12/12/2020
Kisukari Husababishwa Na Nini?
Dalili Za Kisukari Na Je Kuna Tiba Ya Kisukari?
Kisukari ni ugonjwa wa kimetabolisim (ikimaanisha ni matokeo ya ufanyaji kazi wa mwili) unaotokea baada ya shida kwa mwili kupangilia utolewaji wa kichocheo ama hormone ya insulin. Hivo dalili za Kisukari ni matokeo ya kupanda kwa kiwango cha sukari kwenye damu kunakotokana na kufeli kwa kichocheo hiki cha insulin kufanya kazi, mpenzi msomaje hapa napenda uelewe kwamba kiwango cha sukari kwenye damu kitaaanza kuleta athari endapo kiwango cha insulin kinachomwagwa ni kidogo yaani hakitoshelezi kutokana na seli za beta zilizopo kwenye kongosho ambazo hutengeneza kichocheo hiki kuwa na hitilafu, sababu ya pili ni pale mwili unakuwa hausikii uwepo wa insulin kwenye damu kitaalamu tunaita INSULINI RESISTENCE., yaani kongosho linamwaga insulin kwenye damu lakini kiwango cha sukari bado kipo pale pale hapa ndipo tunapata kisukari cha ukubwani. Hii ni hatua mbaya kufikia ambapo wagonjwa wengi hukosa tumaini na hukata tamaa katika kutafuta dawa ya kisukari cha kupanda. Huhitaji kufikia huko fuata lishe sahihi utaishi bila Kisukari.
Aina Za Kisukari
Kuna aina kuu 2 za Kisukari, aina ya kwanza ambayo Kisukari cha utotoni na aina ya pili ya Kisukari ambacho ni Kisukari cha ukubwani.
1. Kisukari Cha Utotoni
Aina hii ya Kisukari huanza pale mtoto anapozaliwa hadi kufkia umri wa miaka 18 au 20, husababishwa na mpambano kati ya kinga ya mwili dhidi ya seli za beta ambazo hutengeneza homoni ya insulin (homoni inayorekebisha kiwango cha sukari kwenye damu), sasa mpambano huu hupelekea kupungua kwa uzalishaji wa insulini ama kukosekana kabisa kwa insulin kwene kongosho, na kwasababu miiili yetu imeubwa kutumia insulini wagonjwa hawa huhitaji kudungwa sindano za insulin kila siku ili kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.
Dalili Za Kisukar Cha Utotoni ( Type 1 Diabetes)
Wagonjwa wenye aina hii ya Kisukari huwa wamekonda na kudhoofu sana afya zao
▪Seli za kutengeneza kichocheo cha insulin zinakuwa zimeangamizwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mpambano na kinga ya mwili.
▪Kiwango cha insulin kwenye damu huwa kipo chini sana kutokana na uwezo mdogo wa kongosho kutengeneza insulin.
Kisukari Cha Ukubwani (Type 2 Diabetes)
Aina hii ya Kisukari nafahamika sana na imekuwa janga la dunia nzima likiathiri mamia ya watu kila siku. Kinyume na Kisukari cha utotoni, aina hii ya Kisukari husababishwa na kiasi kikubwa cha insulin kwenye damu. Hivo ukiwa na Kisukari cha ukubwani ni kwamba insulin iliyo nyingi kwenye damu na mwili hauwezi kuitumia vizuri hali hii kitalamu ni insulin resistence, ama kongosho yako inatengeneza insulini nyingi lakini imezidiwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu. Kupanda kupita kiasi kwa kiwango cha insulin kwenye damu huweza kuletekeza ama kupelekea matatizo mengine ya kiafya k**a.
▪Stroke na matatizo mengine ya utendaji wa ubongo k**a Alzheimer
▪Kupanda kwa shinikizo la damu
▪Magonjwa ya viuongo k**a arthritis
▪kupungua uwezo wa kuona na hatimaye Upofu
▪Kitambi na uzito mkubwa
▪Kufeli kwa figo
▪Kurundik**a kwa Mafuta mabaya kwenye viungo muhimu k**a ini
▪Saratani
▪Upungufu wa nguvu za kiume matatizo ya uzazi kwa wanawake k**a ugumba na uvimbe na
matatzo ya upumuaji/kupumua kwa shida na alegi.
Dalili Za Ugonjwa Wa Kisukari Aina Ya Pili(Kisukari Cha Ukubwani)
▪Kupumua kwa shida, alegi
▪Vidonda kutopona mapema, maambukizi ya mara kwa mara.
