21/01/2026
Kutapika hupelekea mtoto kupoteza maji mwilini, kitu ambacho ni cha hatari mnoo. Kutapika husababishwa mara nyingi na maambukizi ya virusi vya Rota. Virusi hivi havina tiba (dawa)
Kumpatia mtoto mchanganyiko safi wa ORS husaidia kuzuia hatari ya kuishiwa maji mwilini. Kumpa ORS mtoto anayetapika ni changamoto mnoo lkn unaweza fanya hivi;
- mpatie kidogo kidogo kwa kijiko cha chai (5mls), vijiko 2-4 kila baada ya dk 5-10
- unaweza mpatia iliyo ya baridi ili kupunguza uwezekano wa kutapika
- usikimbilie kumpatia chakula kingine isipokua maziwa ya mama kwa mtoto anayenyonya.
- Subiri walau masaa 3-4, ndipo uanze kumpa vitu vya maji maji k**a juice ya apple, chungwa etc. Epuka maziwa.
- Subiri walau saa 6–8 tangu atapike kwa mara ya mwisho kabla ya kumpa kwa kiwango kidogo vyakula vyepesi k**a ndizi, wali, au viazi vilivyopondwa. Epuka tumbo kujaa.
- Ikitokea ametapika tena subiria nusu saa ipite kisha anza tena hatua za mwanzo.
Karibu AHP Healthcare Polyclinic kwa huduma bora.
Tunapokea pia bima za NHIF, Strategis na Jubilee.
Tunapatikana Kilwa Road, Mbagala Zakiem, jirani na ofisi za TRA Mbagala.
📱0764427947