Afya Ya Mzazi na Mtoto

Afya Ya Mzazi na Mtoto You're Health is Our Concern ~
Call Us +255655562181 / +255769600821

KUTANUKA AU KULEGEA KWA MISULI YA UKE - - ( Vaginal Laxity).Kutanuka au kulegea kwa misuli ya uke (Vaginal laxity) ni ha...
15/12/2025

KUTANUKA AU KULEGEA KWA MISULI YA UKE - - ( Vaginal Laxity).

Kutanuka au kulegea kwa misuli ya uke (Vaginal laxity) ni hali ambapo misuli ya uke inapoteza uimara wake wa kawaida. Ni jambo la kiafya linalowapata wanawake wengi, hasa baada ya mabadiliko fulani ya mwili.

Sababu kuu:-

1. Kujifungua mara nyingi, hasa kwa njia ya kawaida (normal delivery).
2. Kuongezeka kwa umri – homoni ya estrogen hupungua.
3. Kupungua kwa homoni (hasa baada ya kujifungua au menopause).
4. Kufanya kazi nzito au kubeba mizigo mizito mara kwa mara.
5. Kukohoa kwa muda mrefu au kufunga choo (constipation) – huongeza presha kwenye misuli ya nyonga.
6. Kukosa mazoezi ya misuli ya nyonga (pelvic floor).

Dalili zinazoweza kuonekana.

- Kutoa hewa ukeni wakati wa Tendo na sauti k**a ya kujamba.
- Kuhisi uke β€œkuwa mpana” kuliko kawaida
- Kupungua kwa msisimko au raha wakati wa tendo la ndoa
- Kushindwa kujizuia mkojo (mkojo kutoka bila kutarajia)
- Hisia ya uzito au kitu kushuka chini ya uke

Muhimu kukumbuka - Si ugonjwa wa aibu, ni hali ya kawaida na inarekebishika

- Epuka kutumia vitu vya kuingiza ukeni visivyo salama (mimea, kemikali n.k.) bila ushauri wa kitaalamu
- Ukiona dalili zinaongezeka au una maumivu/kuvuja damu, muone mtaalamu wa afya.

KWA MSAADA ZAIDI πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

-πŸ“ž"Wasiliana nasi kuhusu afya - Kupitia Simu Namba 0655562181 / 0769600821

Β°Au Kuchart Nasi Moja Kwa Moja Watssapp Bofya link hapo chini πŸ‘‡πŸ‘‡
http://.wa.me/255655562181

- Pia Waweza Jiunga na Group letu la Afya la WhatsApp Kwa Kubonyeza Link Hii hapa πŸ‘‰πŸ‘‰πŸ‘‰ https://chat.whatsapp.com/C4qdsFaTDTB7tUPplBak8Q

, & Usaidie na Wengine

Address

Kijitonyama , Dar Es Salaam
Dar Es Salaam
T17

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya Ya Mzazi na Mtoto posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share