▪Kuongezeka uzito kusiko kawaida pengine hata bila kubadili lishe yako.
▪Kupata kiu ya mara kwa mara na mdomo kukauka
▪Mwili kujiskia mechoka mda mwingi na kupata ganzi kila mara.
▪Kupata athari za neva na kusababisha maumivu ya viungo na kutetemeka kwa miguu na mikono
▪Kupungua kwa uwezo wa kuona
▪Kupata njaa na kujiskia kula mara kwa mara, hata k**a umekula hivi karibuni
▪Kupoteza uwezo wa kufatilia mambo na kujitambua (consciousness) .
Kumbuka kwamba siyo lazima uone dalili zote hizi ndipo unaashiria umeanza kuugua Kisukari, unaweza kujipima mwenyewe na kuchukua hatua ya kufika hospitali upate ushauri ili upunguze hatari ya kuugua Kisukari.
Hivo magonjwa haya huambatana na tatizo la Kisukari na kadri ugonjwa unavokomaa na kufkia hatua mbaya ndivyo magonjwa haya ambatanishi yanavojitokeza Zaidi, najua unaweza kuwa ni muhanga wa ugonjwa huu na umeteseka kwa miaka mingi umetumia madawa mengI bila mafanikio, napenda kukupa tumaini kuwa suluhisho lipo, ni kurekebisha lishe yako tu na kutumia virutubisho muhimu. Unachotakiwa ni kufuta imani ulopewa hapo awali kwamba kula mboga za majani kwa wingi na matunda, maana elimu hiyo haijakusaidia na bado unaumwa na kuteseka na Kisukari.
Nini Chanzo Cha Kisukari Cha Ukubwani?
Kwanza kabisa ni vyema kufahamu kwamba ugonjwa wa Kisukari siyo ugonjwa wa kuwa na sukari nyingi hapana, Kisukari ni ugonjwa wa homoni, homoni ya insulin, kumbuka kwamba mwili unahitaji kiwango kidogo tu cha glucose kukibadilisha kuwa nishati ili kuendesha shuguli zake, kiwango kingine kinachozidi huwa hakipotei bali huhifadhiwa katika seli za mwili kwenye mfumo wa mafuta, hivo kazi ya insulin ni kusukuma sukari iliyozidi kwenda kwenye seli ili ibadilishwe kuwa mafuta. Sasa inapotokea mwili hausikii uwepo wa insulin kwenye damu yaani insulin inamwagwa lakini kiwango cha sukari kwenye damu kipo pale pale hao ndipo hatari ya kuugua Kisukari cha ukubwani huanza.
Sasa ni wakati wa kutambua kwamba aina ya chakula unachokula kinachangia kwa kiasi kikubwa kupata magonjwa haya k**a Kisukari na uzito mkubwa,vyakula k**a wanga na sukari hupandisha insulin kwenye damu kwa kasi sana huku vyakula vya protini na mafuta vikithibitika kupandisha insulin kwa kiasi kidogo sana. Kula wanga na sukari nyingi na kufanya mazoezi sana haikusaidii kuepuka magonjwa haya ya Kisukari na uzito mkubwa badala yake kula vyakula vya mafuta k**a parachichi, samaki, nyama, mayai , n**i na mboga za majani kwa wingi muhimu.
Natumaini tumepata kujifunza kuhusiana na Ugonjwa wa kisukari na sisi tunadeal na ushauri wa kiafya na usambazi wa virutubisho au tiba lishe kwa ajili ya kupambana na haya magonjwa sugu tuna virutubisho kwa ajili ya kusaidia tatizo la kisukari lakini pia kwa ajili ya kujikinga dhidi ya kisukari kwa maelezo au jinsi ya kupata maelezo zaidi wasiliana nasi kwa kupiga au sms +255 785 520 102 (Ipo pia WhatsApp) au +255 785 520 102 karibuni nyote kusudi letu ni kujenga Tanzania yenye afya bora naomba ulike page yetu na ushare na wenzako wengi ili wapate hizi taarifa njema za kiafya asante sana.
Hapa chini ni shuhuda ya mgonjwa wetu tuliyemuhudimia katika tatizo la kisukari pata kumtaza kwa kubonyeza hii link hapa chini 👇👇👇
https://youtu.be/7tpi7cKOMgQ