Msingi wa afya ni kuijua afya yako.

Msingi wa afya ni kuijua afya yako. Nasaidia kutatua changamoto za kiafya kwa kutumia virutubisho lishe.

JE? WAJUA MAANA YA CD4 NA KAZI ZAKE MWILINICD4+ ni aina ya seli nyeupe za damu zinazohusika na kinga  dhidi ya magonjwa ...
13/03/2023

JE? WAJUA MAANA YA CD4 NA KAZI ZAKE MWILINI

CD4+ ni aina ya seli nyeupe za damu zinazohusika na kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na pia zinasaidia seli nyingine za kinga ya mwili. CD4+ hushambuliwa na na VVU kwa sababu katika hizi seli virusi huzaliana. CD4+ hupungua taratibu hivyo na hivyo magonjwa nyemelezi huanza kushambulia na hata kusababisha kifo.

1.Kiwango cha kawaida cha CD4+ ni 1000. Mtu mwenye maambukizi ya VIRUSI VYA UKIMWI CD4+ hupungua kwa kiwango cha seli 60 kwa mwaka

2.CD4+ 400-200 (baada ya miaka 7)
Katika kiwango hiki mtu anay+zknaeishi na VVU huanza kuonyesha dalili mfano kupungua uzito, homa, kuvimba mitoki pamoja na kutoka jasho wakati wa usiku. Pia mgonjwa hupata maradhi ya ngozi mfano mkanda wa jeshi pamoja na uchovu.

CD4 zinapokuwa chini ya 400 maambukizi ya bacteria mfano Kifua Kikuu (Tb) huongeza zaidi

3.CD4+ pungufu ya 200 (mwaka wa nane)
Magonjwa nyemelezi ambayo ni hatari zaidi huanza kushambulia mwili baada ya kinga kushuka zaidi, mfano nimonia kali, maambukizi ya fangasi na minyoo kwenye ubongo.

4.CD4+ chini ya 50
Katika kiwango hiki cha CD+ kinga ya mwili ni k**a haifanyiki kabisa. Baadhi ya maradhi ambayo hayaathiri binadamu huweza kusababisha maradhi na hata kifo.

KWA TIBA NA USHAURI WASILIANA NASI
0652 400 350

JE WAJUA KUWA KIHARUSI KINATIBIKA?KIHARUSI (STROKE) NI UGONJWA GANI?Stroke au kiharusi ni tatizo linalotokea ghafla kwen...
07/03/2023

JE WAJUA KUWA KIHARUSI KINATIBIKA?
KIHARUSI (STROKE) NI UGONJWA GANI?

Stroke au kiharusi
ni tatizo linalotokea ghafla kwenye ubongo ambapo mtiririko wa damu kwenye eneo fulani la ubongo husitishwa ghafla au kupungua sana hivyo kusababisha eneo hilo la ubongo kukosa damu na virutubishi muhimu na seli za eneo hilo kuanza kufa. Hili linaweza kutokea pale mishipa ya damu ya kuelekea kwenye eneo hilo ikiziba au mishipa ndani ya ubongo katika eneo hilo kupasuka. Seli za ubongo za eneo hilo zikianza kufa kwa kukosa damu, shughuli zote zinazoendeshwa na eneo hilo la ubongo husimama kwa mfano kumbukumbu au misuli.

NB
Kiharusi ni ugonjwa wa dharura hivyo tiba inatakiwa ipatikane mapema iwezekanavyo. Kimsingi kiharusi huweza kumpata mtu ye yote wakati wowote.

AINA ZA KIHARUSI
Kuna aina tatu za stroke; ischemic, hemorrhagic na TIA. Kundi la watu lililo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu ni lile la watu wenye miili mikubwa, umri zaidi ya miaka 55, wenye historia ya ugonjwa huu kwenye familia zao, ambao hawafanyi mazoezi , wanaokunywa sana pombe au kutumia madawa haramu.

Kiharusi Husababishwa Na Nini?

Kila moja ya aina za stroke hapo juu inasababishwa na vitu tofauti.

1)Ischemic strokes, ndiyo aina ya stroke inayowaathiri watu wengi zaidi, asilimia 85 ya wagonjwa wa stroke hupatwa na aina hii ya stroke. Aina hii ya stroke husababishwa na kuziba kwa ateri (mishipa ya kusafirisha damu safi) zinazoelekea kwenye ubongo au kusinyaa kwa mishipa hiyo, hivyo kusababisha hali inayoitwa ischemia (upungufu mkubwa wa mtiririko wa damu).
Kuziba kwa mishipa ya damu hutokea baada ya damu kuganda ndani ya ateri zinazoeleka kwenye ubongo au katika maeneo ya mbali zaidi na kusukumwa kwenye mishipa yenye kipenyo kidogo ndani ya ubongo. Mishipa hii inaweza kuzibwa pia na mafuta yaliyoganda ndani ya ateri (plaque).

