06/05/2026
Najua unayopitia muda mwingine hauyasemi kwa kila mtu. Unatabasamu, unaendelea na majukumu, lakini ndani kuna maumivu ambayo si rahisi kuyaeleza. Mungu anayajua hayo yote. Anafahamu machozi unayoyafuta kimya kimya, na zile jitihada unazofanya kuhakikisha ndoto yako inatimia. Kusubiri kwako hakumaanishi Mungu amekusahau.
Ninapoongea hivi, ninaongea na wewe moja kwa moja. Yule mwanamke anayejitahidi kila siku kubaki imara, hata pale nguvu zinapopungua. Najua umejaribu, umeomba, umechoka kusikiliza maneno ya watu, lakini bado unaendelea. Naomba ujue, thamani yako haipimwi kwa kile ambacho bado hujakipata. Safari yako bado ni halali, na imani yako bado ina nafasi mbele za Mungu.
Naomba nikukumbushe hili kwa upole: pamoja na hatua zote unazochukua, pamoja na dawa, ushauri na juhudi zako imani ibaki mbele. Mungu hafanyi makosa, na muda wake hauchelewi. Mtoto ni mpango wa Mungu, na hata katika kipindi cha kusubiri, maisha yanaendelea, na wewe bado una nafasi kubwa ndani ya mpango wake.
Zingatia endelea kuimarisha Afya yako ya uzazi na kutibu changamoto ya mfumo wa Uzazi, ipo siku na wewe utaitwa Mama
kwa ushauri na matibabu zaidi wasiliana nasi what's app, Call 📞📞📞 +255 676 768 478
k**a kaulimbiu yetu inavyosema "Furaha yako ni furaha yetu"