Amana Hospital Ilala

Amana Hospital Ilala Karibu katika Ukurasa Rasmi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana

MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 23 ATOLEWA UVIMBE WENYE KILO 12 KWENYE KIZAZIHospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana imefanikiwa ...
02/09/2026

MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 23 ATOLEWA UVIMBE WENYE KILO 12 KWENYE KIZAZI

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana imefanikiwa kufanya upasuaji wa kuondoa uvimbe wenye uzito wa takribani kilo 12 kwenye kizazi cha mwanamke mwenye umri wa miaka 23 uliomtesa kwa muda mrefu.

Akizungumza wakati wa upasuaji huo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Afya ya Uzazi, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dkt. Musa Stambuli amesema kuwa uvimbe huo ulikuwa kwenye mayai ya upande wa kulia ambao umemtesa kwa zaidi ya miaka miwili.

Akuzungumzia kuhusu dalili za uvimbe huo amesema kuwa dalili za uvimbe huo mara nyingi zinafanana na zile za mfumo wa chakula ambapo mgonjwa anaweza kuhisi tumbo kujaa kila wakati, kupata maumivu ya mara kwa mara ya tumbo, kupata haja ndogo na kubwa mara kwa mara au kushindwa kupata haja kubwa k**a kawaida.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa ni vyema mtu anapoona dalili hizo kuwahi hospitali kufanyiwa uchunguzi ili kubaini chanzo cha uvimbe huo kwa kuwa endapo tu atachelewa anaweza kupelekea kupata saratani ya kizazi

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dkt. Bryceson Kiwelu, Menejimenti na Wafanyakazi wote tunakupongeza ...
01/09/2026

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dkt. Bryceson Kiwelu, Menejimenti na Wafanyakazi wote tunakupongeza kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunakutakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yako mapya ya kulitumikia Taifa.

HOSPITALI YA AMANA YAPOKEA UGENI KUTOKA SINGIDA RRHWatumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkaoa wa Singida leo tarehe 01Sept...
01/09/2026

HOSPITALI YA AMANA YAPOKEA UGENI KUTOKA SINGIDA RRH
Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkaoa wa Singida leo tarehe 01Septemba, 2026 wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana kwa lengo la kujifunza na kubadilisha uzoefu katika utoaji huduma.

Watumishi hao wametembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Idara ya Radiolojia, Idara ya Magonjwa ya nje (OPD), Kitengo cha Ustawi wa Jamii, Famasi, Idara ya Mipango, Kitengo cha Habari na Mawasiliano pamoja Wodi ya Watoto wachanga.

Akizungumza na wageni hao Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dkt. Japo Lukali amewapongeza watumishi hao kwa kutembelea Hospitali ya Amana na kusema kuwa hospitali hiyo ni moja ya hospitali ambayo inaongoza katika kutoa huduma bora na inahudumia wagonjwa wengi zaidi.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa Hospitali ya Amana imefanikiwa kufanya vizuri kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya viongozi pamoja na watumishi wake kuanzia ngazi ya juu mpaka ngazi ya chini.

“Watumishi wa Hospitali ya Amana tunafanya kazi kwa upendo na tunaishi k**a familia moja na kila mteja anayefika Amana kupata huduma atahudumiwa bila kikwazo chochote na kwetu sisi wateja wote ni sawa hivyo wanahudumiwa kwa usawa”Amesema Dkt. Lukali

Hospitali ya Amana imekuwa ikipokea wageni kutoka hospitali mbalimbali hapa nchini ambao wanakuja kujifunza na kubadilishana uzoefu katika kutoa huduma bora zinazokidhi matarajio ya wateja.

Msanii wa Filamu nchini Bw. Othman Njaidi maarufu kwa jina la Patrick Kanumba ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ama...
27/08/2026

Msanii wa Filamu nchini Bw. Othman Njaidi maarufu kwa jina la Patrick Kanumba ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana na kutoa zawadi kwa baadhi ya wanawake waliojifungua Hospitalini hapo ikiwa ni sehemu ya kuonyesha upendo, faraja na kuwapongeza wanawake katika kusherekea siku yake ya kuzaliwa.