2)Hemorrhagic strokes, husababishwa na ateri ndani ya ubongo kuvuja damu au kupasuka. Damu hii iliyovuja huleta mgandamizo kwenye seli za ubongo na kuziharibu. Kupasuka kwa mishipa ya damu husababishwa na hypertension, trauma au dawa zinazofanya mishipa hii ya damu kupungua unene wake

3)Transient ischemic attack (TIA), hii ni tofauti na aina hizo mbili za stroke hapo juu kwani hapa mtiririko wa damu kuelekea kwenye ubongo huvurugwa kwa muda mfupi kwa sababu zile zile tulizozitaja hapo juu tulipozungumzia ischemic strokes. Stroke ya aina hii ni ishara ya kutokea strokes nyingine baadaye k**a hatua zinazostahili hazitachukuliwa.

Dalili Za Kiharusi (Stroke)

Ugonjwa wa stroke humpata mtu ghafla na dalili hutokea kwa muda mfupi sana. Dalili kuu za ugonjwa huu ni:
• Kuchanganyikiwa, mtu akipata shida ya kuongea na kuelewa anachoambiwa
• Maumivu ya kichwa yanakwenda pamoja na kupoteza fahamu kwa vipindi na kutapika
• Ganzi katika viungo vya uso, mkono na mguu na hasa vikiwa vya upande mmoja wa mwili
• Kupata shida ya kuona kwa jicho moja au yote
• Kupata shida ya kutembea vikichanganyika na kizunguzungu na kukosa mpangilio wa matendo ya mwili

ATHARI ZA KIHARUSI zinaweza kuwa ni za muda mrefu. Kulingana na muda uliopita kabla ya kuugundua na kuutibu ugonjwa huu,

mtu anaweza kupata ulemavu wa muda mfupi au wa kudumu. Pamoja na madhara ya stroke k**a yalivyoorodheshwa hapo juu,

mgonjwa wa stroke anaweza pia kupata yafuatayo:
• Msongo wa mawazo
• Maumivu kwenye mikono na miguu yanayoongozeka baada ya viungo hivyo kufanya kazi au kutokea mabadiliko ya hali ya hewa.
• Kupooza au udhaifu wa upande mmoja wa mwili
• Kupata shida katika kufanya matendo ya kuonyesha hisia za mwili
• Kushindwa kumudu matumizi ya kibofu cha mkojo au viungo vya njia ya haja kubwa

TIBA ZA STROKE NA NAMNA YA KUZUIA STROKE

Kwa vile aina kuu mbili za stroke, ischemic na hemorrhagic, kila moja ina chanzo kilicho tofauti, kila moja inahitaji tiba iliyo tofauti na ya aina nyingine. Ni sharti kujua kwa uhakika ni aina gani ya stroke iliyotambuliwa kwani tiba ya stroke ya aina moja inaweza kuwa na madhara kwa stroke ya aina nyingine.

1)TIBA KWA ISCHEMIA STROKE: Ischemic strokes hutokea pale mishipa ya damu inapoziba au kupungua kipenyo hivyo tiba ya tatizo hili ni kuhakikisha damu ya kutosha inaufikia ubongo. Tiba huanza kwa kotoa dawa za kuyeyusha damu au mafuta yaliyoganda na kuzuia hali hiyo isitokee tena.

2)TIBA KWA HEMORRHAGIC STROKE: Stroke ya aina hii hutokea pale damu inapovuja ndani ya ubongo hivyo tiba yake italenga katika kuzuia damu isiendelee kuvuja na kupunguza mgandamizo wa damu iliyovuja juu ya ubongo. Tiba huanza kwa kutoa dawa za kupunguza mgandamizo kwenye ubongo, kupunguza msukumo wa damu kwa ujumla na kuzuia kusinyaa kwa ghafla kwa mishipa ya damu.

ILI KUJILINDA NA STROKE AU KUZUIA STROKE YAFUATAYO YANAWEZA KUFANYWA:
• Kutotumia madawa haramu
• Kula chakula chenye mboga na matunda kwa wingi na chenye cholesterol kidogo
• Kufanya mazoezi kila wakati
• Kuhakikisha unadhibiti blood pressure
• Kuhakikisha unadhibiti kiwango cha sukari mwilini
• Kuwa una uzito unaofaa
• Kunywa pombe kwa kadri au kuacha kabisa
• Kuacha kuvuta sigara
WASILIANA NASI KWA TIBA NA USHAURI
0652 400 350

