08/05/2026
Training on Seaweed Value Addition for 78 Women in Rural Zanzibar. Alhamdulillah kila kitu kimeenda sawa na tulianza na tumemaliza salama our 5-Day Training from 4-8 May, 2026 thanks to our funders and in Colloboration with ZMBF
——
Leo tumeanza mafunzo ya uongezaji thamani wa mwani kwa wakulima wanawake 78 kupitia mradi wa Mpango wa Pamoja wa Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Wanawake wa Vijijini unaotekelezwa chini ya ufadhili wa IFAD.
Washiriki kutoka Mkoa wa Kusini watajifunza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na mwani, ikiwemo mbolea za shambani na vipodozi, kwa lengo la kuongeza ubora, ushindani wa masoko, na kipato.
Moja ya changamoto wanazokabiliana nazo ni hasara wanazopata pindi mnunuzi asipopatikana au kushindwa kujadiliana bei kutokana na utegemezi wa mnunuzi mmoja. Mafunzo haya yanalenga kupanua wigo wa masoko na kuongeza thamani ya zao la mwani, ili kuwapa wakulima uhuru zaidi wa kiuchumi na kuongeza kipato chao.
📍Maruhubi, Unguja – Shear Illusions Industries
📆 4 May 2026