09/06/2026
SOMA SOMO HAPA UENDELEE KUJIFUNZA na Dr. Ebby 0757991560
Kuna watu wakisikia mambo ya afya wanasema..
“Acha kujisumbua, wote tutakufa tu.”
Ni kweli.
Lakini kuna tofauti kubwa kati ya kuishi na kuendelea kuvuta pumzi.
Gari ukifanya service kwa wakati, ukaweka oil nzuri, ukaweka genuine parts, mara nyingi litakupa performance nzuri na litadumu zaidi.
Ndiyo, siku moja linaweza kuharibika.
Lakini si sawa na gari ambalo service ya kuungaunga, linaendeshwa ovyo na kila taa ya tahadhari inapowaka dereva anaipuuza.
Mwili wetu nao uko hivyo.
Kula vizuri, kulala vizuri, kunywa maji ya kutosha, kufanya mazoezi na kupunguza msongo wa mawazo hakutufanyi tuishi milele.
Lakini kunatusaidia kuishi miaka mingi yenye afya, nguvu na furaha.
Afya si tu kuongeza miaka kwenye maisha.
Ni kuongeza uhai ndani ya miaka hiyo.
Mwisho wa yote, Mungu ndiye mpaji wa uzima na afya. Lakini katika kanuni alizoweka, moja ya njia za kutunza zawadi hiyo ni kuishi kwa mtindo unaouheshimu mwili aliotupa.
Usikate tamaa kwa sababu tu siku moja utakufa.
Ishi vizuri leo.
Ishi kwa afya leo.
Ishi kwa kusudi leo.
ISHI!🫶
Somo hili likawe Funzo na lenye thamani kwako.... K**A UMENIELEWE TUANDIKIE (NIATAILINDA AFYA YANGU)
Health Community care Tunajali na kuthamini afya yako.. sisi Tunapatikana Mwanza eneo linaitwa Mkolani jirani na Ghorofa la Family corner.. k**a una changamoto yoyote ya kiafya Karibu tukusaidie kwa ushauri na matibabu ya uhakika kupitia mimea asili na vyakula lakini tutakusadia mtindo sahihi wa maisha... Karibuni wake kwa waume🤝Dr. Ebby 📱0757991560👉 face book follow . Ebby Herbal.. on Instagram
Usichoke kujifunza, endelea kujifunza