JE?WAJUA KUWA MSH*TUKO WA MOYO (HEART ATTACK) UNATIBIKAMsh*tuko wa moyo hutokea pale mtiririko wa damu kuelekea kwenye m...
04/03/2023

JE?WAJUA KUWA MSH*TUKO WA MOYO (HEART ATTACK) UNATIBIKA

Msh*tuko wa moyo hutokea pale mtiririko wa damu kuelekea kwenye moyo unapozibwa. Mara nyingi kuziba huku hutokana na kujikusanya kwa mafuta, cholesterol na vitu vingine, ambavyo hufanya utando ndani ya ateri zinazopeleka damu kwenye moyo (coronary arteries). Mara nyingine utando huu hubomoka na kufanya donge la damu linaloziba mtiririko wa damu. Kuziba huku kwa damu kunaweza kuharibu sehemu ya musuli wa moyo.

Mshtuko wa moyo, ambao kitaalamu huitwa myocardial infarction, unaweza kuua, lakini siku za karibuni tiba yake imeboreshwa. Ni muhimu kupiga 911 au namba ya dharula endapo unahisi unanyemelewa na mshtuko wa moyo.

Dalili Za Msh*tuko Wa MOYO

Dalili za kawaida za msh*tuko wa moyo ni pamoja na: Pressure, kubana kifua, maumivu, na kubana au kuwashwa kifuani na mikononi kunakoweza kuenea hadi maeneo ya shingo, taya au mgongoni Kichefu, kuvimbiwa, kiungulia au maumivu ya tumbo Kuhema kwa shida Jasho baridi Uchovu Kizunguzungu cha ghafla

Dalili Za Msh*tuko Wa Moyo Hutofautiana
Si watu wote wanaopata msh*tuko wanapata dalili zile zile au za uzito ule ule. Wengi hupata maumivu ya kiasi, wengine maumivu makali. Wengine hawaoni dalili zo zote. Kwa baadhi yao, dalili ya kwanza ni moyo kusimama kufanya kazi.
Mash*tuko wa moyo mara nyingine huja ghafla, lakini kwa watu walio wengi, dalili huonekana saa, siku au hata wiki kadhaa kabla. Dalili ya wawali kabisa yaweza kuwa maumivu kifuani yanayojirudia (angina) yanayoanza unapokuwa na shughuli na kuacha ukipumzika. Angina husababishwa na kupungua kwa muda mfupi kwa mtiririko wa damu kwenye moyo.

Nini Cha Kufanya K**a Unaona Mtu Amepatwa na Msh*tuko Wa Moyo
K**a unamwona mtu amepoteza fahamu na unahisi amepata msh*tuko wa moyo, kwanza piga simu kuomba msaada wa dharula. Kisha chunguza k**a anapumua na ana mapigo ya moyo. K**a hapumui na hana mapigo ya moyo, mpe huduma ya CPR.
Sukuma kwa nguvu na kwa haraka juu ya kifua chake ukitumia misukumo ya haraka inayolingana – k**a misukumo 100 hadi 120 kwa dakika.

Chanzo Cha Msh*tuko Wa Moyo

Msh*tuko wa moyo unatokea wakati ateri moja au zaidi ya moja ya kupeleka damu kwenye moyo inapoziba. Muda ukienda, mafuta ikiwa ni pamoja na cholesterol, hujijenga na kutengeneza plaque, ambayo itapunguza kipenyo cha ateri (atherosclerosis). Hali hii, iitwayo ugonjwa wa ateri za moyo (coronary artery disease), ndicho chanzo cha mish*tuko ya moyo iliyo mingi.

Wakati msh*tuko unapotokea, plaque inaweza kuwa imebomoka na kumwaga cholesterol na vitu vingine ndani ya mkondo wa damu. Donge la damu hutokea eneo plaque ilipobomoka. Endapo donge hilo ni kubwa, linaweza kuziba mtiririko wa damu ndani ya ateri, na kuufanya moyo ukose oksijeni na virutubishi (ischemia).

Unaweza kuwa na tatizo la mishipa kuziba kiasi au kuziba kabisa.
Ikiziba kabisa una ST elevation myocardial infarction (STEMI). Ikiziba kiasi una non-ST elevation myocardial infarction (NSTEMI).

Uchunguzi na tiba hutofautiana kulingana na aina ya tatizo ulilo nalo.

Sababu nyingine ya msh*tuko wa moyo ni kukaza kwa ghafla kwa mshipa wa damu unaoelekea kwenye moyo (spasm of a coronary artery) ambako kutazuia damu isifike kwenye eneo fulani la musuli wa moyo. Matumizi ya tumbako na madawa ya kulevya, k**a co***ne, huweza kusababisha hali hii inayotishia maisha.

