01/10/2026
TEZI DUME NI NINI?
Tezi dume (Prostate) ni tezi inayopatikana kwa mwanaume, chini ya kibofu cha mkojo na kuzunguka sehemu ya mrija wa mkojo. Huwa na nafasi muhimu katika mfumo wa uzazi wa mwanaume.
🔹 AINA/CHANGAMOTO KUU ZA TEZI DUME 1️⃣ BPH – tezi dume kuongezeka ukubwa bila kuwa saratani. 2️⃣ Prostatitis – kuvimba kwa tezi dume, mara nyingine kutokana na maambukizi. 3️⃣ Saratani ya tezi dume – ukuaji wa seli zisizo za kawaida kwenye tezi dume.
🔹 SABABU/VICHOCHEZI • Kuongezeka umri
• Maambukizi au uvimbe wa tezi dume
• Mabadiliko ya homoni
• Historia ya familia, hasa kwa saratani ya tezi dume
• Sababu nyingine za kiafya zinazoweza kuongeza hatari
🔹 DALILI ⚠️ Kukojoa mara kwa mara, hasa usiku
⚠️ Kuanza kukojoa kwa shida
⚠️ Mkojo kutoka kwa kusuasua au kwa nguvu ndogo
⚠️ Kuhisi kibofu hakijaisha baada ya kukojoa
⚠️ Maumivu au kuungua wakati wa kukojoa
⚠️ Damu kwenye mkojo au shahawa
⚠️ Maumivu kwenye nyonga, mgongo wa chini au sehemu za siri — kulingana na chanzo
🔹 MADHARA YAKIACHWA BILA KUDHIBITIWA ❗ Kuziba kwa mkojo
❗ Maa