri na njia za kuimarisha afya yako

Klamidia ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na bakteria zinazoitwa na sayansi k**a Chlamydia trachomatis.Vijudu...
02/10/2025

Klamidia ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na bakteria zinazoitwa na sayansi k**a Chlamydia trachomatis.

Vijududu vinavyosababisha klamidia
Ugonjwa huo huwa hauonyeshi dalili za wazi kwa karibia asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume, hivyo maambukizi mengi hushindwa kufahamika mapema.

Kulingana na wakala wa afya wa Marekani Centers for Disease Control and Prevention ndiyo ya kwanza kati ya maradhi ya zinaa yanayoripotiwa zaidi nchini humo: wataalamu wamekisia kuwa karibia watu milioni tatu huambukizwa klamidia kila mwaka, lakini kulingana na CDC, ni maambukizi 660,000 tu ndiyo ambayo huripotiwa.

Watu ambao hawajafahamu kuwa wameambukizwa klamidia wanaweza wasitafute tiba na hivyo wakaendelea kufanya ngono, bila ya kujua kuwa wanaeneza ugonjwa.

Wakati dalili zinapoanza kujitokeza wanaume husikia maumivu wakati wa kukojoa au kutokwa usaha katika uume. Wanawake wanaweza kutokwa damu nje ya kipindi chao, maumivu wakati wa kukojoa, kutokwa usaha katika uke, au maumivu chini ya kitovu.

K**a utaachwa bila kutibiwa katika wanawake, klamidia inaweza kuleta madhara makubwa kwa afya ya binafsi na ya jamii. Klamidia huaribu tishu za uzazi za mwanamke na kusababisha uvimbe katika fupanyonga (pelvic inflammatory disease, PID). PID inaweza kusababisha mauvimu makali sana katika fupanyonga, utasa/ugumba au utata katika ujauzito ambao unaweza kusababisha kifo.

Watoto waliozaliwa na mama aliyembukizwa klamidia huwa na hatari ya kupata upofu au maambukizi katika mapafu.

Uchunguzi wa maambukizi ya klamidia hufanyika kwa kuchunguza fupanyonga na kiwango kidogo cha majimaji kutoka katika uke au uume ambayo huchunguzwa kwa uwepo wa Chlamydia trachomatis.

Uchunguzi mpya k**a ule wa mkojo ili kufahamu uwepo wa bakteria wa klamidia umekuwa ukitumika pia ili kufanya uchunguzi rahisi zaidi wa watu ambao hawaonyeshi dalili za ugonjwa.

Klamidia inatibika kwa antibaotiki.

Hiyo Sciatic Nerve ndiyo mshipa wa fahamu mkubwa katika mwili wa binadamu unaunganisha na imeesambaa eneo kubwa la mwili...
27/04/2024

Hiyo Sciatic Nerve ndiyo mshipa wa fahamu mkubwa katika mwili wa binadamu unaunganisha na imeesambaa eneo kubwa la mwili mikononi, miguuni na uti wa mgongo...niedelee au inatosha..🀣

06/01/2024
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema uchunguzi wa Maabara ya Taifa umethibitisha uwepo wa virusi vya Marburg ambavyo vina...
22/03/2023

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema uchunguzi wa Maabara ya Taifa umethibitisha uwepo wa virusi vya Marburg ambavyo vinasababisha ugonjwa wa Marburg Virus Disease (MVD) katika Mkoa wa Kagera ambao umesababisha vifo vya Watu watano hadi sasa ambapo amesema Ugonjwa huo hauna tiba mahususi bali hutibiwa kwa dalili anazokuwa nazo Mgonjwa.

Akiongea leo Dar es salaam, Ummy amesema β€œUchunguzi ambao tumeufanya katika Maabara yetu ya Taifa ya Afya ya Jamii umethibitisha uwepo wa virusi vya Marburg ambavyo vinasababisha ugonjwa unaojulikana k**a Marburg Virus Disease(MVD)” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Je,wajua??
18/12/2022

Je,wajua??

*KARIBUNI SANA WAGENI* Nikianza na Aliyeuliza juu ya mtoto wake:- Angalia nichakula gani anachopenda kisha mtafutien ung...
18/08/2022

*KARIBUNI SANA WAGENI* Nikianza na Aliyeuliza juu ya mtoto wake:- Angalia nichakula gani anachopenda kisha mtafutien unga wa lishe uliothibitishwa na Wizara ya Afya uitwao "Virutubisho" ndani yake una:-
1) *wanga*- kazi yake nikuleta nguvu mwilini.mfano Mahindi, ngano, viazi mchele.
2) *protin* kazi yake nikujenga mwili, mfano wa vyakula:- Nyama, njegere, mayai, maharage
3) *Vitamin* kazi yake kubwa ni kulinda mwili mfano Maembe, mananasi, Machungwa, zabibu.
4) *Madini* Huhusika sana katika kuuwezesha mfumo wa mwili, mfano, Chumvi, dagaa mboga za kijani, (vyanzo vya baadhi ya madin. Na faida nyingi sana ambazo vyote nilivyo kutajia hapo viko kwenye huo unga lishe, hivyo hii itakuwa nimsaada mkubwa kwa mtoto..

04/05/2022
Kwa wenye shida kuvimba viungo au joint kufa ganzi miguu na mikono..viungo kukaza
18/11/2021

Kwa wenye shida kuvimba viungo au joint kufa ganzi miguu na mikono..viungo kukaza

Thibitisha kauli hiiπŸ˜‚πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹
22/10/2021

Thibitisha kauli hiiπŸ˜‚πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹

Address

Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kona Ya Ushauri wa Afya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kona Ya Ushauri wa Afya:

Share