Health_farm_tz

Health_farm_tz Elimika, Hamasika, Chukua Hatua Kabla Mwili Haujachoka!
(1)

Health_farm_tz inapatikana kwenye Instagram, WhatsApp na Facebook kwa jina Hilo hilo.karibuni Sana kwaajili ya elimu ya afya ya binadamu.

10/06/2026

Katika mahojianao yaliyofanywa na na Daktari bingwa wa uzazi na magonjwa ya wanawake na mkuu wa kitengo cha uzazi pandikizi kutoka hospitali ya taifa Muhimbili (MNH) Dr Matlida Ngarina anaeleza kuwa:-

wakati wa mchakato wa uzazi pandikizi (IVF) Kuna baadhi ya wanawake hukabiliwa na ukosefu wa mayai licha ya kuchomwa sindano za dawa ya kuchochea uchavushaji wa Mayai.

Ametaja pia kuna baadhi ya wanawake wanaweza kutoa mayai na kufanikiwa kurutubishwa na mbegu za baba lakini vijusi vinavyozaliwa hapo vinakuwa havina ubora stahiki wa kutengeza kiumbe kamili.

Hii imekuwa ni moja ya changamoto kubwa inayowakabili wanawake wengi sana wanaotazamia kufanya IVF k**a njia pekee iliyobaki kwa ajili ya kutimiza ndoto ya kuitwa mama au baba.

Kwa Mujibu wa Dr Ngarina, amesema unaweza kupata Mayai na kurutubisha vizuri lakini vijusi visiwe na ubora,

Na cha msingi ni kwamba swala la kupata mtoto linategea zaidi pande zote mbili baba na mama hivyo afya ya uzazi ni muhimu kwa jinsia zote mbili.

ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

CREDIT: Full Video Ipo YouTube

06/06/2026

Baada ya hedhi kukoma (menopause) kiwango cha hormone muhimu ya estrogen hushuka kwa kasi hali ambayo huleta mabadiliko ya ghafla katika mwili wa mwanamke.

Moja kati ya athari muhimu zaidi ni mabadiliko katika ujazo (density) wa mifupa ya mwanamke,

kupungua kwa kiwango cha hormone ya estrogen husababisha mifupa kuwa dhaifu na laini hali hii kitaalamu inajulikana k**a Osteoporosis.

Halii hii huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa kwa urahisi mno isivyo kawaida, na ndio maana wanawake wengi umri wa kukoma hedhi au waliokwisha koma hedhi hukabiliwa na changamoto za mifupa.

Kuna njia kadhaa za kupunguza hatari hii ya kuvunjika kwa mifupa na moja wapo ni matumizi ya virutubisho muhimu vya madini ya calcium na vitamin D ambavyo husaidia kujenga mifupa na kupunguza kasi ya mifupa kudhoofika k**a alivyoeleza Dr Ngarina.

N.B
Kwenye Video ni Dr Matilda Ngarina, Bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi na mkuu wa kitengo cha uzazi pandikizi kutoka Hospital ya Taifa Muhimbili (MNH) akizungumza kuhusu athari na dalili za Hedhi kukoma (menopause) katika tukio liloandaliwa na BarbaraHassan foundation.

ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

Credit:

04/06/2026

Katika mahojiano ya kipindi cha cha UTV na Dr Boniface Charles ambae ni daktari bingwa wa wanawake na uzazi kutoka hospitali ya Tanzanite ametaja Vipodozi K**a moja ya vyanzo vya hormonal imbalance kwa wanawake.

Aidha Viambato K**a phthalates, parabens, BPA, Triclosan, oxybenzone n.k ambavyo vinapatikana kwenye Vipodozi na bidhaa nyingi za urembo na usafi wa mwili vinahusishwa sana na muingiliano au mvurugiko wa hormones.

Matumizi holela au ya Mara kwa Mara ya bidhaa hizi inatajwa K**a chanzo cha Tatizo la hormonal imbalance kwa baadhi ya wanawake.

Je unafahamu Vipodozi unavyotumia vinaviambato gani ?

ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

VIDEO:

Matumizi holela ya Vipodozi na bidhaa za urembo zinaweza kuwa chanzo cha hormonal imbalance kwa wanawake wengi!ELIMIKA, ...
04/06/2026

Matumizi holela ya Vipodozi na bidhaa za urembo zinaweza kuwa chanzo cha hormonal imbalance kwa wanawake wengi!

ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

04/06/2026

Hospitali za Umma zimekuwa zikitoa msamaha wa Matibabu kwa ma elfu ya Watanzania, Je umewahi kusamehewa gharama za Matibabu katika Hospitali gani ya umma?

🇹🇿

03/06/2026

Mwanaume kuota matiti (breast) k**a mwanamke kitaalamu inaitwa gynaecomastia.

Hali hii husababishwa na mabadiliko ya homoni hasa ongezeko la homoni ya k**e ya estrogen kuliko homoni ya kiume testosterone wakati wa balehe, Hali hii huisha yenyewe baada ya uwiano wa homoni kukaa sawa.

Wakati mwingine hali hii husababishwa na uzito mkubwa(Kitambi), Ugonjwa wa Ini, Figo, tezi ya thairoid, Uvimbe au tatizo kwenye korodani au matumizi ya baadhi ya dawa, Ulevi wa pombe, na bangi.

Hali hii inaweza kuathiri sehemu zote mbili za kifua au upande mmoja Tu.

Ingawa hali hii haina madhara lakini wakati mwingine inaweza kuchangia Tatizo la upungufu wa Nguvu za kiume!

ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

🇹🇿

Sio tu kwamba wanawake wanakuwa na hatari ya kupata presha kuliko mwanaume baada ya hedhi lakini pia ikitokea amepata in...
03/06/2026

Sio tu kwamba wanawake wanakuwa na hatari ya kupata presha kuliko mwanaume baada ya hedhi lakini pia ikitokea amepata inakuwa ni ngumu kuidhibiti.

Wanawake wenye umri Kati ya 61-64 wako katika hatari kubwa mno ya kupata presha kuliko wanaume wenye umri sawa.

Mtindo wako wa maisha katika miaka yako ya 20 - 30 ndio utaamua maisha yako ya miaka 50+.

ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

03/06/2026

Dalili za Saratani ya kibofu zinafanana na dalili za UTI au kuvimba kwa tezi dume.

Endapo unatibu UTI isoyopona unatakiwa kufanyiwa uchunguzi zaidi kwasababu inaweza kuwa ni dalili ya Saratani ya kibofu cha mkojo.

Lakini pia UTI sugu isiyoisha inaweza kupelekea saratani ya kibofu cha mkojo au figo kufeli.

Endapo unateseka na maambukizi ya kujirudia rudia kwenye njia ya mkojo ni vyema kwenda kufanya uchunguzi zaidi.

ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

🇹🇿

02/06/2026

Je wajua?
Baada ya miaka 35 -40 uwezo wa figo kufanya kazi unaanza kupungua kwa 1% kila mwaka!

Inakadiriwa kuwa Mpaka kufikia miaka 70 figo zako zitakuwa zimepungua ufanisi kwa 30%.

ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

🇹🇿

02/06/2026

Hii inaitwa Genu Recurvatum ni hali ambapo goti hupinda kuelekea nyuma zaidi ya kiwango cha kawaida wakati wa kusimama au kutembea.

Kwa kawaida goti hupinda upande wa nyuma kwa nyuzi 0-10 tu lakini kwenye Hali hii huzidi kiwango.

Hali hii inaweza kuwa ya kuzaliwa nayo au kusababishwa na udhaifu wa misuli, kulegea kwa mishipa ya goti, majeraha, au baadhi ya magonjwa ya mfumo wa neva.

Dalili zake zinaweza kujumuisha maumivu ya goti, kutembea kwa shida, na kuhisi goti kutokuwa imara.

Matibabu hutegemea chanzo chake na yanaweza kujumuisha mazoezi ya tiba ya viungo (physiotherapy), matumizi ya vifaa vya kusaidia goti, au matibabu mengine ya upasuaji maalumu.

Ukiona goti linapinda nyuma isivyo kawaida, pata ushauri wa mtaalamu wa afya mapema sio kukimbilia kwa waganguzi🥸

ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

🇹🇿

Address

Gongo La Mboto
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Health_farm_tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Health_farm_tz:

Share