WASILIANA NASI KWA TIBA NA USHAURI
0652 400 350

JE? WAJUA KUWA MOYO MPANA UNATIBIKAMoyo nikiungo kinacho sukuma damu mwilini kupitia mishipa ya damu mwilini.MISHIPA YA ...
01/03/2023

JE? WAJUA KUWA MOYO MPANA UNATIBIKA

Moyo nikiungo kinacho sukuma damu mwilini kupitia mishipa ya damu mwilini.

MISHIPA YA DAMU (BLOOD VESSELS) ni mirija maalumu ambayo inasambaza damu sehmu zote za mwili

DAMU ni kimiminika chenye rangi nyekundu kInachopita kwenye mishipa ya damu. kazi yake nikubeba hewa ya oxygen,chakula,virutubisho, hormones nk nakupeleka sehemu ambako mwili unahitaji

MOYO KUPANUKA Ni hali inayosababishwa na ukinzani wa moyo jinsi unavyotoa na kuingiza damu katika mishipa ya moyo na kuelekea sehemu mbalimbali za mwili.

• Moyo kupanuka kutokana na kutokana na mazingira ya kusukuma damu kwa nguvu ya ziada tofauti na kawaida, hivyo kusababisha misuli ya moyo kutanuka.

• Moyo ukiwa mpana hadi uwezo wake wa kusukuma damu unashuka hadi kupelekea kushindwa kabisa kusukuma damu na ile safi na chafu huchanganyika

KWA TIBA NA USHAURI WASILIANA
+255 652 400 350

Je? WAJUA  KUWA PRESHA YA KUPANDA (HYPERTENSION) INATIBIKA.JE?WAJUA MAANA ,VISABABISHI,DALILI,MADHARA NA TIBA ZAKE.1) MA...
27/02/2023

Je? WAJUA KUWA PRESHA YA KUPANDA (HYPERTENSION) INATIBIKA.
JE?WAJUA MAANA ,VISABABISHI,DALILI,MADHARA NA TIBA ZAKE.

1) MAANA YA PRESHA YA KUPANDA , hii ni hali ya kuwepo na ukizani wa damu kupita vizuri kwenye mishipa ya damu yaani moyo unasukuma damu na wakati mishipa ya damu hairuhusu damu kupita ipasavyo
2) VISABABISHI VYA PRESHA YA KUPANDA :
1) Uzito mkubwa
2) Kula vya kula vya wanga sana
3) Kula vyakula vilivyo pikiwa mafuta ya viwandani kwa wingi
4) Historia ya familia / ukoo
5) Uvutaji wa sigara na unywaji pombe
6) Kutofanya mazoezi
3) DALILI ZA PRESHA YA KUPANDA
1) Kifua kuuma upande wa kushoto ,maumivu yanakwenda mpaka kwenye kidevu
2) Mtu kuchoka hata akifanya kazi ndogo au kupandisha ngazi
3) Miguu kuvimba
4) Wakti mwingine kichwa kuuma (haswa nyuma ya kichwa na asubuhi)
4) MADHARA YA PRESHA YA KUPANDA
1) HUPELEKEA MOYO KUPANUKA(MOYO MPANA)
2) KIHARUSI(STROKE)
3) SHAMBULIO LA MOYO(HEART ATTACK)
4) FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI
5) KUPATWA GAZI BAHADHI YA SEHEMU ZA MWILI
6) MIGUU KUWAKA MOTO NA KUVIMBA
7) UPUNGUVU WA NGUVU ZA KIUME
8) UPOFUA (KUFANYA MTU HASHINDWE KUONA)
5) NAMNA YA KUTATUA TATIZO LA PRESHA WASILIANA NASI KWA TIBA NA USHAURI
+255 652 400 350

HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEPATWA NA PRESHA YA KUSHUKAMaisha yamejaa mambo ya kushangaza na vitu vingi vigeni. Hata hi...
22/02/2023

HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEPATWA NA PRESHA YA KUSHUKA

Maisha yamejaa mambo ya kushangaza na vitu vingi vigeni. Hata hivyo, kwa kuwa na elimu nzuri na iliyosawa kabisa mtu anaweza akarekebisha matatizo yanayoweza kutokea ghafla.

Presha ya kushuka:
Presha ya kushuka (Low Blood Pressure (BP)), au kwa lugha ya kisayansi huitwa Hypotension. Hali hii inatokea pale msukumo wa damu unapokuwa mdogo na dhaifu, hali ambayo husababisha kila kiungo katika mwili k**a vile ini, mapafu, moyo nk. Kushindwa kupokea kiasi kinachojitosheleza cha damu na Oxygen.

Sababu za Presha ya Kushuka: ·

Mshtuko ·
Ukataji tama ·
Mawazo mengi yaliyopitiliza ·
Mlo usio kamili – vitamin, Protini na ukosefu wa madini ·
Ukosefu wa maji mwilini.

