NICAS AFYA

NICAS AFYA Tunasaidia wanawake kuondokana na shida za azazi bila upasuaji.....Tiba zetu ni za virutubisho lishe.

Hapa kuna vyanzo kumi vya matatizo ya ugumba kwa wanawake na wanaume:Vyanzo vya matatizo ya ugumba kwa wanawake:1. Matat...
03/05/2023

Hapa kuna vyanzo kumi vya matatizo ya ugumba kwa wanawake na wanaume:

Vyanzo vya matatizo ya ugumba kwa wanawake:
1. Matatizo ya ovulation (kutokwa kwa yai)
2. Maambukizi ya njia ya uzazi
3. Endometriosis (ugonjwa wa kuenea kwa tishu za ndani ya mfuko wa uzazi)
4. Utoaji mimba uliopita kiasi (miscarriage)
5. Ugonjwa wa polycystic o***y syndrome (PCOS)
6. Ugonjwa wa fibroids (uvimbe wa kwenye mfuko wa uzazi)
7. Matumizi ya dawa za kukinga mimba muda mrefu (contraceptives)
8. Matatizo ya mfumo wa kinga ya mwili (autoimmune disorders)
9. Matatizo ya thyroid
10. Umri mkubwa (above 35 years)

Vyanzo vya matatizo ya ugumba kwa wanaume:
1. Uzalishaji mdogo wa manii
2. Kuziba kwa njia ya uzazi
3. Ugonjwa wa varicocele (uvimbe kwenye mishipa ya damu ya korodani)
4. Maambukizi ya njia ya uzazi
5. Matumizi ya dawa fulani (k**a steroids)
6. Uvimbe kwenye korodani
7. Ugonjwa wa prostate
8. Ugonjwa wa mifumo ya uzazi k**a hydrocele (uvimbe wa maji kwenye korodani)
9. Ulevi wa kupindukia
10. Umri mkubwa (above 45 years)

Ni muhimu kukumbuka kuwa sababu nyingi za ugumba zinaweza kutibika . Iwapo unadhani una tatizo la ugumba, unashauriwa kufanya vipimo na kuanza matibabu kuepusha tatizo kuwa sugu.

ugonjwa huu unaweza kujiknga nao kwa kuepuka mambo mbalimbali na kufanya mambo yatakayotusaidia kutopata ugonjwa huu kwa...
27/04/2023

ugonjwa huu unaweza kujiknga nao kwa kuepuka mambo mbalimbali na kufanya mambo yatakayotusaidia kutopata ugonjwa huu kwa kuzingatia kanuni ya afya na USAFI

1. Vaa chupi ambazo hazibani na zilizotengenezwa kwa pamba au hariri epuka kutumia chupi aina ya synthetic underwear.

2. epuka kufanya mapenzi na mpenzi wako mwenye maambukizi haya

3.kula mlo wenye virutubsho muhimu

4. epuka kuoga maji ya moto sana (Hot baths) tumia maji ya uvuguvugu

5.osha sehemu zako za siri kwa kutumia maji Safi na jikaushe kwa kutumia taulo au kitambaa Safi

6.usikae na pedi mda mrefu

7. kunywa maziwa aina ya mtindi yenye live culture Mara kwa Mara yatakusaidia kuepusha maambukizi ya fangasi ukeni.

8.epuka matumizi ya vifaa vya kupanga uzazi na vifaa vya kufanyia mapenzi (s*x toys, diaphragm cervical caps) husababisha maambukizi ya fangasi ukeni

9.epuka kutumia sabuni za kemikali/dawa kuoshea ukeni

*Najua Unapata Damu Ya Hedhi Inayoambatana Na Mabonge Mabonge/Vinyama Na Inayotoka Kwa Muda Mrefu...!*Kwa ujumla,chanzo ...
22/04/2023

*Najua Unapata Damu Ya Hedhi Inayoambatana Na Mabonge Mabonge/Vinyama Na Inayotoka Kwa Muda Mrefu...!*

Kwa ujumla,chanzo cha kuganda kwa damu wakati wa hedhi yako hutokana na kushindwa kutoka kwa ute
wenye kemikali unaozuia kuganda kwa damu kibaolojia
huitwa *anticoagulants*
ambapo kazi ya ute huu ni kuukinga ukuta wa kizazi usiharibike.

Wakati wa hedhi, ute mzito unakuwa kwenye ukuta wa
kizazi huanza kutoka. Ute huu unaokuwa na kemikali huanza kuachiliwa ili kuzuia damu isigande wakati wa
hedhi.

Wanawake wengi wanaotokwa na damu ya hedhi muda mrefu hutoka na damu yenye mabonge kwa sababu damu inayotoka kwenye ukuta wa mfuko wa
kizazi(uterus) hutoka kwa kasi kuliko ute wenye kemikali ya kuiyeyusha isigande.

Hali hi ndio husababisha damu kuganda na hedhi kutoka na mabonge ya damu kwa muda mrefu.

Visabibishi vya kupungua kwa ute huu (anticoagulants) ni
uwepo wa tatizo katika kizazi mfano.

♨️Uvimbe Katika Kizazi (Uterine Fibroids)
Uvimbe mmoja au zaidi.

♨️Matumizi ya njia za Kisasa za Uzazi Wa Mpango.
Dhumuni kuu la njia za kisasa za Uzazi wa mpango ni kuvuruga mpangilio wa homoni za mwanamke.Kivurugika
kwa homoni hauharibu tu ukomavu wa mayai bali
huharibu vichochezi ya homoni ya estrogen na Progesterone.

♨️Maambukizi
Aina ya kwanza ya maambukizi yanayoweza kusababisha
hali hi ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi ni maambukizi katika via vya uzazi(P.I.D)

Ili kujua chanzo cha tatizo ni vipimo vifuatavyo vinaweza kufanyika;
♨️ Ultrasound
♨️Kipimo cha homoni

Tatizo la kutokwa na hedi yenye magonge magonge au hedhi kwa muda mrefu linatibika vizuri kabisa kwa kutibu chanzo cha tatizo.

Wasiliana nami ujipatie suluhisho la tatizo lako

Address

Bariadi
789

Telephone

+255654967705

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NICAS AFYA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share