01/03/2023
UJUE UGONJWA WA KIHARUSI,DALILI ZAKE PAMOJA NA TIBA Yake.
STROKE (KIHARUSI)
Kiharusi ni ugonjwa ambao husababishwa na kufa kwa cell za ubongo.
AINA ZA KIHARUSI
Kuna aina mbili za kiharusi.
I) ISCHEMIC
II) HEMORRHAGIC
I) ISCHEMIC
Hiki ni kiharusi ambacho husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu baada ya mishipa hiyo kujaa mafuta(cholesterol) na kusababisha damu kutofika vizuri kwenye ubongo.
II) HEMORRHAGIC
Hiki ni kiharusi ambacho husababishwa na kupasuka kwa baadhi ya mishipa ya damu kwenye ubongo na kusababisha damu kusambaa kwenye ubongo na kusababisha mmbonyeo ndani ya ubongo.
Watu wenye presha wako kwenye hatari kubwa ya kupata kiharusi na kiharusi huweza kuuwa kwa haraka sana.
Kiharusi kiko hivi, k**a ubongo wa upande wa kulia ndio utakaoathirika basi utaparalaizi upande wa kushoto,na k**a ubongo utaathirika upande wa kushoto basi utaparalaizi upande wa kulia.
DALILI ZA KIHARUSI
1.kupooza mguu au mkono.
2.Kuchanganyikiwa kupata shida kuongea