Dalili: ·

Udhaifu usioutegemea (ghafla) ·
Udhaifu au kuona ukungu. ·
Mdomo kukauka ·
Kizunguzungu ·
Kuanguka ghafla na kupoteza fahamu.

Huduma ya kwanza:
K**a mtu ataanza kusikia kizunguzungu, muweke akae katika kiti au mlaze chini. ·

Mnyanyue kichwa chake wakati ukiwa umemlaza chini, kwa kumuwekea mito chini ya kichwa chake. ·

Haraka mnyweshe maji uliyochanganya na chumvi au mpatie mgonjwa huyo electrolyte solution. ·

Kuwa makini unapomuinua kutoka chini au sehemu aliyokuwa amekaa. Muinuko wa ghafla unaweza kuzidi kupunguza msukumo wa damu. ·
Hali ikidumu kwa muda mfunge mgonjwa katika mguu wake umbali wa nchi k**a tano hivi chini ya goti kwa kutumia lastiki au mpira unaovutika ili kuzuia damu isiende chini ya miguu, ili kufanya damu ibakie hasa sehemu ya juu ya mwili. ·

Ushauri
Kunywa juisi ya kiazisukari kibichi au maziwa ya mtindi ni dawa nzuri ya presha ya kushuka.

Onyo: ·

Punguza kunywa Vinywaji vya alcohol au kafeini ·
Jitahidi kuwa unakula matunda freshi na mbogamboga katika mlo wako ·
Jitahidi kunywa maji mengi ili kuepuka ukosefu wa maji ·
Usipende kunyanyua mizigo mizito sana. ·
Chukua mazoezi kwa ratiba maalum.

Kumbuka dharura huwa hazipigi hodi zinapokuja katika maisha yako. Hivyo basi, siku zote kuwa ni mwenye kujiandaa. Wakati mwingine matendo madogo madogo na kuwa na akili iliyotulia inaweza ikaokoa uhai, mpaka pale dharura za kitabibu zitakapofika.

Wasiliana nasi kwa tiba na ushauri
+255 652 400 350

Je wajua Maana ya Msongo Wa Mawazo; Visababishi Na Dalili Za Msongo Wa MawazoMara nyingi sana umesikia mtu akisema “nina...
20/02/2023

Je wajua Maana ya Msongo Wa Mawazo; Visababishi Na Dalili Za Msongo Wa Mawazo

Mara nyingi sana umesikia mtu akisema “nina stress”, mwingine akasema ana msongo wa mawazo na mara chache katika mazungumzo ukasikia mtu akitumia neno mfadhaiko. Haya ni maneno yanayoingiliana kimazungumzo mitaani na mara nyingi mtu hutumia neno moja katika hayo bila kujua tofauti zake. Katika mada yetu tutayachambua na kujua tofauti za matatizo yanayowasumbua watu hadi kupelekea kuyatumia maneno haya. Na mwisho tutatoa ushauri wa namna ya kuondokana na matatizo hayo.

Maana Ya Stress Au Msongo Wa Mawazo



Maisha ya dunia ya leo yamejaa pilikapilika za kila aina, una vitu vingi vya kuvifanya katika muda uliopangiwa (deadlines), vitu vingi vya kukukatisha tamaa na matakwa mengi ya binafsi na watu walio karibu na wewe. Mtindo huu wa kuishi umekuwa karibu ni wa kila mtu. Kila wakati unakuwa na msongo wa mawazo (Stress). Msongo wa mawazo kwa kiasi fulani siyo mbaya, unakusaidia kutekeleza majukumu yako ukiwa umebanwa na kukupa nguvu ya ziada ya kuyafanya vizuri kadiri ya uwezo wako. Lakini k**a utaendelea kufanya shughuli zako kwa mtindo huu, wakati utafika ambapo ubongo wako utachoka na kupata tatizo la kiafya linaloitwa mfadhaiko (Depression).

Kwa hiyo msongo wa mawazo (Stress) ni namna ya kawaida ya mwili wako kukabiliana na mambo ya kukutisha au kukufanya uwaze.

Unapohisi hatari, ya kweli au siyo ya kweli, mwili hukupa nguvu haraka kukabilina na suala lililopo mbele yako, hii ni ni namna ya mwili wako kukulinda. Katika mazingira hayo, mwili hukufanya uwe mwangalifu zaidi na kukupa nguvu ya ghafla. Katika mazingira ya hatari, unaweza kuokoa maisha yako kwa kupata hiyo nguvu na ujasiri wa ghafla. Mfano mzuri ni pale unapoendesha gari na ghafla ukakanyaga breki za gari kuzuia ajali mbele yako.

