19/05/2026
📌*Mwamko wa uwekezaji ni suala zuri sana kwangu hasa kwa Watanzania wenzangu.*
Nilikuwa nafuatilia mkutano wa wanahisa wa CRDB, katika mengi niliyoyaona, nilivutiwa zaidi kumuona *Clement Mzize* Mchezaji wa *Young Africans SC* k**a mwanahisa wa CRDB.
Hii ni kubwa sana ni k**a anawaamsha wachezaji wenzake pia wawekeze kwenye soko la Hisa.
Wengi hukimbilia kununulia magari ya kifahari na kusahau kuwa maisha ya mpira ni mafupi sana na ukicheza kete zako vibaya basi utateseka sana baada ya kustaafu.
Ikumbukwe kuwa wachezaji wengi hasa wa team ndogo ambazo sio dominant mishahara yao ni kidogo na k**a hawatafanya uwekezaji wakati wakiwa active viwanjani basi inaweza kuwa mateso mbeleni.
Wewe umeanza kuwekeza kwenye Hisa?
Umeanza kuwekeza kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja k**a UTT Amis?
Kwanini hujaanza kuwekeza?
Unajua unaweza kujitengenezea kiinua mgongo kwa kufanya uwekezaji nje na mifuko rasmi ambayo unawekewa mafao yako?
Jifunze uwekezaji.
Kisha anza kuwekeza.
*See You At The Top* 🕵🏽