12/05/2026
TANZANIA YATOA UZOEFU WAKE KATIKA UFUATILIAJI WA MASUALA YA LISHE NCHINI.
Tanzania imepata fursa ya kuungana na mataifa mengine 22 , kutoka katika nchi za Africa Magharibi na Kati na kutoa uzoefu wake katika kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa musuala ya lishe nchini.
Hayo yamejiri katika mkutano wa Mawaziri wa Kikanda uliofanyika nchini Togo, kuanzia tarehe 11/5/2026 na unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 13 Mei 2026, mkutano huo umeenda na kauli mbiu ya βWekeza katika Lishe kwa kuzingatia Miaka ya Mwanzo ya Ukuaji wa Mtotoβ umehusisha nchi za Magharibi na Kati ya Afrika ambao umeandaliwa na Bank ya Dunia.
Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Bi. Deborah Charwe ni miongoni mwa wataalamu waliowasilisha mada katika mkutano huo ambapo amewaeleza washiriki faida ambazo Tanzania kupitia Taasisi yake ya Lishe imezipata kupitia usimamizi na utekelezaji wa Kadi Alama Jumuishi ya Lishe.
Katika mkutano huo jumla ya wajumbe 345 kutoka katika nchi 22 za Magharibi na Kati ya Africa wamehudhuria mkutano huo wenye lengo la kujadili na kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia kupunguza tatizo la utapiamlo kwa nchi husika.
TFNC