Msongo wa mawazo hukusaidia kukabiliana na vikwazo mbalimbali. Utakuwa makini sana wakati unawasilisha mada mbele ya kadamnasi, utakuwa na umakini zaidi wakati unashiriki kwenye mechi na timu pinzani na utasukumwa kwenda kusoma ili ujiandae kwa mitihani yako badala ya kuangalia kipindi kizuri cha kwenye luninga unachokipenda.

Lakini k**a tulivyodokeza hapo awali, kiwango cha msongo wa mawazo kikizidi, badala ya kukusaidia kitakuletea matatizo ya afya, kitaathiri utendaji wako wa kazi, kitavuruga mahusiano yako na wengine na kudunisha maendeleo yako ya maisha.



Visababishi Vya Msongo Wa mawazo



Kuna vitu vingi vya kimazingira au kimsukumo vinavyoweza kusababisha uwe na msongo wa mawazo, vitu hivi hutwa “stressors”. Nafikiri msomaji wangu unafikiri kuwa kila kitu kinachokuletea msongo wa mawazo (Stressor) ni kibaya, k**a kubanwa sana na kazi au mahusiano mabaya ya kimapenzi. Stressor ni kitu cho chote kinachodai matumizi ya juu ya uwezo na nguvu zako za mwili. Inawezekana kuwa kikawa kitu kizuri tu, k**a kuoa/kuolewa, kununua nyumba, kujiandaa kwenda chuoni au hata kupandishwa cheo kazini.

Msongo wa mawazo unaweza kutokana na fikra zako binafsi mbali na sababu hizo ambazo ni za nje ye mwili wako. Unaweza kuwa na msongo wa mawazo kutokana na kukifikiria na kukiogopa kitu ambacho kinaweza kutokea au ambacho hakiwezi kutokea au tu ukawa na mawazo chanya kuhusu maisha.

Ni kitu gani kitakupa msongo wa mawazo na kipi hakitakusumbua inategemea sana na namna wewe mwenyewe binafsi utakavyokichukulia kitu kilicho mbele yako, kitu hicho hicho ambacho wewe kinakusumbua, kinaweza kuwa ni burudani kwa mtu mwingine. Kuendesha gari katika foleni toka Mbezi kuingia kazini kwako Posta kunaweza kuwa kero kubwa kwako, wakati kwa mwingine ni fursa yake ya kupata muziki mwororo asubuhi.

Vitu ambavyo vinasababisha msongo wa mawazo ni pamoj na:

Mabadiliko ya maisha
Kazi au shule
Matatizo katika mahusiano
Matatizo ya kifedha
Kubanwa na shughuli nyingi
Watoto na familia
Wasiwasi wa muda mrefu
Tabia ya kuona kila kitu ni kibaya
Kupenda yasiyowezekana
Kutaka kila kitu kiwe sahihi (kikae juu ya mstari) kila wakati
Kutopenda kushauriwa au kubadilika kutokana na hali halisi
Kujidharau mwenyewe kwenye mazungumzo
Msongo wa mawazo unaotokana na majibizano na rafiki yako, au ule unaotokana na msongamano wa magari au wa kuwa na ratiba ndefu na ngumu ya shughuli ni tofauti na msongo wa mawazo wa kuwa na majukumu mengi katika familia. Msongo wa mawazo unaokwenda kwa muda mrefu ni hatari kwa afya na huweza kuvuruga vitu vingi katika mwili wako ukaishia na magonjwa k**a ya high blood pressure, upungufu wa kinga za mwili, kiharusi, ukosefu wa uwezo wa kuzaa au kuzalisha na kuzeeka haraka. Msongo wa mawazo wa muda mrefu huweza kusababisha mfadhaiko (Depression).

Wasiliana nasi kwa tiba na ushauri
+255 652 400 350

JE? Wajua hypotension (presha ya kushuka) Ni ugonjwa ambao mara nyingi huathiri vijana. Inakadiriwa kuwa zaidi ya 30% ya...
19/02/2023

JE? Wajua hypotension (presha ya kushuka) Ni ugonjwa ambao mara nyingi huathiri vijana.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya 30% ya watu zaidi ya 65 wanapata shinikizo la damu.

