31/03/2025
JINSI YA KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA UGONJWA WA KISUKARI.
Kisukari ni ugonjwa hatari ambao unaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya yako.
Kwa bahati mbaya, idadi ya watu wanaougua kisukari inaongezeka kila mwaka, hivyo ni muhimu kuchukua hatua za kuzuia ugonjwa huu mapema kabla ya kujitokeza
Idadi ya watu wenye Ugonjwa wa Kisukari(diabetes) Duniani iliongezeka kutoka Million108 mwaka1980 mpaka kufikia Watu million 422 kwa mwaka 2014, Je k**a Idadi inaongezeka kila mwaka leo hali Ipoje?
Pia ugonjwa huu wa Kisukari ni chanzo kikubwa cha matatizo mengine k**a vile;
● Upofu wa macho(blindness),
● Tatizo la Figo kushindwa ●kufanya kazi(kidney failure),
● Shambulio la moyo(heart attacks),
● Tatizo la kiharusi(stroke)
● Pamoja na Tatizo la watu Kukatwa MIGUU
📌 Kuna hatua kadhaa za kufuata ili kupunguza hatari ya kupata kisukari, na makala hii itakusaidia kujifunza jinsi ya kufanya hivyo.
1.Punguza au Acha kula vyakula vya wanga au carbohydrates. (Vyakula vilivyo kobolewa )
Vyakula vyenye kiwango cha juu cha sukari, wanga, na mafuta yasiyofaa ni hatari kwa afya yako na vinaweza kuongeza hatari ya kupata kisukari.
Kwa hiyo, ni muhimu kuzingatia ulaji wa vyakula sahihi, k**a vile matunda, mboga mboga za majani, protini, na wanga unaochujwa.
2. Fanya Mazoezi ya mara kwa mara
Mazoezi ya mara kwa mara yanasaidia kupunguza hatari ya kupata kisukari,
Jaribu kufanya mazoezi kwa angalau dakika 30 kwa siku, angalau siku tano kwa wiki.
Mfano wa mazoezi haya ni pamoja na
●Mazoezi ya kutembea,
●kukimbia,
●kuogelea,
●Kuendesha baiskeli,
●Pamoja na yoga.
3. Punguza Unene wa mwili
Unene wa mwili ni hatari kwa afya yako na inaweza kuongeza hatari ya kupata kisukari. Kwa hiyo, ni muhimu kupunguza uzito wako kwa kupitia lishe bora na mazoezi ya mara kwa mara.
4. Tumia Maji ya kutosha
Unywaji wa maji wa kutosha ni muhimu kwa afya yako na inaweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata kisukari. Jaribu kunywa angalau lita 2.5 ya maji kwa siku.
5. Punguza Matumizi ya Pombe
Matumizi ya pombe ni hatari kwa afya yako na inaweza kuongeza hatari ya kupata kisukari. Kwa hiyo, ni muhimu kupunguza matumizi ya pombe au kuepuka kabisa matumizi yake.
✍️Ni muhimu kufuata hatua hizi k**a njia ya kudumu ili kuhakikisha afya yako na kuepuka hatari ya kupata kisukari.
🥦K**a umeshapata ugonjwa huu upate tiba za mimea asilia zenye uwezo wa kushusha sukari na kuwa katika kiwango sahihi kinachotakiwa
KWA USHAURI NA TIBA JUU YA CHANGAMOTO YA KISUKARI TUWASILIANE KWA NAMBA 0741438383