25/10/2023
Madhara Yatokanayo Na PID Au VISABABISHI
PID ambayo Haikupata Tiba Inaweza kusababisha Makovu NA Vifuko Vyenye Maji Yenye Wadudu KWENYE Mkondo WA Nnjia YA Uzazi YA Mwanamke. Vitu Hivi Vinaweza Kusababisha Madhara YA Kudumu KWENYE VIUNGO VYA UZAZI.
Madhara Yanayoweza KUTOKEA NI PAMOJA NA:
✍️Mimba nje ya mirija (ectopic pregnancy): PID ndiyo sababu kubwa ya mimba kutunga nje ya kizazi. Mimba huweza kutunga nje ya kizazi endapo PID imesababisha makovu ndani ya mirija ya uzazi. Makovu haya husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye nyumba ya uzazi. Badala yake yai hunata ndani ya mirija ya uzazi . Mimba nje ya kizazi husababisha utokaji wa damu usio wa kawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke.
✍️Ugumba: Uharibifu wa viungo vya uzazi huweza kusababisha ugumba – kushindwa kupata ujauzito. Kadiri unavyozidi kupata PID mara nyingi zaidi, ndivyo hatari ya ugumba inavyozidi. Kuchelewa kupata tiba ya PID kunaongeza hatari ya ugumba.
✍️Maumivu sugu ya nyonga: PID inaweza kusababisha maumivu ya nyonga yanayoweza kudumu kwa miaka mingi. Makovu ndani ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kuleta maumivu wakati wa kujamiiana na wakati yai linadodondoshwa (ovulation).
✍️Tube-ovarian abscess: PID huweza kusababisha kutunga kwa usaha na kufanya majipu ndani ya njia ya uzazi. Mara nyingi majibu haya hutokea ndani ya mirija ya uzazi na ovari, ingawa huweza kuota ndani ya nyumba ya uzazi na shingo ya kizazi. K**a tiba haitatolewa, unaweza kupata maambukizo hatarishi kwa maisha.