Hypotension ya muda mrefu ni hali ambayo huathiri wanaume zaidi kuliko wanawake

Hypotension ni, kwa kifupi, hypotension ya arterial. Ni hali ambayo shinikizo la damu la systolic liko chini ya 90 mmHg, wastani wa shinikizo la ateri liko chini ya 60 mmHg, au inaonyeshwa kuwa shinikizo la damu hushuka kwa zaidi ya 40 mmHg ikilinganishwa na maadili ya kawaida ya mgonjwa. Kwa watu ambao wanakabiliwa na shinikizo la damu la muda mrefu,
wasiliana nasi ka tiba na ushauri
+255 652 400 350

JE WAJUA MADHARA YANAYO WAPATA WATU WENYE PRESHAPresha ya kupanda inaweza kupelekea athari kubwa na mbaya sana kwenye af...
17/02/2023

JE WAJUA MADHARA YANAYO WAPATA WATU WENYE PRESHA

Presha ya kupanda inaweza kupelekea athari kubwa na mbaya sana kwenye afya ya mtu. Presha ya kupanda isipotibiwa ama mtu asipofuata masharti ya kuishi na ugonjwa huu madhara makubwa yanaweza kutokea.
1. Kifo,
2. kupasuka kwa mishipa ya damu,
3. kupalalaizi,
4. kuharibika kwa figo na moyo kushindwa kufanya kazi na
5. upofu mtu kutokuona kabisa
6. kupata shambulio la moyo yote haya yanaweza kuwa ni matokeo ya presha ya kupanda pindi isipotibiwa ama mtu asipofata masharti.:-

wasiliana nasi kwa ajili ya tiba na ushauri
+255 652 400 350

MARADHI YA PRESHA YA KUPANDA (HYPERTENSION)Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg. Mara n...
16/02/2023

MARADHI YA PRESHA YA KUPANDA (HYPERTENSION)

Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg. Mara nyingi huwezi kujitambua k**a unapresha hii ya kupanda mpaka pale inapotokea. Na ndio maana huitwa silent killer yaani muuwajiwa siri. Presha ya kupanda isipo tibiwa ama mgonjwa asipofata maelekezo vyema inaweza kusababisha shambulio lamoyo na kupalalaizi.

Presha ya kupanda isipotibiwa ama mgonjwa kufuata maelekezo vyema inaweza kusababisha athari kwenye moyo, kibofu na ubongo. Watu wengi wanakufa duniani kwa sababu ya presha ya kupanad. Wataalamu wa afya wametuwekea staili ambazo zinaendana na ugonjwa huu. K**a mgonjwa atafata maelekezo haya itamsaidia kuishi bila ya kupata presha ama tena k**a ana presha itaweza kupunguza athari na isiwe inatoka mara kwa mara.

NJIA ZA KUKABILIANA NA PRESHA YA KUPANDA (HYPERTENSION)

1.Fanya mazoezi ya mwili na viungo walau kila siku kwa dakika k**a 30 mpaka 60. si lazima uwe unakimbia ama mazoezi magumu ya kutoa jasho, hapana unaweza hata kuamua kutembea kwa miguu kwa mwendo mrefu kwa lisaa limoja na ikawa ni mazoezi tosha.

2.Kula vyakula vilivyo bora kwa afya, ambavyo vinasaidia kupunguza ama kuzuia presha. Kitaalamu mlo huu huitwa DASH yaani Diet Aproaches to Stop Hypertension. Vyakula hivi ni k**a:
A.Matunda
B.Mboga za majani
C.Nafaka nzima
D.Samaki, karanga na korosho
E.Wacha kula vyakula vyenye mafuta mengi

3.Punguza ulaji wa chumvi sana. Kuzidi kwa ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi kunaweza kusababisha presha ya kupanda. Kitaalamu ni kuwa ukila chumvi sana mwili unahitaji kupata maji mengi na hali hii itapelekea presha.
4.Punguza uzito uliozidi mwilini. Rafiki mkubwa wa presha ni kuzidi kwa uzito. Na tambuwa kuwa uzito wa mwili unatakiwa uendane na urefu wa mtu na si umri ama unene alio nao. hivyo tambua. Ili kuhakikisha k**a uzito wako upo sawa unaeza kujipimia kiuno chako. Kikawaida wanaume wnatakiwa viuno vyao visizidi nchi 40 na wanawake viuno vyao visizidi nchi 35.

5.Punguza matumizi ya sigara ama wacha kabisa. Ndani ya sigara kuna kemikali za ni****ne na nyinginezo. Ni****ne ni rafiki sana na presha ya kupanda.
6.Punguza unywaji wa pombe ama wacha kabisa. Unywaji wa pombe sio hatari tu wa afya ya moyo lakini pia unaweza kuleta shida nyingine za kiafya k**a saratani. Hakikisha k**a ni mnywaji unapunguza unywaji ama unawacha kabisa itakuwa ni bora kwako.
7.Hakikisha huna misongo ya mawazo. Misongo ya mawazo inaweza kuwa ni adui mkubwa wa afya ya ubongo. Ni vyema kusamehe wanaokukosea na kuomba msamaha unapo kosea hali zote hizi mbili zitakusaidia kupunguza misongo ya mawazo. Jichanganye na watu na pemba kuwa mbali na fujo.

