29/07/2022
Kipanda uso(Migraine) ni tatizo ambalo huhusisha mtu kupatwa na maumivu makali sana ya kichwa ambayo hutokana na sababu mbali mbali k**a vile;
hali ya kutanuka kwa mishipa ya damu kichwani k**a vile mishipa aina ya Artery,Β
mabadiliko ya mfumo wa damu yaani Blood stream na mabadiliko ya vichocheo k**a vile; kichocheo aina ya Serotonin ambacho huhusika na kudhibiti kiwango cha maumivu kwenye mfumo wa fahamu.
Vyote hivi huchangiwa na sababu mbali mbali k**a vile;
β Mtu kuwa na msongo wa mawazo
β Matumizi ya pombe kali kupita kiasi
β Kunywa vinywaji vyenye caffeine nyingi k**a kahawa N.k
β Kukosa muda wa kutosha wa kulala
β Matumizi ya dawa mbali mbali k**a vile; vidonge vya uzazi wa mpango n.k
β mabadiliko ya hali ya hewa mfano; Kuwa na jua kali pamoja na joto sana
N.k
DALILI ZA TATIZO LA KIPANDA USO(MIGRAINE) NI PAMOJA NA;
Siku moja au mbili kabla ya tatizo hili kutokea,mtu huweza kupata mabadiliko k**a vile;
β’ Kuanza kupata choo kigumu
β’ Kupoteza mood
β’ Shingo kukak**aa
β’ Kiu ya maji kuongezeka sana pamoja na mtu kukojoa sana
β’ Mtu kupiga miayo sana
β’ Kuanza kupata shida ya kutokuona vizuri au kuona marue rue
NDIPO BAADAE dalili zingine hujitokeza mfano;
- Maumivu makali ya kichwa
- Mshipa kucheza chezaΒ upande mmoja wa kichwani
- Kupatwa na hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika
- Mtu kupata kizunguzungu kikali
- Kuhisi sauti za makelele masikioni
- Kupata shida ya kuongea
- Mwili kutetemeka
- Mwili kukosa nguvu
- Dalili za kuchanganyikiwa
N.K
MATIBABU YA TATIZO HILI LA KIPANDA USO
β’ Zipo dawa mbali mbali za kuondoa maumivu haya k**a vile; Ibuprofen, Paracetum N.k
japo endapo mtu hupata dalili mbaya zaidi k**a kushindwa kuongea,mwili kutetemeka, n.k ni vizuri kuwaona wataalam wa afya.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255683481046
πΉπΏ