Akizungumza na kinamama hao Kanumba amewapongeza na kuwapa moyo katika kipindi hiki cha malezi na kusema kuwa wanawake ni watu wa muhimu katika kujenga taifa.

Pamoja na hayo ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wasanii wengine kujitokeza kugusa maisha ya wanawake kwakuwa kufanya hivyo ni ishara ya kuwajali na kutambua umuhimu wa jukumu walilolibeba katika familia na jamii.

Patrick Kanumba ameacha tabasamu na furaha kwa akina mama hao, huku akionesha kuwa upendo na kujali vinaweza kuleta faraja kubwa kwa mtu anayepitia kipindi muhimu cha maisha.

HOSPITALI YA AMANA YAPONGEZWA KWA UBORESHAJI WA MIUNDO MBINUHospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana imepongezwa kwa kuendelea k...
26/08/2026

HOSPITALI YA AMANA YAPONGEZWA KWA UBORESHAJI WA MIUNDO MBINU

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana imepongezwa kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya.

Pongezi hizo zimetolewa na wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana walipotembelea hospitali hiyo kwa lengo la kukukagua na kuangalia ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma unaoendelea hospitalini hapo.

25/08/2026
JESHI LA MAGEREZA MKOA WA DAR ES SALAAM WATOA MSAADA NA KUCHANGIA DAMU HOSPITALI YA AMANAMaafisa wa Jeshi la Magereza Mk...
24/08/2026

JESHI LA MAGEREZA MKOA WA DAR ES SALAAM WATOA MSAADA NA KUCHANGIA DAMU HOSPITALI YA AMANA

Maafisa wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 24 Agosti, 2026 wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana na kutoa msaada wa vitu mbalimbali Pamoja na kuchangia damu kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.

Akipokea msaada huo Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dkt. Bryceson Kiwelu amelipongeza jeshi hilo kwa kuona umuhimu wa kutembelea hospitali hiyo na kusema kuwa mahusiano baina yao yataendelea kuboreshwa zaidi ili kuhakikisha wagonjwa wa;iolazwa hospitalini hapo wanaendelea kupata huduma baora zaidi.

"Hospitali ya Amana tumekuwa tukishirikiana kwa ukaribu na jeshi la magereza na kila wanapokuja hospitanini hapa tunahakikisha kuwa wanahudumiwa kwa wakati bila usumbufu wowote tumekuwa tukiwapa kipaumbele katika kila eneo la kutolea huduma"amesema Dkt. Kiwelu

Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam ACP Robert Masali amesema jeshi la magereza kazi yake kuu ni kuhakikisha inatoa uhifadhi salama kwa wafungwa na mahabusu wote na usalama huo unaenda sambamba na kuwa na afya bora ndio maana wameona kuna umuhimu wa kutembelea hospitali hiyo ili kuendelea kuwaunga mkono wagonjwa wanaohudumiwa hospitalini hapo.

Msaada uliotolewa ni pamoja na Viti mwendo, Maziwa ya Watoto wachanga, Taulo za Watoto, mafuta ya Watoto wachanga pamoja na majora ya mashuka ya wagonjwa,

AMANA HOSPITALI YATEMBELEWA NA WAGENI KUTOKA IRINGA NA GEITA RRHHospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana imepokea ugeni kutoka H...
19/08/2026

AMANA HOSPITALI YATEMBELEWA NA WAGENI KUTOKA IRINGA NA GEITA RRH

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana imepokea ugeni kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na Geita kwa ajili ya ziara ya kujifunza namna ya kutoa huduma katika maeneno ya kimkakati k**a vile huduma za Bima, Mionzi, huduma za dawa na vifaa tiba, huduma za uuguzi na huduma za ustawi wa jamii, Watoto sambambana na kujifunza namna bora ya kuhudumia watu mashuhuri na viongozi (VIP)

Address

Ilala
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Amana Hospital Ilala posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Amana Hospital Ilala:

Shortcuts

Share