VYAKULA AMBAVYO HUSAIDIA KUPUNGUZA PRESHA YA KUPANDA AMA HULINDA MWILI DHIDI YA PRESHA YA KUPANDA.
Presha ya kupanda inaweza kupelekea athari kubwa na mbaya sana kwenye afya ya mtu. Presha ya kupanda isipotibiwa ama mtu asipofuata masharti ya kuishi na ugonjwa huu madhara makubwa yanaweza kutokea. Kifo, kupasuka kwa mishipa ya damu, kupalalaizi, kuharibika kwa figo na moyo kushindwa kufanya kazi na kupata shambulio la moyo yote haya yanaweza kuwa ni matokeo ya presha ya kupanda pindi isipotibiwa ama mtu asipofata masharti.:-

Unaweza kupamana na presha kwa kufuata mashari k**a kufanya mazoezi, kula vyakula salama kwa presha, kupunguza misongo ya mawazo, kupunguza kula chumvi, kupunguza uzito, kupunguza ama kuacha sigara na pombe. Miongoni mwa vyakula salama kwa presha ni k**a

1.Mboga za majani ambazo zina madini ya potassium kwa wingi. Madini haya ni mujarabu sana katika kulinda na kuimarisha afya ya moyo. Ulaji wa mboga hizi unaweza kuwa ni njia ya kujilinda na presha ya kupanda. Miongoni mwa mboga hizi ni k**a spinachi

2.Maziwa: maziwa ni katika vyakula vyenye madini ya calcium kwa wingi na pia yana mafuta kwa uchache. Hali zote mbili hizi ni muhimu kwa afya ya moyo.

3.Ndizi; ndizi ni katika matunda yenye madini ya potassium kwa wingi. Ulaji wa ndizi unaweza kuwa ni msaada mzuri kwa kulinda mwili dhidi ya presha ya kupamda.

4.Mayai

5.Samaki aina ya salmon na wanaofanana nao.

6.Ulaji wa mbegu za mimea k**a maboga na alizeti

7.Kitunduu thaumu: unaweza kutumia vitunguu thaumu kwa kula ama kutafuna, ni vyema kufunga mdomo wakati unapotafuna.

8.Makomamanga; unaweza kula tunda hili k**a juisi ama kula kawaida.

13.HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPANDWA NA PRESHA

1.Muweke mgonjwa kwenye sehemu tulivu na iliyopowa
2.Mpunguzie nguo na abakiwe na ngue nyepesi na chache
3.Unaweza kumpepea ana muweke kwenye feni
4.Mpe vitunguu thaumu atafune, na afunge mdomo wakati anatafuna
5.K**a hali itaendelea mpeleke kituo cha afya kilicho karibu au

wasiliana nasi kwa ajili ya tiba na ushauri
+255 652 400 350

Athari za MsongoWaMawazo Kihisia zinamfanya Mtu kuwa na Hofu kupita kiasi, Mfadhaiko, Hisia za kukosa Ulinzi, Kusahau, k...
15/02/2023

Athari za MsongoWaMawazo Kihisia zinamfanya Mtu kuwa na Hofu kupita kiasi, Mfadhaiko, Hisia za kukosa Ulinzi, Kusahau, kushindwa Kufikiri ipasavyo, kukosa Utulivu, na kuwa na Huzuni

Tabia ya Mtu mwenye Msongo wa Mawazo inaweza kubadilika kwa kuanza Kula Chakula kingi au kushindwa Kula baadhi ya Vyakula, kuwa na Hasira, Ulevi na Kujitenga na Jamii.

wasiliana nasi kwa ajili ya ushauri na tiba
0652 400 350

Mtu anayesumbuliwa na Kumbukumbu za Matukio mabaya (Trauma) k**a vile Kubakwa, Ajali, Kufiwa au Kutekwa Nyara, asipopata...
15/02/2023

Mtu anayesumbuliwa na Kumbukumbu za Matukio mabaya (Trauma) k**a vile Kubakwa, Ajali, Kufiwa au Kutekwa Nyara, asipopata msaada wa Ushauri mapema anaweza kupatwa na Ugonjwa wa Akili unaotokana na Msongo wa Mawazo

> Kumbukumbu nyingine ni Talaka, Ujauzito Kuharibika, Kutengana, Kufungwa, Kuuguza, Kufukuzwa au Kukosa Kazi kwa Muda Mrefu

Unatumia njia zipi Kukabiliana au Kumsaidia Mtu mwenye Msongo wa Mawazo?

wasiliana nasi kwa ajili ya ushauri na tiba
0652400350

Address

Ilala
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Msingi wa afya ni kuijua afya yako. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Msingi wa afya ni kuijua afya yako.:

Share